CCM wazidi kujiumbua kwa kupinga muundo wa muungano sasa muundo wa bunge wawaumbua

Bekabundime

JF-Expert Member
Aug 6, 2014
2,016
1,732
Wanajamvi,

Ni wazi kabisa wenzetu wa Lumumba sasa wanaumbuka kwani walichokikataa kwenye rasimu ya Warioba bado kinawasumbua kwenye muundo wa bunge,wengine wakisema pawepo na mabunge matatu la Zanzibar,la Tanganyika,na Bunge la seneti litakalo shughulika na masuala ya muungano na wengine wakitaka iwe kama ilivyo sasa.

Sasa nauliza je huwo si muundo wa serikali tatu?

Nawasilisha.
 
Acha wajionee wenyewe,wanadhani watakuwa madarakani for ever. Waulize wastaafu wa leo.
 
...hii mijamaa ni hatari sana kwa maslahi ya taifa,inajali matumbo yao tu...
 
Katiba mpya walishatoka nayo nje Ukawa, kichoachwa dodoma ni uchakachuaji na posho za wachakachuaji!
 
Wanajamvi,

Ni wazi kabisa wenzetu wa Lumumba sasa wanaumbuka kwani walichokikataa kwenye rasimu ya Warioba bado kinawasumbua kwenye muundo wa bunge,wengine wakisema pawepo na mabunge matatu la Zanzibar,la Tanganyika,na Bunge la seneti litakalo shughulika na masuala ya muungano na wengine wakitaka iwe kama ilivyo sasa.

Sasa nauliza je huwo si muundo wa serikali tatu?

Nawasilisha.

aisee kumbe Hakuna tofauti ya Bunge na Serikali eeeh?
 
Hili mbona nimelileta hapa kabla ccm wa Zanzibar walioko bungeni wanajaribu kudai mambo yafananayo kama yale ya ukawa lakin sasa tatizo linakuja kwenye mfumo wa s2 ni ngumu lazima tu kubadilike muundo na wao walilazimishwa mambo fulani fulani kutoka kwa makada wa Zanzibar.
 
Hivi huu u-dikteta wa nini? Si Wananchi eventually wataamua why bother? Acha BMK waandike watakavyo, kutakuwa na compaign eventually za kusema katiba ni nzuri au mbaya na Baada ya hapo Wananchi tutapiga picha hizi Kelele za u-dikteta za nini?
 
Kweli wabongo wepesi kusahau mara hii umeshasahau uchakachuaji wa kula za hapana ndio zina kuwa ndio ha ha ha haaa.
 
jana walituambia kamati no 8 ilipendekeza kuwapo kwa mabunge matatu la zanzibar la muungano na la tanganyika.
sababu walizozitoa ni kuwa wabunge wa zanzibar hawana mamlaka ya kujadili mambo ya tanganyika hivyo ni bora kuwe na bunge la seneti litakalokuwa na wabunge 20 wa muungano watakaojadili wizara kama tano za muungano.
wanapojichanganya.
kama wabunge wa zanzibar hawana mamlaka ya kujadili mambo kwenye bunge la muungano kwa mambo ya tanganyika watapata wapi mamlaka ya kushighulikia mambo ya tanganyika wakiwa kwenye serikali ya muungano?je watawatenganisha vipi katika serikali hiyohiyo?je walisoma vitabu vya kitafiti vya tume ya warioba kuhusu hilo?
je bunge la tanganyika litawajibika kuisimamia serikali ipi maana ya muungano tayari itakuwa inasimamiwa na bunge la muungano?
nawatakia bmk kazi njema ila wasisahau kuweka kile kipengele cha BINADAMU WOTE NI NDUGU ZANGU NA AFRIKA NI MOJA katika katiba yao.
 
"Wanachokifanya CCM kwenye bunge la Katiba ni Utoto" By WARIOBA.

Rasimu ya katiba haiwezi kujadiliwa kwa vifungu viwili ambavyo walisema kuwa ni msingi yaani muundo wa muungano, rasimu hii itawaumbua sana kadiri muda unavyooenda, sasa mabunge matatu maana yake nini nyie mbumbumbu?, nyie kaani siku hizo 84 mpate posho zenu kwani hilo ndilo lililowapeleka bungeni yaani njaa sio katiba.
 
Kweli ujenzi wa mnara wa babeli (katiba) tayari unawaumbua ccm. Bunge la tatu kusimamia serikali ipi? Hivi watatumia njia gani kumwomba radhi warioba na tume yake kwa matusi yote waliyomtukana? Au kikwete atakuja tena anachekacheka kama hayawani aanzishe uongo mpya?
 
Hivi huu u-dikteta wa nini? Si Wananchi eventually wataamua why bother? Acha BMK waandike watakavyo, kutakuwa na compaign eventually za kusema katiba ni nzuri au mbaya na Baada ya hapo Wananchi tutapiga picha hizi Kelele za u-dikteta za nini?

Na wasipo pata kile wanachokitaka wanchi unajua matokeo yake?
kama hujuhi kaulize kenya. na hicho ndio wancho ogopa UKAWA.
Heri ya nusu shari , kuliko shari kamili. Heri ya lawama kuliko fedhea.
 
hapo wakishapitisha mabunge matatu na serikali mbili bunge la tanganyika litaisimamia na kuitungi sheria nchi ya kusadikika.
 
Back
Top Bottom