Elections 2010 CCM yatafakari mbinu za kuzima mdahalo wa Uraisi...

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,174
Shubiri ya kukwepa midahalo kwenye chaguzi za ubunge zimeishtua CCM - Chama Cha Mafisadi - baada ya kuona TBC1 imewajenga mno wagombea mbalimbali wa upinzani hususani Chadema..............

Wasiwasi umetanda ndani ya ngome ya mafisadi kuwa endapo TBC1 au NGO yo yote ile ikaitisha mdahalo wa wagombea Uraisi bila ya JK kushiriki huo utakuwa ni msumari mwingine kwenye jeneza la CCM ambalo kaburi lake tayari limechimbwa.

Ngazi za juu ndani ya serikali na CCM wapo kwenye mkakati mzito wa kuzuia mdahalo huo usifanyike ili kuokoa jahazi la CCM na hususani la JK ambalo tayari limekwisha kuzama na hakuna utetezi hapo.

Wanachohofia mafisadi hawa ni mdahalo huo kuibua kashfa za ufisadi zile nzito kama ya Richmond, Dowans, radar, Meremeta, Kigoda, Majengo mapacha ya BOT, Epa n.k ambayo JK bila ya shaka yoyote ile atapata wakati mgumu kutetea hatua ambazo serikali yake imechukua kuokoa mali ya umma na kuwaadhibu vibosile wa CCM ndani ya serikali ambao ndiyo chimbuko la wizi na ubadhirifu unaoendelea serikalini.
 
maskini atajibu nini JK akienda?
Huu mdahalo inabidi utafitiwe ratiba mapema ndani ya raundi hii ya mwisho
 
ITV waitishe huu mdahalo, I am telling you, Mengi atajenga reputation kubwa sana toka kwa watanzania kama akifanya hivi.
 
Kweli kabisa. Mafisadi walitaka kumuumiza ile mbaya, na nisikiavyo kuna vigogo wa juu kabisa katika sisiemu wanahusika katika sakata hilo la kutaka kubambikiwa madawa ya kulevya. Mzee mengi hakutaka tu kusema mengi siku ile, alitaka wenyewe mafisadi waseme.

Nasikia pia mikakati mikubwa iko kazini kujaribu kumbembeleza asahau hayo na apeane mikono (sic) na wabaya wake.
 
Wakati uliokubalika ni sasa. Watu wasiojihamini wanakwepa debate. Ukifuatilia hao walianzia shuleni kukwepa midahalo
 
Mdahalo kitu kidogo sana kwa JK, hakuna asiyefahamu kwamba uwezo wa JK ni mkubwa mno kupitiliza ukimlinganisha na wapinzani na hususani slaa ! namshauri slaa angerudi kwenye ubunge tu ! angalau ubunge SLAA anafanananao.
 
just imagine kikwete against Slaa what would jk say, ataishia kusema,kidumu chama cha mapinduzi, Slaa would eat him alive.
 
Tatizo kama unachuki binafsi inakuwa ngumu kuukubali ukweli ingawa roho yako inatambua kuwa JK anauwezo mkubwa sana wa kupanga hoja na kuzieleza kwa kina ! Hata hivyo kwanini unang'ang'ania mpambano wa Man United na Lipuli ya Iringa. Slaa mlinganishe na mutamwega angalau utaonekana unaakili timamu.
 
Hivi kuna chombo chochote cha Habari au mtu yeyote amefikia uamuzi wa kuandaa mdahalo huo (Urais) au ndio simulizi za JF?
 
Tatizo kama unachuki binafsi inakuwa ngumu kuukubali ukweli ingawa roho yako inatambua kuwa JK anauwezo mkubwa sana wa kupanga hoja na kuzieleza kwa kina ! Hata hivyo kwanini unang'ang'ania mpambano wa Man United na Lipuli ya Iringa. Slaa mlinganishe na mutamwega angalau utaonekana unaakili timamu.

Nani kakuambia jk atapanga hoja gani, ngoja nikuulize swali sasa kama anajiamini anaweza mbona awataki mdhahalo, si wangekubali tuone umahiri wake wa kucheka kizaramo!
 
Mdahalo kitu kidogo sana kwa JK, hakuna asiyefahamu kwamba uwezo wa JK ni mkubwa mno kupitiliza ukimlinganisha na wapinzani na hususani slaa ! namshauri slaa angerudi kwenye ubunge tu ! angalau ubunge SLAA anafanananao.

Tatizo kama unachuki binafsi inakuwa ngumu kuukubali ukweli ingawa roho yako inatambua kuwa JK anauwezo mkubwa sana wa kupanga hoja na kuzieleza kwa kina ! Hata hivyo kwanini unang'ang'ania mpambano wa Man United na Lipuli ya Iringa. Slaa mlinganishe na mutamwega angalau utaonekana unaakili timamu.

Huwa mwalimu wenu ni nani? Wanafunzi wake wote mnafanana katika kujenga hoja na matumizi ya lugha, mwambie awafundishe kwa ubunifu zaidi mmezidi ku copy-paste
 
POLICY FORUM wanaweza kushinikiza kuwepo na mdahalo.
Kama hizi media zetu watakuwa bias au waoga, basi iwezekane hata faculty mojawapo ya political science ktk universities zetu iandae hii kitu.

Mdahalo kitu kidogo sana kwa JK, hakuna asiyefahamu kwamba uwezo wa JK ni mkubwa mno kupitiliza ukimlinganisha na wapinzani na hususani slaa ! namshauri slaa angerudi kwenye ubunge tu ! angalau ubunge SLAA anafanananao.

Unadhalilisha taaluma za kupima uwezo wa watu au labda unaangalia nyota kama Sheik Yahaya. Dr. wa heshima (wakupewa kishkaji wa kuchakachua) awe na uwezo kuliko PHD holder aliyesotea kwa miaka its a joke. Lakini wapime kwa hoja kwa wananchi kati yao nani anaeleweka? Halafu jipime wewe hapa jamvini michango yako inahoja zipi? Au angalia mtaani kwako wanasemaje kuhusu hawa watu wawili? Mwisho usijeukakubukqa shuka shuka wakati kumekucha utaacha.
 
Kweli kabisa. Mafisadi walitaka kumuumiza ile mbaya, na nisikiavyo kuna vigogo wa juu kabisa katika sisiemu wanahusika katika sakata hilo la kutaka kubambikiwa madawa ya kulevya. Mzee mengi hakutaka tu kusema mengi siku ile, alitaka wenyewe mafisadi waseme.

Nasikia pia mikakati mikubwa iko kazini kujaribu kumbembeleza asahau hayo na apeane mikono (sic) na wabaya wake.

Kuna tetesi kuwa Mengi alitaka kuwa mgombea binafsi nadiyo maana CCM hawampendi. Kuhusu madawa ni kweli maana ukiwasema mafisadi ni sawa na kuisema CCM. Mafisadi=CCM=Mafisadi. No difference
 
Tatizo kama unachuki binafsi inakuwa ngumu kuukubali ukweli ingawa roho yako inatambua kuwa JK anauwezo mkubwa sana wa kupanga hoja na kuzieleza kwa kina ! Hata hivyo kwanini unang'ang'ania mpambano wa Man United na Lipuli ya Iringa. Slaa mlinganishe na mutamwega angalau utaonekana unaakili timamu.

hakuna haja ya kuandikia mate wakati wino upo. Mshauri JK aje kwenye mdaharo siku ukitangazwa. Uone aibu atakayoivuna. hatasahau katika maisha yake. Labda kama anataka kudondoka tena!!!
 
POLICY FORUM wanaweza kushinikiza kuwepo na mdahalo.
Kama hizi media zetu watakuwa bias au waoga, basi iwezekane hata faculty mojawapo ya political science ktk universities zetu iandae hii kitu.

Itabidi tuwaandikie na kuwaomba. Nitaleta jibu wakinijibu.
 
Back
Top Bottom