CCM watwangana ngumi mkutanoni Kyela

Mwiba

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
7,607
1,744
Na Mwandishi wetu.

MTAFARUKU mkubwa umezuka ndani ya kikao cha Kamati ya Maadili ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilayani Kyela uliosababisha Polisi kuingilia kati na kumwokoa Katibu wa chama hicho wilaya, Bi. Maria Mwambanga.

Polisi walichukua hatua hiyo baada ya, Bi. Mwambanga kupokea kipigo kutoka kwa wanachama hao waliomtuhumu kuwa ni kibaraka wa baadhi ya wanasiasa huku wajumbe wengine wakitwangana makonde wao kwa wao.

Kikao hicho cha Kamati ya Maadili, kiliwaita makatibu kata wa chama hicho wa Kata za Kyela mjini, Kajunjumele, Makwale, Lusungo, Katumba Songwe, Itope na Diwani wa Kyela Mjini, Bw. Visk Mahenge wakidaiwa kuwa walimkashifu Mbunge wa Kyela, Dkt. Harrison Mwakyembe kwenye kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya

Kamati hiyo ikiongozwa na Mwenyekiti, Bw. Japhet Mwakasumi na Katibu wake Bi. Mwambanga, waliwaeleza makatibu hao na diwani kuhusu kumkashifu, Dkt. Mwakyembe na kuwataka waeleze sababu za kufanya hivyo na kwanini wasichukuliwe hatua za kinidhamu.

Kwa mujibu wa mmoja wa watuhumiwa hao, ugomvi uliibuka baada ya wao kuhoji hatua ya kuitwa peke yao bila pande zote zinazohusika kwenye mvutano huo.

Baada ya suala hilo kuzua mtafaruku mkubwa, Polisi walifika eneo hilo la ofisi ya CCM wilaya kumwokoa Katibu huyo aliyekuwa akipokea kipigo, huku wajumbe wa kikao hicho wakisambaratika kila mtu na njia yake kwa hofu ya kukamatwa na Polisi.

Mwenyekiti wa CCM Wilaya, Bw. Japhet Mwakasumi alipotakiwa kuzungumzia sakata hilo alisema kwa muda huo akili yake ilikuwa haijatulia hadi hapo baadae.

Naye Mwandishi Grace Michael anaripoti kuwa katika kile kinachoonesha kuwa hali si shwari katika majimbo mengi ndani ya CCM kuelekea Uchaguzi Mkuu mwakani, Mbunge wa Ukonga Dkt. Makongoro Mahanga ameonya dhidi ya tabia ya wana CCM kuchafuana.

Dkt. Mahanga amewataka badhi ya wanachama wenye nia ya kugombea udiwani na ubunge kuacha mara moja tabia ya kupitapita kwa wananchi na kuchafua majina ya viongozi waliopo madarakani kwa lengo la kujipatia umaarufu kisiasa.

Alidai mbali ya kuchafua majina ya vingozi pia wanakwamisha utekelezaji wa Ilani ya CCM kwa kuwachanganya wananchi na kupoteza mwelekeo wao wa kushirikiana na viongozi katika shughuli mbalimbalia za maendeleo.

Akifungua semina ya Jumuiya ya Wazazi katika Kata ya Ukonga, Dar es Salaam juzi, Dkt. Mahanga alisema ni vyema wanachama wa CCM, wakatumia muda huu kuweka mikakati ya namna chama hicho kitakavyoibuka na ushindi wa kishindo katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

"Wapo baadhi ya wana CCM ambao tayari wameanza kuwapitisha wagombea wao kwa wananchi ili kufanya kampeni za ubunge mwakani, hatukatai watu kujitokeza kugombea kwani ni haki yao kidemokrasia lakini ni lazima kanuni na taratibu za uchaguzi za CCM zifuatwe kwa maana ya muda wa kuanza kampeni hizo," alisisitiza Dkt. Mahanga.

Alisema kuwa tatizo kubwa linalofanywa na wagombea hao ni kupita kwa wananchi huku wakitoa kashfa kwa viongozi ambao bado wako madarakani nakuwataka kuacha mara moja tabia hiyo na kujikita katika kumaliza kero za wananchi zilizobaki katika kipindi hiki.

Dkt. Mahanga alisema kuwa, vitendo vya kuchafuana kwa sasa vitasababisha kukwama kwa utekelezwaji wa Ilani ya CCM, ambapo kiongozi aliyepo madarakani anatakiwa kushirikiana na wananchi wake katika utekelezaji huo.

"Kuanza kuvutana kwa sasa ni kupoteza dira kwani uchaguzi ni mwakani hivyo ni bora tukajikita kwanza kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na sio kuweka nguvu katika uchaguzi ambao muda wake bado, lakini wanaotumia jina la Mbunge kusaka udiwani hilo nalo pia ni tatizo linaloweza kunigombanisha na wanachama wangu, haya mambo tuyaache kwanza," alionya Dkt. Mahanga.

Naye Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji, Bw. Ahmad Mkude, alisema kuwa vitendo vya watu kupita kwa wananchi huku wakiharibu majina ya viongozi, si sahihi hivyo aliwataka wanajumuiya hiyo kuwa makini na watu hao.

"Hawa watatugombanisha na viongozi wetu, tunatakiwa kuwa makini zaidi na sio kusikiliza maneno ya watu bila kuangalia wamefanya nini ndani ya jamii yetu, wanatakiwa kuja kwa hoja lakini si kwa kashfa kwa kiongozi aliyepo na tukiendekeza itatugawa na madhara makubwa yatatokea ndani ya chama chetu," alisema Bw. Mkude.
 
ukabila mbeya umezidi!!! ACHA TU WAENDELEE KUTWANGANA! INGEKUWA KAMA WANATWANAGANA KWA SPIDI HII KUTETEA MAENDELEO YA TAIFA, BASI HAKIKA LEO HII TUNGEKUWA MBALI ! Mzee six mwenyewe anakwambia, speed na viwango, LOL! So, wazazi endeleeni tu kutwangana !
 
Sasa hapa jumba bovu linamwangukia Mwakyembe au wabaya wake??? mbona kama hao wote wamemkashifu mwakyembe then hata yeye si shwari sana huko kwao?

Mh siasa za bongo kwa kweli zinataka moyo... sometime ni bora kutafuta nama ya kuifanya siasa kuwa haina high profile kwa maendeleo yetu

HAO WALIOITWA MKUTANO, HAWAKATHIRI UZALISHAJI KWA SIKU HIYO KATIKA NYANJA WALIZOMO??

NA SIKU HIZI HATA VIJANA VERY INTELIGENT NA PRODUCTIVE NAO WAMEJIINGIZA HUMO KWENYE MICHEZO YA MAIGIZO

SHIT!!!!

INAUMA SANA MJOMBA KUTUMIA KURA ZETU KAMA MAZALIO YAO
 
ukabila mbeya umezidi!!! ACHA TU WANENDELEE KUTWANGANA! INGEKUWA KAMA WANATWANAGANA KWA SPIDI HII KUTETEA MAENDELEO YA TAIFA, BASI HAKIKA LEO HII TUNGEKUWA MBALI ! Mzee six mwenyewe anakwambia, speed na viwango, LOL! So, wazazi endeleeni tu kutwangana !

Kule speed ya maendeleo ni kubwa sana. Ndiyo maana wanatwangana. Ukilala lala huwezi kumbuka kumtwanga mwezako anayeongea mbofu mbofu
 
Kutwangana kwa wenyewe kwa wenyewe ni dalili ya CCM kuporomoka kama chama chenye maadili. Kama ufisadi ukishaingia, unategemea uadilifu na uvumilivu kuwapo?

Kuna tofauti gani na chama cha Mrema? Wanatwangana kule kwa kugombea ruzuku -- ni ufisadi tu. Juzi Tambwe Hiza alivikandia vyama vya upinzani kwa mambo kama haya -- hivi sasa atasema nini kuhusu chama chake alichokipiga teke na kukirudia?
 
ukabila mbeya umezidi!!! ACHA TU WAENDELEE KUTWANGANA! INGEKUWA KAMA WANATWANAGANA KWA SPIDI HII KUTETEA MAENDELEO YA TAIFA, BASI HAKIKA LEO HII TUNGEKUWA MBALI ! Mzee six mwenyewe anakwambia, speed na viwango, LOL! So, wazazi endeleeni tu kutwangana !

Sijaelewa au mimi ndio sijui maana ya ukabila. Waliotwangana ni watu wa wilaya ya kyela na wote ni wa kabila moja. Kama wote ni wa kabila moja, kinachowagombanisha ni ukabila au kitu kingine?
 
Na watangwana sana mwaka huu (serikali za mitaa) na mwakani (uchaguzi mkuu)

Na wanatwangana kikweli ila habari zinakuwa wanazifichaficha lakini kuna mapigano na sio mapigano bali kuna makonde sasa fikiria mwenyewe ,halafu jamaa wanaambizana kama tuone kama kiti cha ubunge utakikalia ,kwa maana atamnunulia viungo vya binadamu kwa bei yeyote.
 
sijaelewa katika haya makundi waliokuwa pro Mwakyembe ni akina nani? na hao waliohongwa pesa za kampeni ni kina nani? isije ikawa kuna mkono wa rostam aziz hapa, hawa wahindi watatuvuruga sana mwaka huu.

HII NI NCHI YETU, TUSIKUBALI KAMWE KUKATANA MAPANGA KWA VISENTI VYA MAFISADI
 
sijaelewa katika haya makundi waliokuwa pro Mwakyembe ni akina nani? na hao waliohongwa pesa za kampeni ni kina nani? isije ikawa kuna mkono wa rostam aziz hapa, hawa wahindi watatuvuruga sana mwaka huu.

HII NI NCHI YETU, TUSIKUBALI KAMWE KUKATANA MAPANGA KWA VISENTI VYA MAFISADI

Jamani Rostam Azizi si mhindi ,wahindi na wairani picha haziendi kabisa ni watu mbalimbali na mambo yao hayalingani wala hawashirikiani ,matajiri wengi wa kihindi ni mahindus na huyu ni mpiga kifua shia wa kiirani.
 
Siasa za kyera zaidi uuavyo.....waachieni wenyewe wa kyera wameshaizoea....
 
Sijaelewa au mimi ndio sijui maana ya ukabila. Waliotwangana ni watu wa wilaya ya kyela na wote ni wa kabila moja. Kama wote ni wa kabila moja, kinachowagombanisha ni ukabila au kitu kingine?

kama huwajui watu wa mbeya mzee, haya. uliza uambiwe !
turudi kuleeeeee-- mwakyembe vs mwakipesile!
 
kama huwajui watu wa mbeya mzee, haya. uliza uambiwe !
turudi kuleeeeee-- mwakyembe vs mwakipesile!
Mwakyembe Vs Mwakipesile wote wanyakyusa. Sasa kinachowagombanisha ni ukabila au ni kitu kingine? Ingekuwa mwakyembe angekuwa msafwa halafu Mwakipesile mnyakyusa hapo mi ningekuelewa.
 
Huu mgogoro ulianza kama wiki mbili zilizopita. Kulikuwa na kikao cha CCM wilaya na mbunge akiwa mjumbe. Mbunge alipopewa nafasi ya kuongea aliwashambulia wajumbe na kudai wanamwomba mwomba pesa kisa wanamsaliti, wamehongwa lakini yeye hawamuwezi na hawezi kushindana na wajinga ambao hawajui kitu na kwamba yeye anashindana na Rostam. Baada ya hayo maneno hao watu wa CCM walichukia na kuanza kuguna na kuzomea.

Baadaye Mwenyekiti wa CCM kwa kushirikiana na katibu wake wakaitisha kikao cha maadili na kuwatuhumu hao wajumbe waliotajwa kwenye hiyo makala kwamba wamemkashifu mbunge. Waliposomewa mashitaka yao ndio wakaanza kuhoji mbona mbunge ambaye naye aliwatukana hajaitwa? Baada ya hapo wakaanza kutembeza mikono wakidai wamechoka kutukanwa kwamba wamehongwa wakati hakuna ukweli wowote. Pia walikuwa wanamtuhumu mwenyekiti wao kuhongwa pikipiki na Mengi kupitia kwa mbunge. Mimi nimeiona hiyo pikipiki mpya (hizo za India) lakini sijui kahongwa au kanunua kwa pesa zake.

Hapa Kyela mambo hayako sawa kabisa na tutashuhudia mengi mno kabla ya hiyo 2010. Kuna mengi tu hatuandiki maana watu watasema tunamwandama Mbunge na tumetumwa na Rostam.

CCM imemhamisha huyo katibu mara moja na kumpeleka Mbeya vijijini. Pia wameamua kesi isipelekwe mahakamani, kwa kifupi hakuna kesi tena. Sijui hiyo nguvu ya kuwaamuru polisi wasipeleke kesi mahakamani wameitoa wapi?
 
Kazi kweli kweli! afadhali tuanzishe boxing team labda wengine watafaidika kuliko kutwangana mangumi shauri ya wanasiasa uchwara.

Ujinga na njaa vikukutana huwa balaa kabisa!

CCM watwangana makonde
• Katibu wa Wilaya aokolewa na polisi


na Richard Kilumbo, Kyela




VURUGU kubwa zimeibuka ndani ya Kikao cha Kamati ya Maadili ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilayani Kyela, kulikosababisha viongozi kadhaa wa kamati hiyo kupigwa huku Katibu wa CCM Wilaya, Maria Mwambanga, akilazimika kuokolewa na askari polisi.

Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Maadili ya chama hicho waliozungumza kwa sharti la kutoandikwa majina yao gazetini, walisema kikao hicho kiliwaita baadhi ya makatibu kata, akiwamo Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Wilaya, Visk Mahenge, ambao walikuwa wakituhumiwa kwa makosa tofauti.

Walisema baada ya wajumbe hao kuwasili na mwenyekiti kufungua kikao majira ya saa 7.30 mchana na kuanza kuitwa kwa mjumbe mmoja mmoja, ili kusomewa makosa yake, makatibu wanne kati ya walioitwa walivamia ndani ya ofisi na kuufunga mlango mkuu na kuanza kuwashambulia wajumbe wa kamati hiyo kwa kuwapiga ngumi na mateke.

Wajumbe hao walisema makatibu kata hao walikuwa wakiwashambulia viongozi wao huku wakiwatuhumu viongozi wakuu waandamizi kwamba wanaendesha vikao kwa kushinikizwa na baadhi ya wanasiasa wasioitakia mema CCM.

Mwenyekiti wa CCM Wilaya, Japhet Mwakasumi, akizungumzia sakata hilo alisema, waliamua kuitisha kikao hicho si kwa shinikizo la mtu bali alifanya hivyo kwa lengo la kuleta amani ndani ya chama hicho kutokana na vurugu zilizoletwa na baadhi ya wajumbe katika kikao cha halmashauri kuu kilichoketi Machi 31, mwaka huu.

Alisema pamoja na kusababisha vurugu katika kikao hicho, pia baadhi ya makatibu walitenda kosa la kuendesha kikao nje ya kikao kilichoitishwa na Katibu wa CCM Wilaya kwa kudaiwa kupatiwa pesa nje ya utaratibu, zilizodaiwa zilitolewa kwa lengo la kuendesha kampeni za kisiasa.

Mwakasumi alisema kabla ya wajumbe hao kuelezwa makosa yao, alishangazwa kuvamia ofisi na kuanza kumtwanga ngumi kila mmoja aliyekuwamo katika kikao hicho, huku nguvu zaidi wakizielekeza kumshambulia kwa ngumi na mateke Katibu wa CCM, kabla ya kuokolewa na askari polisi waliofika muda mfupi baada ya kuibuka tukio hilo.

Aliwataja wajumbe waliowashambulia viongozi kuwa ni makatibu kata Jossephat Mwakajinga (Kajunjumele), Gyrson Mwaikambo (Kyela Mjini), Alex Mwaisombwa (Lusungo) na Ipyana Mwangunga ambaye ni Katibu Mwenezi Kata ya Makwale na kwamba suala lao litafikishwa katika vikao vya juu kwa maamuzi zaidi.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti, baadhi ya makatibu kata hao walisema tangu kuchaguliwa kwa Mwenyekiti wa CCM Wilaya, amekuwa akiendesha na kuitisha vikao kwa shinikizo kutoka kwa mmoja wa viongozi wilayani hapo.

Walisema hata kuitishwa kwa kikao hicho na kamati ya maadili hakukufuata katiba ya chama, ambapo walisema iwapo palitokea tuhuma zozote zilizowagusa wao, Kamati ya Siasa ilipaswa kukaa na kuagiza Kamati ya Maadili ikae na kusikiliza pande zote kabla ya kupelekwa katika vikao vya juu, kitu ambacho hakikufuatwa.
 
Kule speed ya maendeleo ni kubwa sana. Ndiyo maana wanatwangana. Ukilala lala huwezi kumbuka kumtwanga mwezako anayeongea mbofu mbofu

Mikoa ya kusini imechoka na ujinga unaoendelea ndio maana sasa wanademonstrate kwa wapindisha mambo, That's fine
 
Kazi kweli kweli! afadhali tuanzishe boxing team labda wengine watafaidika kuliko kutwangana mangumi shauri ya wanasiasa uchwara.

Ujinga na njaa vikukutana huwa balaa kabisa!

kwi kwi kwi kwi kwi kwi..........unajua nilifikiri Dada yangu alikuwa akisingizia tu....kuwa anapigwa pigwa na shemeji.........aroo this time nikisikia tu Dada yangu kapigwa kutawaka moto........
 
Hi Ogah, ukisikia dada kapigwa utafanyaje? Utamfuata shemeji au nawe utampiga dada wa shemeji yako uliyepanga naye bed-room moja?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom