CCM waumbuka Uwanja wa Taifa, Makamba akumbana na nguvu ya UKAWA

Na mimi ngoja niende kulipia watu wote quality plaza wafanye chochote wanachokitaka kwa siku ya leo.
 
Leo kwenye uwanja wa taifa katika mechi ya Stars na Nigeria bwana Januari Makamba akajitia pedezjee kulipia watu wote walokuwa nje waingie ndani bure, ilipofika half time mtangazaji wa PA ya uwanja akaanza kumnadi Januari kwa mbwembwe zote, cha ajabu uwanja mzima ulilipuka na kuanza kuzungusha mikono kuashiria mabadiliko bendera na picha za Lowassa hata sijui ziliibukia wapi ilikuwa patashika. Kweli Lowassa kiboko yenu.

VIDEO


Na kama alikua anataka kutest CCM inakubalika vipi amepata majibu yake Jana, uwanja mzima ulilipuka lowasa, lowasa,lowasa, peopleeees....Watanyooka tu
 
Last edited by a moderator:
Mwachen mpumbavu ktk upumbavu wake,
WATANZANIA TUMEITWA WAPUMBAVU na ndo sisi MALOFA tunaotaka mabadiliko ya nchi hii!.
VIVA UKAWA
 
hivi hizo hela Makamba alizotumia kuwalipia watu kutizama mpira si angejitolea kununua madawati ya watoto wa shule? kiongozi kutoa hela kwa dizaini hiyo kipindi cha uchaguzi ni sawa na kuhonga wapiga kura.


Mkuu Triplets, hii ni rushwa dhahiri. Tungekuwa na TAKUKURU ya kuzuia na kupambana na rushwa muda huu Makamba (ya makatani sijui?) yangekuwa yanasaidia polisi kuhusu tukio hili. Lakini hii TAKUKURU (kama alivyoimba jamaa mmoja a Bongo flava) ni ya kukukuza na kuboresha rushwa.

Tungetegemea NEC iwe imesema neno, lakini nayo kimya! Hii ikidhihirisha kuwa sio tume huru ya uchaguzi. Kama unabisha kuwa si huru, kwanini hawakukanusha kwenye madai ya Katiba ya kudai Tume Huru? Hivi kunaweza kuwepo madai ya kitu ambacho tayari kipo?
 
Kuna ukweli wa Habari zako lakini sio kweli kwamba ni Uwanja mzima maana na wengine pia tulikuwepo na hatukuhusika katika hilo.Na kweli kwamba Makamba hapa alichemsha maana wengine walikshaingia kwa kukata tiketi kwa mantiki hio hapo kuliibua pia hasira za wale waliokuwa wameshalipa
 
Hila na fitina hazita wasaidia
Kwanini leo ndio waingie bure?na siku zote watu wanalipa mpaka matamasha ya dini!!!!

Mkuu kati ya wajanja ktk nchi hii wewe ni wakwanza umeshajua mitego ya adui iweje leo wakati siku zote wanaingia kwa pesa zao
 
Uwanja wa Taifa una uwezo wa kubeba watu 60000 Dar ina watu wangapi?

Waliofanya hivyo ni wangapi?Ambao hawakufanya hivyo ni wangapi?
Ukiitwa lofa utachukia?

Hata bilioni uanza na moja!! hujui hilo? wawapi wewe?
 
Pale Jangwani hukuwaona eeeh!!!subiri Oct 25 jioni tumtawaze EL ndo utaelewa wewe na genge lako la wahujumu uchumi
Uwanja wa Taifa una uwezo wa kubeba watu 60000 Dar ina watu wangapi?

Waliofanya hivyo ni wangapi?Ambao hawakufanya hivyo ni wangapi?
Ukiitwa lofa utachukia?
 
Kama kuna mtu aliwa hajui mabadiliko huwa yanatokeaje ndo hivi. Hakuna namna nyingine ya kueleza kuwa wakati wa mabadiliko ni sasa.Mkikaa sehemu watu 8 utakuta sita ni wanamabadiliko! CCM itaponaje?
 
Kama Tanzania ni yako na familia yako tutafanya ivyo. Unaisemea nchi hii kama Mali yako... Timamu kweli wewe!!!!????

Mkuu yote hii ni sababu ya kulewa madaraka wakidhani Tz ni yao na wao ndo wenye uhalali wa kutuchagulia kiongozi lakni mwaka huu cha moto watakiona
 
#HapaKaziTu.

Nyinyi pigeni porojo, bado mna miaka mingi sana ya kuiota ikulu.

Hatuwezi wapa ikulu Ku Klux Klan Tanzania - kumbuka hilo.

Hapa kazi wee unakazi? kauli mbiu za ccm sio za watanzania. Maisha bora yalikuwa kwao wao na familia zao, wanaposema hapa kazi wanamaanisha kwao wao na watoto. Hebu nenda katafute shuhuli ya kufanya, Napita kuja kula pialu ya kuku, niwekee sahani 1 na juice ya ukwaju bibie
 
Back
Top Bottom