CCM yampitisha mgombea wake wa Naibu Meya - Arusha

Mwan mpambanaji

JF-Expert Member
Apr 3, 2008
482
131
Kikao cha madiwani wa ccm kilichokaa jana kimempitisha Mh lota laizer Diwani wa Kata ya Baraa kuwa mgombea wa kiti cha naibu meya,awali walikuwa madiwani wa Moshono mh Paul matsen na mh Ole sekeyani wa Terat waliojaza fomu za kugombea nafasi hiyo,chama Ngazi ya Wilaya kikarudisha majina yote matatu ndipo jina la Lota likapita kwa kupata kura Mh Lota Laizer kura 5,Mh Ole sekeyani 3,na Mh Paul 2.
Mh Lota Laizer aliwahi kuwa Meya wa Arusha kabla ya kulazimishwa kujiuzulu na chama chake kwa kashfa ya kuuza maeneo ya wazi hasa kiwanja kilichoko oposite na Soko la Kilombero.Diwani huyu wa bara ambaye ni fisadi ndio leo anachaguliwa kuwa naibu meya,huyu Mh Lota laizer ameuza viwanja vingi vya wazi Arusha,eneo la Ngiwaranecha,shule ya sekondari Baraa na mengine mengi.
 
Jibu ni rahisi...

Pale CCM bado kuna watu wazuri .... Wahame chama haraka ... Waanzisha CCM yenye misingi na itikadi za Kweli Za TANU na ASP ... Wafanye Update kidogo... Iwe ile CCM AZIMIO LA ARUSHA CCM AA the Conservative CCM... SALM AHAMED SALM anaweza kutoa ushauri kwa hili kundi.

CCM ya Pili hii ya kina Kikwete, Lowasa na wenzake ... CCM AZIMIO LA ZANZIBAR CCM AZ The Liberal CCM.

Hawa Conservative CCM hawa ndio wanaweza kuokoa nchi kwa kuwatimua hawa liberal wasinii wakubwa wanohatarisha Taifa. Hawa CCM AA ndio wanaweza kuchuana ki ukweli na CHADEMA na kuleta upinzani wa kweli wenye tija na maendeleo.

..Ninaamuru hili litokeee!!
 
Hii ni Kali je tutafika? Haohao ndio wanaogawana viwanja Kule kwa Mromboo na Kule Burka mikahawani
 
Kwakuwa wanachaguana wenyewe waacheni wafanye wanavyotaka
 
Back
Top Bottom