GAGL
JF-Expert Member
- Aug 5, 2010
- 390
- 395
Nimeamua kuwaomba CDM japokuwa mimi ni CCM damu kwa kuwa wabunge wetu wa CCM wamekuwa ni watu wa kutetea chama ili kulinda nafasi zao wakati si ccm iliyowapeleka hapo bali ni wapiga kura wao ambao ndo sisi, kwa maana hiyo aidha hawajui wajibu wao au wamesahau wajibu wao kwamba kazi yao ni kuishinikiza serikali kutatua kero za wananchi. Ombi langu ni kama ifuatavyo, tunaiomba CDM kuitisha maandamano ya amani mapema kabla ya bajeti mpya ya 2011- 2012 haijapitishwa, kuishinikiza serikali itenge fungu kwa ajili ya kuwawezesha wajasiriamali wadogo hasa wanaohitimu vyuo na wenye mawazo ya kijasiriamali kama mimi ili waweze kukopeshwa na kuanzisha au kuendeleza miradi waliyobuni. Naona hili linawezekana kwa kuwa mwaka jana mhe. Rais aliipatia TWB, Tanzania Women Bank shilingi bilioni mbili kuiwezesha, na hii ilikuwa nje ya bajeti ya 2010 - 2011. Sasa kwa mtazamo wangu nadhani kwamba TWB si zaidi ya tatizo la ukosefu wa ajira na mitaji kwa wajasiriamali wanaohitimu vyuo au mafunzo yoyote. Tunaombeni mtusaidie ili sauti yetu ya kinyonge isikike, tutajitokeza kwa wingi katika hili.