CCM wadhamiria kulinyakua jimbo la Moshi Mjini!

PISTO LERO

JF-Expert Member
Mar 8, 2011
2,819
1,454
Ndugu zangu wana chadema kuna baadhi ya mambo inabidi tuyaseme hatakama yana uma hii ni kwa kukisaidia chama. Tusipokuwa makini tutalipoteza hili jimbo la Moshi mjini.

Kwa taarifa nilizozipata toka kwa mjumbe wa kamati kuu ya ccm ni kuwa chama hicho kimeelekeza nguvu nyingi mkoani huko haswa baada ya kugundua kuna uzaifu katika nguzo kuu za chadema jimboni hapo. Wengi wanajua kuwa huu ni mhula wa mwisho wa mzee wetu Ndesamburo na sasa anaandaliwa meya wa mji Mh. Jafari ili kupokea kijiti hicho, kwa wale ambao wanamfahamu huyu bwana au kumfatilia watakubaliana nami kuwa ameshaonyesha mapungufu kadhaa katika uongozi wake wa manispaa ya Moshi mjini ila tushukuru sana madiwani wenzake ni wavumilivu sana na wamemstahi vya kutosha la sivyo wangesha mng'oa.

Kwanza ni mbishi, jeuri, mbabe na kwasababu ameshajihisi kuwa ni mrisi wa jimbo Jafari amebadilika sana naweza kusema haambiliki anamaamzi ya kibabe na akiamuwa hashauriki, baada ya Ndesamburo kumwachia shughuli za jimbo kuzisimamia kama msaidizi Chadema Moshi mjini imeharibika taswira na kuonyesha mapengo mengi ambayo ccm wanayatumia ipasavyo kujiimarisha kwa siri kubwa na kwa kasi, katika historia ya chadema hapa Moshi mjini haijawahi tokea kukawa na mgogoro kati ya manispaa na wananchi pindi Manispaa ilikiwa chini ya chadema, ni wakati huu wa Mh.jafari naomba chama kimwangalie kwa ukaribu sana.

Nawaomba viongozi wa Chadema Taifa mliangalie hili kwa umakini mkubwa, ccm wamejipanga kikamilifu haswa baada ya kugunduwa hawawezi kilirudisha jimbo la Arusha mjini na Mtoa taarifa huyo amesema hawawezi kuyaachia majimbo yote makubwa ya kaskazini yaende upinzani sisi kama wanachama na wapemzi hatuko tayari kulipoteza jimbo hili mama lililokilea chama mpaka hapa kilipo sasa Mh. Jafari ameshindwa hata kuendesha mikutano ya kukiamsha chama?

Hi ni aibu chama kiko kama hakiko viongozi mkoa wako singizini wakati wenzao hawalali kikiimarisha chama kwa vikao na wazee wa mkoa na sasa upepo unaanza kubadilika taratibu.

Ukitaka kuyaamini haya ninayo yasema hapa fuatilieni chaguzi mbalimbali za CCM mkoa wa Kilimanjaro haswa jimbo la Moshi Mjini mtajua ni nini kinaendelea.
 
Mkuu kama una nia njema na CHADEMA kwanini usiipeleke kwenye vikao vya chama ikajadiliwe kuliko kuileta humu hadharani!!
 
Kuna mtu ananiambia hapa hata lisimamishe jiwe la chadema na ccm jiwe linaibuka na tsunami!
 
Amesahau kuwa 2010 nguvu kubwa ilielekezwa kulikomboa jimbo hilo wakapoteza mengine matatu. By the way marehemu ally alipigwa na FLYING OBJECT. By shilogile.
 
Ukweli ni kwamba hata CCM wafanye lolote katu Moshi mjini ni CHADEMA daima. Hili hata makada wote wa Ccm wanalijua kuanzia Nape mpaka JK, ndio maana ni rahisi sana kwa CCM kuihusisha Chadema na propaganda za kikabila kwani CCM inachukiwa sana Moshi mjini kuliko hata choo kichafu kibovu.

Mikakati yote ya CCM kulichukua jimbo hili iliishia 2010 chini ya secretarieti ya Yusuph Makamba, baada ya CCM kushindwa vibaya kwa kura na kupoteza viti vingi vya udiwani ilivyokuwa inavishikiria hapo kabla pamoja na jitihada kubwa ya kutaka kuvitetea.

Kama kuna raia wanaojua machungu ya CCM na hasira ya kutaka kuona CCM inaondoka madarakani basi fika Moshi mjini.

Nina uhakika hakuna raia wa Moshi mjini anayeweza kuhongwa kwa kitu chochote halafu iipigie Ccm kura.

Watu wa kwanza kuichukia CCM hapo Moshi mjini ni wakinamama na wazee.

Uchaguzi wa 2015 nina uhakika CCM haitapata hata kiti kimoja cha udiwani Jimbo la Moshi Mjini achilia mbali ubunge.
 
Yaani Moshi waichaguwe CCM? wewe unaota ndoto za mchana, muulize Aggrey Mareale alikuwa ameanza harakati za kugombea jimbo hilo kwa tiketi ya CCM wazee wa Kichaga wakamwambia mwanetu kwa heshima ya Mangi Maleale tunakusihi mapema usipote pesa wala muda wako kwenye jimbo hili.
 
yaani moshi waichaguwe ccm? Wewe unaota ndoto za mchana, muulize aggrey mareale alikuwa ameanza harakati za kugombea jimbo hilo kwa tiketi ya ccm wazee wa kichaga wakamwambia mwanetu kwa heshima ya mangi maleale tunakusihi mapema usipote pesa wala muda wako kwenye jimbo hili.

haya ndiyo mazowea yatakayo tugharimu siku za usoni
 
Wamejaribu kuwashawishi watu wengi maarufu ambao ni makada wa CCM ili wajaribu, lakini wahusika walipima maji wakaona ni parefu wakasita, kuanzia Aggrey Malleale, Reginal Mengi nk.
 
Ushauri wako ni mzuri ila kwa taarifa ni kwamba jafari anakubalika kuliko unavodhani Moshi hawaangalii nani Ana gombea Bali wanaangalia chama gani, Ndesamburo sio **** kumpa jafari jimbo anajua anakubalika izo kasoro unazosema ni zengwe la ccm ndio wasiomkubali hususani akina mama kinabo mkurugenzi na timu yake. Kwa taarifa jafari Mimi namjua kuliko umjuavyo wewe Labda imekula na hili kwa chuki zako binafsi na jafari swala la yeye kuto shaurika ni pale mkurugenzi anapotaka amtumie ndipo wanapokosania na jafari kwa ujumla Moshi CDM wa simamishe jiwe ccm imsimamishe Reginald mengi jiwe litashinda kwa asilimia 95.7 na Iyo asilimia 4.3 ni ccm tena watapewa na wasomali wa ushwahilini akina karia and family na mamluki wachache sorounding Moshi. Hata ccm Wanajua Moshi ni territory ya CDM wa kuivunja ni maisha bora kwa Wana Moshi na sio propaganda zako wala za nape na mukama..
 
hakuna mchaga asiejua udhaifu wa CCM
sidhani kama watakuwa wadhaifu kuliachia jimbo kirahisi
Rombo walimwambia Mramba hawataki mwizi, Hai, Vunjo, Moshi Mjini hawadanganyiki
kwa CCM ni sawa na ndoto za mchina 2015 ndio watajuta zaidi kwa ubabe wao na wizi walioufanya kwa miaka yote
 
Hizo nafasi mnarithishana kama magenge ya mbogamboga!!! Yaani imeshaamuliwa nani asimamishwe baada ya Ndesa!!! Halafu mnajiita wapenda mabadiliko. very interesting...
 
Ukweli ni kwamba hata CCM wafanye lolote katu Moshi mjini ni CHADEMA daima. Hili hata makada wote wa Ccm wanalijua kuanzia Nape mpaka JK, ndio maana ni rahisi sana kwa CCM kuihusisha Chadema na propaganda za kikabila kwani CCM inachukiwa sana Moshi mjini kuliko hata choo kichafu kibovu.

Mikakati yote ya CCM kulichukua jimbo hili iliishia 2010 chini ya secretarieti ya Yusuph Makamba, baada ya CCM kushindwa vibaya kwa kura na kupoteza viti vingi vya udiwani ilivyokuwa inavishikiria hapo kabla pamoja na jitihada kubwa ya kutaka kuvitetea.

Kama kuna raia wanaojua machungu ya CCM na hasira ya kutaka kuona CCM inaondoka madarakani basi fika Moshi mjini.

Nina uhakika hakuna raia wa Moshi mjini anayeweza kuhongwa kwa kitu chochote halafu iipigie Ccm kura.

Watu wa kwanza kuichukia CCM hapo Moshi mjini ni wakinamama na wazee.

Uchaguzi wa 2015 nina uhakika CCM haitapata hata kiti kimoja cha udiwani Jimbo la Moshi Mjini achilia mbali ubunge.
Duuh!Karia bado yupo tu?kule wanapandisha bebdera ya ccm ili waendele kuuza gomba na madili mengine.
 
Ungekuwa na nia nzuri ungelipeleka katika chama. Mpiganaji maridadi hajioneshi hadharani. Huna hoja
 
Mbona leo simuoni Zomba hapa na yule naniii...hehehe

Anyway taarifa ni nzuri, intellejensia ya chama itafanyia kazi
 
Nadhani maoni ya Mleta mada yaheshimiwe, na yawe kama darasa! Ni busara sn kukubali mapungufu pale yanapokuwepo.
Namheshimu sn member @T2015CDM na kwa uzoefu wake na cdm naamini ana substance!
Kama ana ukaribu na vikao vya ndani vya chama km ambavyo mnadai basi aliseme huko pia.
 
Ndugu zangu wana chadema kuna baadhi ya mambo inabidi tuyaseme hatakama yana uma hii ni kwa kukisaidia chama. Tusipokuwa makini tutalipoteza hili jimbo la Moshi mjini.

Kwa taarifa nilizozipata toka kwa mjumbe wa kamati kuu ya ccm ni kuwa chama hicho kimeelekeza nguvu nyingi mkoani huko haswa baada ya kugundua kuna uzaifu katika nguzo kuu za chadema jimboni hapo. Wengi wanajua kuwa huu ni mhula wa mwisho wa mzee wetu Ndesamburo na sasa anaandaliwa meya wa mji Mh. Jafari ili kupokea kijiti hicho, kwa wale ambao wanamfahamu huyu bwana au kumfatilia watakubaliana nami kuwa ameshaonyesha mapungufu kadhaa katika uongozi wake wa manispaa ya Moshi mjini ila tushukuru sana madiwani wenzake ni wavumilivu sana na wamemstahi vya kutosha la sivyo wangesha mng'oa.

Hivi na CDM nako mmejenga utamaduni wa kurithishana vyeo? Wacha muda ukifika wanachama wapambane na atakayewapiku wenzake apeperushe bendera ya chama.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom