Byendangwero
JF-Expert Member
- Oct 24, 2010
- 871
- 56
Baada ya bodi ya Tanesco kumsimamisha mkugenzi wa shirika hilo la umma kwa tuhuma za ufizadi Zitto Kabwa alijitokeza hadharani kupinga hatua hiyo, na tangu wakati huo vyombo vingi vya habari vimekua vina,taja kuwa miongoni mwa wabunge waliopewa hongo na hao watendaji waandamizi wa Tanesco waliosimamishwa ili kuwatetea. Kwakua Zitto mwenyewe hajazikana habari hizo, nachukulia ni za kweli. Leo hii kambi ya upinzani, ambayo Zitto ni maibu kiongozi wake, imetoa msimamo wake kuhusiana na sakata hilo la Tanesco,; msimamo huo wa kambi la upinzani unakinzama kabisa na msimamo alionao Zitto juu ya suala hilo. Ni jambo la kawaida kwa watu waliyo kwenye kambi moja kuhitirafiana kimawazo; hata hivyo panapojitokeza hali hiyo, haina budi wahusika wote wajadiliane ili upatikane muafaka, baada ya hapo kila mtu ndani ya kambi hiyo anatakiwa kutoonyesha upinzani wowote juu ya muafaka huo hadharani. Kwa mtu yeyote ambaye amekuwa akifuatilia mwenedo wa Zitto atakubaliana na mimi kwamba mara nyingi Zitto upendelea kujitokeza hadharani na msimamo unaokinzama na wawenzake, Kisaikolojia janbo hilo siyo la ajabu , kwani inaeleweka kwamba miongoni mwa watu **** wale wanaoitwa "achievers", hao kwa kawaida siyo "team player" kwani kila nara wao wanachokipa umuimu siyo mafanikio ya timu yote bali mafanikio ya wao wenyewe binafsi. Hata hivyo katika suala hili la Zitto tatizo siyo tu la kuwa "achiever", inaonekana tatizo ni kubwa zaidi ya hapo; yeye anaonekana misimamo yake mingi inachukuliwa kwa lengo la kukidhi maslahi ya baadha ya makundi kwenye chama tawala, hata kwenye ili sakata la Tanesco ni dhahili Zitto amekuwa akijitahidi kusimamia maslahi ya akins Rostamali