CCM yasimamisha uchapishaji wa gazeti la Uhuru kwa siku 7 na kuwasimamisha Watendaji Wakuu watatu

Khadija Mtalame

Senior Member
Jul 14, 2021
186
715
DANIEL CHONGOLO AMBAE NI KATIBU MKUU CCM TAIFA AMELIFUNGIA SIKU SABA GAZETI LA UHURU KWA KUCHAPISHA HABARI ISEMAYO KUWA RAIS SAMIA HASSANI SULUHU HANA MPANGO WA KUGOMBEA 2025.

GAZETI LA UHURU LIMEFUNGUWA SIKU SABA

Uhuru wa vyombo vya habari saizi uko huru.

Pia soma

----
Chama cha Mapinduzi kimesimamisha uchapishaji wa gazeti la Uhuru kwa muda wa siku saba huku kikiwasimamisha kazi watendaji wakuu watatu wa gazeti hilo kwa madai ya upotoshaji wa kauli ya Rais Samia Suluhu Hassan.

Mapema leo chama hicho kilitoa taarifa kikieleza kusikitishwa na kitendo kilichofanywa na gazeti hilo cha kupotosha kauli ya Rais Samia Suluhu Hassan iliyotokana na mahojiano ya kiongozi huyo na Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC), ambapo chama kiliahidi kuchukua hatua za kinidhamu dhidi ya wote waliohusika katika uandaaji wa habari hiyo.

Gazeti hilo la CCM, toleo la leo Agosti 11, limeandika habari yenye kichwa kisemacho “Sina wazo kuwania urais 2025-Samia”, ambayo imepewa uzito mkubwa.

Akizungumza na waandishi wa habari baadaye leo Jumatano Agosti 11, 2021, Katibu Mkuu wa chama hicho, Daniel Chingolo amesema uamuzi wa kuwasimamisha kazi viongozi hao umetolewa na bodi ambayo imeenda mbali na kuunda kamati ya kuchunguza sababu za jambo hilo kutokea.

“Ukifuatilia mahojiano aliyofanya Rais Samia Suluhu Hassan hakuna mahali alipozungumza maneno yaliyoandikwa kwenye kichwa cha habari cha gazeti la Uhuru la leo, amelishwa maneno na uungwana ni vitendo tunamuomba radhi Rais.

Viongozi waliosimamishwa kazi ni Mkurugenzi Mtendaji wa gazeti hilo, Ernest Sunguya ambaye pia ni mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Mhariri Mtendaji, Athumani Mbutuka na msimamizi wa gazeti hilo, Rashid Zahoro.

“Tumeamua mambo kadhaa, bodi ilikutana na kuleta taarifa ya hitimisho la kikao chao, ninaipongeza kwa uamuzi walioufanya na mimi kama Katibu Mkuu nimesimamisha kuanzia leo uchapishaji wa gazeti la Uhuru kwa siku saba, hayo ni mamlaka yangu,” amesema Chongolo.

Chanzo: Mwananchi
 
DANIEL CHONGOLO AMBAE NI KATIBU MKUU CCM TAIFA AMELIFUNGIA SIKU SABA GAZETI LA UHURU KWA KUCHAPISHA HABARI ISEMAYO KUWA RAIS SAMIA HASSANI SULUHU HANA MPANGO WA KUGOMBEA 2025.

GAZETI LA UHURU LIMEFUNGUWA SIKU SABA

😅😅😅😅😅😅😅
Uhuru wa vyombo vya habari saizi uko huru.
Mbuzi wa bwana heri amekula mahindi kwenye shamba la bwana heri
 
Movie za kihindi!

Kwanza mjiulize hayo mamlaka kayapata wapi?

Labda aseme wameamua kusitisha uchapishaji kwa muda wao kama wamiliki na sio kulifungia unless atuambie amelifungia kwa kutumia sheria na kwa mamlaka gani aliyonayo.
 
Kwa sheria ipi inayompa nguvu ya kufungia chombo chochote cha habari kama katibu wa chama cha kisiasa???? Mtoa uzi weka chanzo kabla katibu wangu wa kikundi hajakufungia pia kwa upotoshaji huo
 
DANIEL CHONGOLO AMBAE NI KATIBU MKUU CCM TAIFA AMELIFUNGIA SIKU SABA GAZETI LA UHURU KWA KUCHAPISHA HABARI ISEMAYO KUWA RAIS SAMIA HASSANI SULUHU HANA MPANGO WA KUGOMBEA 2025.

GAZETI LA UHURU LIMEFUNGUWA SIKU SABA

😅😅😅😅😅😅😅
Uhuru wa vyombo vya habari saizi uko huru.
Katibu mkuu CCM alifungia Uhuru?
 
Haya maigizo hayana mvuto
ndiyo yale yale ya picha la kidindi, kwa sterling kufa kwny matutabya viazi..

gazeti la chama, muhusika anaadhibiwa na chama kimya kimya, au ni mzunguko? au kuna gazeti linatafutwa kufungiwa ili wana nzengo wakija kulalamika waambiwe hata uhuru lilifungiwa.
 
Huko ndani kumechafuka mpaka kunanuka
 
DANIEL CHONGOLO AMBAE NI KATIBU MKUU CCM TAIFA AMELIFUNGIA SIKU SABA GAZETI LA UHURU KWA KUCHAPISHA HABARI ISEMAYO KUWA RAIS SAMIA HASSANI SULUHU HANA MPANGO WA KUGOMBEA 2025.

GAZETI LA UHURU LIMEFUNGUWA SIKU SABA

😅😅😅😅😅😅😅
Uhuru wa vyombo vya habari saizi uko huru.
Source please
 
Huko ni kulifungia au kulizuia lisitoke. Sababu mmiliki akiamua kutokulitoa gazeti lake hata kwa mwaka sidhani kama ni kulifungia.

Ni kama mtu akiamua kujiweka lockdown nyumbani kwake, sidhani kama hapo atakuwa amefungiwa bali ameamua kujifungia mwenyewe ?
 
Katibu Mwenezi wa hovyo sijawah ona , tangu apeleke majina utopolo kwenye teuzi za U-DC ndo nikaona Choo cha kike hiki
 
Back
Top Bottom