CCM yazidi kubomka Ngara; jembe jingine lahamia CHADEMA

CCM yazidi kubomoka Ngara; jembe jingine lahamia CHADEMA
Katika hali inayoonesha kuendelea kufa taratibu kwa chama cha mapinduzi, Jumapili wiki iliyopita (10/6/2012) kulifanyika mikutano mikubwa miwili katika kata za Rulenge na Benako zote za wilayani Ngara, mkoa wa kagera. Mkutano wa Rulenge ulikuwa maalum kumpokea shujaa Philemon Charles maarufu kwa jina la Muha aliyekuwa mwenyekiti wa CCM kata ya Rulenge. Kwa wale wasiojua, hapo Rulenge ndiko nyumbani kwa mwenyekiti wa wilaya hiyo mwalimu Helena Adrian.

Akihutubia mamia ya wananchi, Muha aliwaambia wananchi kuwa amejitoa CCM kwa sababu ameona CCM imeishakufa bali baadhi ya viongozi wanadhani bado iko hai. Alisema anasubili kikao cha wananchi wote wa kijiji cha Rulenge ili awahoji viongozi wa kijiji hicho matumizi ya shilingi milioni 11 walizodai kutumia kukarabati chumba kimoja cha machinjio fedha ambayo ni nyingi kwa ukarabati wa chumba kimoja na kazi iliyofanyika haifahamiki.

Katika mkutano huo wa Rulenge, wana CCM waliorudisha kadi walikuwa 50 zaidi ya wanachama wapya waliojiunga na Chadema walikuwa 57.
CHADEMA Vema

Halleluya...!
 
Kauli ya Nape inakaribia kutimia kwamba atabaki peke yake M4C iongeze Kasi ccm imelegea
 
Back
Top Bottom