Elections 2010 CCM watupa mti na jongoo - Butiama

Njowepo

JF-Expert Member
Feb 26, 2008
9,710
2,226
Viongozi kitaifa wakacha kumbukumbu Butiama

na Sitta Tumma, Butiama

MAADHIMISHO ya miaka 11 ya kifo cha hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere jana yaliingia doa baada ya kiongozi wa kitaifa hata mmoja kutoonekana nyumbani kwake, kijijini Butiama kwa ajili ya kuungana na familia yake.
Kitendo cha kiongozi wa kitaifa hata mmoja kutofika Butiama kilionekana kuwashtua wakazi wa kijiji hicho ambao walihudhuria misa iliyofanyika Kanisa Katoliki Butiama kabla ya maandamano ya kuelekea nyumbani kwake eneo la Mwitongo.
Hali hiyo, iliibua minong’ono mingi kwa baadhi ya wananchi waliohudhuria kumbukumbu hiyo, huku Mhashamu Baba Askofu wa Jimbo Kuu la Musoma, Marco Msonganzila, akilaani kitendo hicho.
Katika misa ya maombezi, iliyohudhuriwa na Waziri Mkuu na Makamu wa Kwanza wa Rais mstaafu, Jaji Joseph Sinde Warioba, ambaye kwa namna moja au nyingine ni ndugu wa karibu.
Wengine waliohudhuria ni baadhi ya viongozi wa ngazi za chini mkoani humo; baadhi ya watu walieleza kuwa kitendo cha viongozi wa serikali ngazi ya kitaifa kutohudhuria maadhimisho hayo ni ishara ya kuasi mambo mema na muhimu yaliyofanywa na mwasisi huyo wakati wa uhai wake.
Akitoa nasaha wakati wa mahubiri, Askofu Msonganzila alisema siasa chafu na uchu wa madaraka zimeanza kuhatarisha amani ya nchi.
Alisema inasikitisha kuona baadhi ya vyama kuanza kutamba kwa kusema ushindi ni lazima.
“Hivi sasa nchi yetu imeingiliwa na siasa chafu zenye tamaa, uchu wa madaraka, fitna na ubinafsi kinyume na alivyotaka Nyerere?!” alishangaa askofu huyo.
Kutokana na hali hiyo, Askofu Msonganzila alisema ghasia na vurugu za kisiasa zinazojitokeza sasa zimelenga kuleta machafuko ya kivita iwapo hazitadhibitiwa.
MY TAKE
Naona wamedhamilia kuzika kila kilicho cha Mwalimu kuanzia vitu mpka fikra zake no wonder wameshaanza mwaga damu uku Tarime na Hai kwa kutumia green guard

 
Am sure watajitetea kuwa wako busy na kampeni wakati kila kukicha wanamtaja kwenye izo kampeni
 
JK NA CCM Hawana maslahi kwani FAMILIA ya nyerere wameitupa long time, ndo maana laaana inawatafuna na watakoma, baraka ziko chadema.Tunamuomba Mama yetu mama maria avumilie bado miezi miwili haki zote zitarudi.Tunasikia hata idadi ya walinzi walishapunguzwa pale butiama, sungu sungu ndiyo wanalinda.Tangu JK alivyokwenda mwaka 2005 kujikomba na akapewa zawadi ya biblia na kuchota baraka hajaenda kwa mama nyerere baada ya kupata kasahau, mwaka huu adhabu ataipata 31 oct.
 
Labda JK anadhani ataingia ikulu.... then aende Butiama kujikosha kama alivyofanya 2005
 
Labda JK anadhani ataingia ikulu.... then aende Butiama kujikosha kama alivyofanya 2005

Hata akiingia hatamaliza miaka mi5. Alishashindwa kazi. Amevuruga nchi. Amevuruga hata mtandao uliomuingiza madarakani 2005. Amebaki na kina Malaria Sugu tu. Hao tuta - deal nao October 31.
 
hahaha nimeipenda hii.
watu wanamuenzi Nyerere kwa maneno ili wapate credibility za kutawala
 
CCM wameonyesha daharau ya hali ya juu sana.
Sasa sijui wanamuenzije baba wa Taifa kama ata kwenda kumpa Hi tuu Nongwa.
Naona wengi wao wanaogopa mzimu wake usije wazaba makofi kwa waliyoyatenda so far
 
wangesema nini kama wangeenda? hata kama ni mimi nipo kwenye huo mfumo wa kifisadi nafsi ingenisuta, kamwe nisingethubutu kujisogeza butiama.
 
Back
Top Bottom