CCM watwangana ngumi mkutanoni Kyela

- Haya mambo ya ajabu sana, hivi huko kwenye ubunge kuna nini hasa mpaka watu wanataka kuuaana?

- Mshahara mbona ni mdogo kuliko hela na ngumi wanazozitumia kuupata, kuna nini hasa huko bungeni?

FMES!
 
Sijaelewa au mimi ndio sijui maana ya ukabila. Waliotwangana ni watu wa wilaya ya kyela na wote ni wa kabila moja. Kama wote ni wa kabila moja, kinachowagombanisha ni ukabila au kitu kingine?
Inakera sana mtu anapoingiza suala la ukabila ata sehemu isiyohusika.
 
huyu doktaa mahanga ana hofu ya uwezo wake mdogo kuwaletea maendeleo watu???

kiongozi makini huwezi kulialia eti wapo wanaonichafuaaaa.....basi wanaloooo

UKONGA MAHANGA HAWAFAIIII
 
Hivyo ni vituko vya Mwakipesile baado ana ndoto za kuwa mbunge. anakosa shukrani kwa Mungu aliyompa u RC baada yakukosa ubunge. Hela ni ya Rostam anayotumia
 
. ...Sasa kinachowagombanisha ni ukabila au ni kitu kingine?.....

Hawa jamaa wana masuala kadhaa ambayo yanwagombanisha, kuna mada nyingi sana hapa ambao tumejadili siasa za Mbeya, we zitafute tu! Ila kwa kuanzia:-

1. Mwakyembe na Mwakipesile waligombea jimbo la Kyela mwaka 2005 na katika kura za maoni Mwakyembe alimshinda Mwakipesile ambaye kwa sasa ni Mkuu wa mkoa wa Mbeya. Wakati wa kampeni za kugombea kuteuliwa kulikuwa na kutokuelewana kwa watu hawa wawili kutokana na kukashfiana wakati wa kampeni.

2. Mwakipesile ni mfuasi wa wanamtandao (JK Group) ilhali Mwakyembe si mfuasi wa mtandao. Kimsingi makundi haya mawili yana ideology (itikadi) tofauti sana, ndio sababu hata katika vita vya ufisadi huwezi kumsikia Mwakipesile akipiga kelele kukemea, kwa sababu anafaidika nao!

3. Mwakipesile ni mkuu wa mkoa PEKEE Tanzania ambaye anaongoza mkoa wenye jimbo la watu WALIOMKATAA kuwaongoza. Kawekwa kwa sababu maalum na wanamtandao wenzake!
Kama nilivyodokeza hapo juu
 
Waacheni wafu wawazike wafu wao!! Lingekuwa jambo la uvumba iwapo mngetuwekea na picha!!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom