CCM Waanza siasa uchwara uchaguzi wa Arumeru!!

Dr Matola PhD

JF-Expert Member
Oct 18, 2010
56,530
93,110
Siasa chafu zaanza Arumeru Mashariki Send to a friend
Friday, 16 March 2012 21:31
0digg

00001asion.jpg
Mgombea Ubunge Jimbo la Arumeru Mashariki kwa tiketi ya CCM, Sioi Sumari akisalimiana na wananchi wa kijiji cha Nambala, Kata ya Kikwe alipowasili kufanya mkutano wa kampeni za uchaguzi mdogo wa jimbo hilo, jana kijijini hapo. Picha na Edwin Mjwahuzi

Neville Meena, Arumeru
SIASA chafu za kupakana matope zimeanza kujitokeza katika kampeni za uchaguzi mdogo wa ubunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki ikiwa ni wiki moja tu tangu kuanza kwake.

Siasa hizo za majitaka zinavihusisha zaidi vyama vyenye upinzani mkali, CCM kinachomnadi mgombea wake, Sioi Sumari na Chadema ambacho kinampigia debe, Joshua Nassari. Vyama hivyo kwa nyakati tofauti vimekuwa vikishutumiana kwa ukiukwaji wa maadili.

Miongoni mwa malalamiko yanayotolewa ni kusambazwa kwa nyaraka za kashfa, wafuasi kufanya fujo katika mikutano ya vyama pinzani, watu kuzuiwa kushiriki kwenye mikutano ya kampeni, matumizi ya lugha chafu dhidi ya viongozi wakuu wa vyama pinzani kwenye majukwaa ya kampeni na kusambazwa kwa taarifa za uchochezi zinazowashawishi wananchi wasishiriki kampeni.

Kadhalika, kumekuwapo na malalamiko ya matumizi mabaya ya picha iliyopo kwenye kipeperushi cha polisi kinachohamasisha umma kutii sheria bila shuruti, kwamba baadhi ya watu wamekuwa wakitumia picha hiyo kuwatisha watu wasihudhurie mikutano ya kampeni.

Picha hiyo ni ile inayomwonyesha kijana ambaye anaburutana na polisi, picha ambayo Chadema wanadai kwamba CCM wameibatiza kwamba ni matukio yanayofanyika kwenye mikutano ya Chadema hivyo kuwatisha watu wasihudhurie kampeni za chama hicho.

CCM kwa upande wake kinalalamika kwamba vijana kinaodai kuwa ni wa Chadema, wamekuwa wakifika kwenye mikutano ya chama chao na kuwafanyia fujo kikiahidi kuwachukilia hatua bila hata kuwafikisha polisi.

Hata hivyo, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, Thobias Andengenye alisema jana kuwa vipeperushi vya polisi vimekuwa vikigawanywa kwa wananchi wote na si sahihi kuhusisha suala la utii wa sheria na itikadi yoyote ya kisiasa.

“Sisi tunasimamia utii wa sheria na vipeperushi hivyo vimekuwapo tangu mwaka jana na vinatawanywa nchi nzima, hapo Arumeru vinagawanywa sana sasa kwa sababu kuna mikusanyiko mikubwa ya kampeni lakini hamasa hii itaendelea hata baada ya uchaguzi,” alisema Andengenye na kuongeza:

“Utii wa sheria hauwezi kuwa ni kwa Chadema au CCM, au chama kingine chochote, kutii sheria ni jukumu la kila raia wa nchi hii na yule anayeingia hapa nchini, kwa hiyo watu watii sheria wawapo kwenye mikusanyiko ya kampeni au kwingineko maana kulazimishwa kutii sheria ni fedheha.”

Kuhusu hali ya amani na usalama kwenye mikutano ya kampeni, kamanda huyo alisema: “Mpaka sasa hakuna matukio yoyote ya uvunjifu wa amani na hatujapata taarifa za aina hiyo, mambo yakiendelea hivi nadhani uchaguzi utakuwa mzuri.”

Msimamizi wa uchaguzi Jimbo la Arumeru Mashariki, Trasias Kagenzi alisema juzi kuwa tayari amepokea baadhi ya malalamiko ya kukiukwa kwa maadili kwenye mikutano ya kampeni na kwamba yatafanyiwa kazi kupitia kamati ya maadili ambayo inaundwa na vyama vyote vya siasa vinavyoshiriki uchaguzi huo.“Tunayo kamati ya maadili ambayo tayari tumeiunda na mimi ndiye mwenyekiti wake, kwa hiyo malalamiko ambayo yamewasilishwa rasmi kwangu tutayajadili na kuyatolea uamuzi katika kamati hiyo,” alisema Kagenzi.

Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Julius Mallaba alisema usambazaji wa nyaraka zozote zinazohusu uchaguzi bila kibali cha msimamizi wa uchaguzi ni kinyume cha sheria.

“Sheria ziko wazi, katika ngazi ya jimbo nyaraka zote yakiwamo mabango na vipeperushi lazima zipate idhini ya msimamizi wa uchaguzi, kwa madiwani lazima idhini ipatikane kutoka kwa wasimamizi wasaidizi na kama ni uchaguzi wa Rais, basi Ofisi ya Tume ya Uchaguzi ndiyo yenye mamlaka ya kuidhinisha,” alisema Mallaba na kuongeza:

“Kwa hiyo hairuhusiwi kwa namna yoyote mtu, chama au taasisi yoyote kusambaza taarifa zinazohusu uchaguzi huu, bila idhini ya msimamizi wa uchaguzi, hivyo tunaomba vyombo vya dola vitusaidie.”

Malalamiko Chadema
Meneja Mwenza wa Kampeni za Chadema katika uchaguzi huo, Vicent Nyerere akituhumu CCM kwamba kimesambaza waraka mitaani unaowakashifu viongozi wao wakuu.

Waraka huo ambao gazeti hili limeuona una kichwa cha habari: “Chadema na Masela,” kikiwataja viongozi kadhaa wa chama hicho hasa wabunge wasiooa au kuolewa kwamba wanamuiga Katibu Mkuu wa wao, Dk Willibrod Slaa ambaye wanadai kwamba aliasi kazi ya ukasisi hivyo kufukuzwa.

Kadhalika, waraka huo unamuonya mgombea wa chama hicho, Joshua Nassari kuachana na Chadema kwa maelezo kwamba atachafua sifa ya familia yake ambayo baba yake ni mchungaji.

Waraka huo ambao mwishoni umeandikwa “…..itaendelea wiki ijayo,” unakihusisha Chadema na ukabila na kwamba ni shirika lisilo la kiserikali (NGO) ya kabila la Wachagga ambalo limekuwa likipokea misaada kutoka kwa wafadhili wa nje.

Hata hivyo, Nyerere alisema Chadema kimeupuuza waraka huo kwani maneno yake yanawiana na kauli alizoziita chafu ambazo alidai kwamba zimekuwa zikitolewa na viongozi wa CCM kwenye kampeni.

“Huu ni ujinga na wala hauwezi kuwasaidia kushinda kwani hakuna jipya ni yaleyale kila siku, waache wapoteze muda sisi tunapigana kutwaa jimbo na hilo tuna uhakika nalo,” alisema Nyerere.

Mkurugenzi wa Bunge na Halmashauri wa Chadema, John Mrema alisema kumekuwapo kwa makundi ya watu ambayo yamekuwa yakiegesha magari karibu na viwanja ambako Chadema kinafanyia mikutano ya kampeni kuwazuia watu wasihudhurie.

“Katika maeneo mengine tumekuta taarifa kwamba mabalozi wa nyumba kumi wanazunguka kuwashawishi watu wasifike kwenye mikutano yetu kwa kuwatisha kwamba kutakuwa na vurugu, hizi ni siasa chafu ambazo hatuwezi kukubaliana nazo,” alisema Mrema.

Malalamiko CCM
Meneja wa Kampeni za CCM, Mwigulu Nchemba aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa chama chake hakina muda wa kuwachafua Chadema na kwamba hizo ni dalili za kutapatapa baada ya wapinzani wao hao, kubaini kwamba watashindwa kwenye uchaguzi huo.

Badala yake Nchemba alisema Chadema ndiyo wamekuwa wakiendesha siasa chafu kwa kuwatuma vijana wao kufanya fujo kwenye mikutano ya CCM na kutoa tahadhari kwamba watawashughulikia hata bila kuwafikisha polisi.

“Hili nalisema hata kwa wanachama wa CCM kama wapo wanaofanya vitendo hivi; siyo lazima uende kwenye mkutano wa kampeni, kama hutaki au mambo wanayozungumza yanakukera, basi lala nyumbani usiende na siyo kwenda kuvuruga mikutano yao,” alisema Nchemba na kuongeza:

“CCM ni chama kikubwa, mikutano yetu ina watu wengi kwa mfano, pale Mbuguni tulikuwa na watu zaidi ya 5,000 sasa wewe mtu mmoja, wawili au watatu mkija kufanya fujo halafu ule umati ukawageukia mtaweza kupona kweli? Sasa Chadema wawaambie vijana wao waache la sivyo tutawashughulikia.”

Kuhusu CCM kwamba kinapanga njama za kuwazuia watu wasihudhurie mikutano ya Chadema Nchemba alisema: “Hawa wenzetu wanatafuta huruma kwa wananchi, sisi CCM tuwazuie watu gani kwa sababu hawana watu, tumemwona mgombea wao akikosa watu sehemu nyingi tu, kwa hiyo wasitafute visingizio.”

Wakati wa uzinduzi wa kampeni za CCM Jumatatu wiki hii, zilizofanyika kwenye Uwanja wa Ngaresero, Usa River, Katibu Mkuu wa chama hicho, Wilson Mukama pia alidai kwamba kulikuwa na njama za kukichafua chama chake kwa kuwavisha sare za chama hicho baadhi ya watu ambao wangetumika kufanya fujo.

Hata hivyo, Chadema kupitia viongozi wake wamekanusha kuwatuma vijana wao kwenye mikutano ya CCM na badala yake kudai kwamba chama hicho tawala kimekuwa kikipingwa na wananchi kutokana na lugha chafu za wapiga kampeni wake.


 
"CCM ni chama kikubwa, mikutano yetu ina watu wengi kwa mfano, pale Mbuguni tulikuwa na watu zaidi ya 5,000 sasa wewe mtu mmoja, wawili au watatu mkija kufanya fujo halafu ule umati ukawageukia mtaweza kupona kweli? Sasa Chadema wawaambie vijana wao waache la sivyo tutawashughulikia."
mwaka huu hadi uishe tutasijia majina /sifa nyingi awali walisema ni chama cha mungu
 
Hapa nimesoma nilichokiona Chadema na CCM wote wanalalamika tu, nadhani wana Arumeru ndio wataamua wenyewe nani wampe ubunge.
 
hivii unaanza kutapatapa mapema wakati bado game ni bichi vyama husika viache woga vifanye kampeni za kistaarabu ili kuwapa nafasi ya maamuzi wananchi hapo tarehe mosi april
 
tunaomba polisi wasiharibu uchaguzi wa wana-arumeru mashariki. hakuna mwenye fujo ila kuna watu wanatafuta jinsi ya kuiba kura. vijana kazi kwenu kulinda kura. kumbukeni tulivyolinda pale manispaa arusha, ubungo loyola na kule mwanza. jamani sitasahau. kura zilishatosha kwa kumzunguka jamaa wa system lakini bado mpaka mwisho walikuwa wanatafuta jinsi ya kuchakachua
 
Hapa nimesoma nilichokiona Chadema na CCM wote wanalalamika tu, nadhani wana Arumeru ndio wataamua wenyewe nani wampe ubunge.
Kwa nini husemi kiini cha malalamiko haya ni nini?. Katoe kwanza tongotongo ndio uje hapa jukwaani.
 
Ni vigumu sana kuitenganisha CCM na siasa za maji machafu ya chooni . Ni kama ilivyo vigumu kuutenganisha moyo na uhai wa binadamu. No siasa chafu no CCM.
 
Hizi ni aina ya siasa za DARUSO - UDSM, naona wameanza kuhamishia mambo ya vyuo mitaani!! Anyway, inabidi kuwa smart zaidi kumshinda adui yako.
 
hiyo ya kuwashughulikia wanaoleta fujo bila pasi kuwafikisha kwenye vyombo vya usalama itawaghalimu kama si kufikia hatua ya kutoana uhai..
 
WanaArumeru, sikilizeni, angalieni na mfanye maamuzi kwa ajili ya maendeleo yenu. Msikubali kuyumbishwa na vishawishi hasa vya pesa na vitu kama hivyo. Mgombea akinunua kura kwenu mtazilipa kwa damu zenu.
 
Hapa nimesoma nilichokiona Chadema na CCM wote wanalalamika tu, nadhani wana Arumeru ndio wataamua wenyewe nani wampe ubunge.
Kweli mkuu wameru ndiyo wanajua nani?wampe sisi yetu macho na masikio siku ya uchaguzi
 
CCM haina k2 tena zaid ya kufanya siasa chafu zasy hata Nape na Jk walishakaa pembeni toka zamani kwami wanajua kwamba kushiriki siasa za kibakwata kama za CCM ni kujochafua mwenyewe.
 
Back
Top Bottom