tanga kwetu
JF-Expert Member
- May 12, 2010
- 2,193
- 1,434
Nimekuwa nikishangazwa sana na kauli (ninazoweza kuziita kebehi) za washabiki wa CCM humu JF au kwenye chombo kingine chochote cha habari wakiwatuhumu CDM kwa msimamo wao juu ya matokeo yaliyo muweka Kikwete (BA) madarakani. Viongozi wa CDM hususan M/kiti wa Taifa (F. Mbowe) na Katibu Mkuu (Slaa (PhD)) wamefafanua vizuri tena consistently bila kupishana maneno juu ya sababu za kufanya hivyo likiwemo tukio la walkout pale bungeni. Naamini kwa 100% kama Slaa (PhD) (Allah amzidishie hekima) na CDM yake wangetu-pump watu maneno ya kichiochezi wakatio ule wa joto la matokeo, hakika tungekuwa tunazungumza mengine muda huu.....wameamua kutumia njia passive kulalamikia mchakato mzima wa kupatikana kwa 'mshindi' lakini CCM wanawaona CDM wajinga. sasa nafikiri CCM walitaka Slaa (PhD) afanye kama Gbagbo au atuhimize mashabiki wake tuingie mitaani kwa maandamano kupinga votes rigging ya NEC na TISS. naomba CCM muipongeze CDM kwa hekima na uzalendo waliouonyesha hata kutumia passive ways na kukubali maombi ya mabalozi na viongozi wa dini (Islam na Christian) kwamba asisambaze nje documents clear za ushahidi wa uchakachuaji. Hii imetufundisha kwamba next time 'kama mbuai,mbuai'='kama noma,na iwe noma' maana CCM wamekosa staha.....wanaiba then wanaleta nyodo!!!!