BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,789
- 288,015
WAKATI tayari baadhi ya vigogo wakiwemo mawaziri wa zamani wanaburuzwa mahakamani kwa tuhuma za ufisadi na kutumia vibaya madaraka, Rais Jakaya Kikwete, amesisitiza mbele ya jumuiya ya kimataifa kwamba, vita bado ni mbichi.
Kauli ya Rais imekuja wakati Watanzania wakisubiri kuona watuhumiwa zaidi wakiwemo wenye tuhuma mbalimbali za ufisadi, wakiburuzwa mahakamani huku serikali ya awamu ya nne ikisifiwa hadi katika anga za kimataifa kutokana na kuimarisha utawala bora.
Akijibu swali la mmoja wa waandishi kutoka nje mara baada ya maazimio ya Mkutano kati ya Afrika na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), aliyetaka kujua mchakato wa vita dhidi ya rushwa, Rais Kikwete alisema bado unaendelea.
"Vita dhidi ya rushwa inaendelea, ni kweli tumekuwa tukipambana na tatizo hilo, lakini bado tunaendelea," alisisitiza juu ya msimamo huo mbele ya Mkurugenzi Mkuu wa IMF Dominique Strauss-Kahn.
Rais kwa ufafanuzi zaidi, alisema vita dhidi ya rushwa ni wajibu wa serikali kuhakikisha inadhibitiwa.
"Vita dhidi ya rushwa ni wajibu wetu, tunapaswa kupambana na rushwa, tumekuwa tukipambana na bado tunapambana," aliongeza Rais.
Tayari vita dhidi ya ufisadi imeonyesha mafanikio kwa kuwafikisha mahakamani baadhi viongozi wakiwemo aliyekuwa Waziri wa Fedha Basil Mramba, Nishati na Madini Daniel Yona na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Uchumi, Grey Mgonja
Mbali ya hao, pia tayari watuhumiwa wengine akiwemo mfanyabiashara maarufu nchini Jeetu Patel na wengine wamefikishwa mahakamani kwa tuhuma za wizi wa fedha katika Akaunti ya Malipo ya Fedha za Nje (EPA) ndani ya Benki Kuu (BoT).
Pia tayari, aliyekuwa Mkurugenzi wa Utawala na Utumishi (DPA) wa BoT, Amatus Liyumba, amefikishwa mahakamani kwa tuhuma za kuishauri serikali vibaya na kuingizia hasara ya zaidi ya sh 200 bilioni katika mradi wa ujenzi wa majengo pacha ya benki hiyo.
Katika hatua nyingine, Rais alisema serikali imejipanga kupunguza utegemezi wa misaada kutoka kwa nchi wahisani.
Akijibu swali la pili la mwandishi huyo wa kigeni aliyetaka kujua kikomo cha Tanzania kutegemea misaada ya wahisani, Rais alisema ni vigumu kueleza kikomo, lakini nia ni nchi kujitegemea.
"Unauliza kikomo, nasema tumekuwa tukijitahidi kupunguza utegemezi wa nchi wahisani, lengo ni kuweza kujitegemea zaidi katika bajeti yetu," alifafanua Rais.
Alisema serikali imekuwa ijjitahidi kutumia rasilimali za ndani, kuhakikisha inaweza kujijengea uwezo zaidi wa kujitegemea.
Katika hatua nyingine, Mkurugenzi Mkuu Mfuko wa Kuuza Mazao Nje (CFC) Balozi Ali Mchumo, alisema pamoja na nia nzuri ya IMF na jumuiya ya kimataifa kuisaidia Afrika, ni vema sasa ikatangaza namna bora ya kuhakikisha inakuwa na mipango ya dharura kuzisadia nchi za Afrika.
Kwa mujibu wa Mchumo ambaye alikuwa mmoja wa wageni waliohudhuria mkutano kati ya Afrika na IMF, kujadili namna ya kujinusuru na mgogoro wa kifedha duniani, alisema nchi za magharibi zimekuwa zikitoa fedha kuokoa taasisi zao.
Balozi Mchumo alifafanua kwamba, iwapo hakutakuwa na mipango hiyo na ikatokea taasisi za fedha katika nchi za Afrika zikaanguka, Wizara za Fedha hazitaweza kutoa fedha kuzinusuru kama inavyofanya mataifa ya magharibi.
"Nafikiri dhamira ya IMF na mashirika mengine ni nzuri tu, lakini wangekuwa na mpango wa dharura kama ambavyo Rais Kikwete ameamua kuunda Task Force (Kikosi Kazi), kuangalia athari hizo," alisema Balozi Mchumo na kuongeza
" Kwa maana, kule ulaya na Marekani tunasikia wao wanatoa mabilioni kuokoa mabenki yao, huku kwetu Afrika ikifikia hali hiyo Wizara zetu za Fedha hazitaweza kufanya hivyo,".
Mkutano huo ambao ulihudhuriwa na washiriki zaidi ya 300, wakiwemo mawaziri na magavana wa nchi za Afrika na viongozi wengine maarufu akiwemo Katibu Mkuu mstaafu wa Umoja wa Mataifa (UN) Dk Kofi Annan na mfanyabiashara maarufu Mo Ibrahim, ulimalizika jana baada ya kujadili mambo mbalimbali kuhusu namna Afrika inavyoweza kujinasua na anguko la uchumi wa dunia.
Source: Mwananchi