Chacha Maboto, Mbunge wa Bunda (CCM): Lugha ya kwenye Mkataba wa DP World sikuielewa, mnisamehe

We mbunge Bora ungepiga kimya unajiaibisha Sana,yaani unakaa kwenye chombo Cha maamuzi halafu kumbe ni maimuna! Looooooh! Na kesi tunazoshindwa huko nje na kulipa mapesa ya faini kumbe mfumo ndiyo huu huu.kwa hivyo kumbe akina mwabukusi wako sahihi!
Siyo wabunge wote waliukubali ila walisubiri muda muafaka waseme ukweli. Huyu dhamira imemsuta akasema ya moyoni.
 
Kuna watu humu hamna hekima. Mnamshambulia wa nini wakati yeye kaelezea ukweli ulivyo??? Wanasheria wa bunge wapo na wao walielimishwa mkataba hauna shida. Na tunasema haina gogoro kabisa.
Wanasheria gani Hawa wanaojitetea kwenye mahakama za kimataifa kuwa wameamka vibaya ndio maana hawaelewi kinachoulizwa mahakamani.
 
Kiukweli tulia hapa aliwaburuza wabunge na alichagua kabisa watu wa kuchangia ,wale watu wa maana waliwekwa pembeni
Itakuwa alifuata maagizo kutoka kwenye Mhimili uliojichimbia. Si unamwona leo akili ilivyokaa sawa akisikiliza waraka.
 
Tec kama wana mtandao mkubwa basi watusaidie tupate KATIBA MPYA waache hizi mbwembwe
Hapana ndugu, hili la kugawa rasilimali ya kiuchumi bila hata ubia ni kubwa kuliko katiba mpya. Huu mkataba ni utumwa mambo Leo.
 
Hapana ndugu, hili la kugawa rasilimali ya kiuchumi bila hata ubia ni kubwa kuliko katiba mpya. Huu mkataba ni utumwa mambo Leo.
Unaweza kuwa hujui,KATIBA MBOVU ndio kiini cha yote haya yanayotendeka leo
 
Tanzania ina katiba ya ajabu sn, yani unatakiwa kujua kusoma na kuandika tu unaingia mjengoni kutunga sheria mamaweeeeeeeeee hatari hii. Si huwa naskia sheria ni profession Sasa hao gumbaru sheria wanaijulia wapi. Bora huyu aliekiri, Sasa atubu atoke mjengoni vinginevyo ataendelea kuchuma dhambi kwa sababu ya njaa ya tumboni.
 
Wabunge wengi wa CCM watakuja kusema ukweli. Wengi waliburuzwa. Kuna yule waliyepishana na Msukuma na kuambiwa alikuwa waziri na hakuna kipya alicholeta. Wote hawa hawakukubaliana na mkataba huu ila walishindwa wafanye nini.
 
IDARA YA HABARI MAELEZO ikihamishiwa Madhabahuni ni Hatari kwa UMOJA wa Taifa letu tukufu
 
Mbona kuna chupa yenye bia ndani yake, kanisa linahusika na bia?
20230402_010117.jpg
 
Back
Top Bottom