CCM vs CHADEMA:Kipi ni chama cha mafisadi?

pepsin

JF-Expert Member
Apr 23, 2015
3,465
6,109
Siku za nyuma ilikuwa ni wazi kabisa kuwa CCM kilikuwa ni chama cha mafisadi,wezi wa mali ya nchi hii.Orodha ya mafisadi iliyotolewa na aliyekuwa katibu mkuu wa CHADEMA na mwanasheria wa chama Dr Slaa na Tundu Lissu kwa mpangilio ilikoleza ufisadi wa CCM.
Mchakato wa uchaguzi mkuu ulimtoa mmoja wa waliotajwa kwenye orodha kutoka CCM na kwenda CHADEMA.Huo ulikuwa ni mwanzo wa debate,kwamba ni chama kipi cha mafisadi? Mpaka sasa makada wa CCM wanawaona CHADEMA kama mafisadi kwa uwepo wa huyo mtu na kujaribu kuhamisha magoli!!
Kuondoa mzizi wa fitina,lazima namba zitumike kwa kutumia ileile orodha ya aibu ya Dr.Slaa ambayo wanaCCM ndio wanaitumia zaidi kuwashambulia CHADEMA.
  • Gavana wa Benki Kuu (BoT), Marehemu, Dk. Daudi Balali (CCM)
  • Mbunge wa Bariadi, Andrew Chenge (CCM)
  • Basil Mramba aliyekuwa mbunge wa Jimbo la Rombo (CCM) na Waziri
  • Gray Mgonja aliyekuwa Katibu Mkuu mstaafu, Hazina (CCM)
  • Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Patrick Rutabanzibwa(CCM)
  • Nazir Karamagi aliyewahi kuwa Mbunge(CCM)
  • Mbunge wa Musoma Vijijini, Nimrod Mkono (CCM)
  • Mbunge wa Igunga, Rostam Aziz (CCM)
  • Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa (CHADEMA)
  • Rais mstaafu, Benjamin Mkapa(CCM)
  • Rais wa Sasa, Jakaya Kikwete(CCM)
Kwenye orodha ya mafisadi 11 waliotajwa na Dr Slaa pale Mwembeyanga,kwa sasa CCM inao 9(+mareh.Balali!!) ilhali CHADEMA wanaye mmoja tu.Kama hii orodha ndio kigezo na kama kweli kila aliyetajwa alikuwa fisadi,ni wazi CCM bado wana kazi kubwa ya kuhusu ufisadi nchini.

mytake:Tumuunge mkono kila anayepiga vita ufisadi wakiongozwa kwa sasa na mh.JPM bila kuwabeza wapiga kelele kama Tundulisuu
 
Wewe raia wa kijani unaejificha ficha,jua kuwa asili ya mafisadi wote hapa Tanzania ni CCM
 
Haki ya mama, nimeamini kumbe CCM imejaa mafisadi na ni mtambo wa kuwatengeneza. Ukitaka kujua hili subiri Mbunge atangaze kukihama chama, utayaona yote. Mbunge wa Singida Magharibi Elibariki Kingu kwa sasa ni msafi kwa sababu yupo CCM na bado anapikwa afuzu kuwa fisadi kamili, lakini akitangaza kuiacha CCM utaiona habari hii hapa chini:

"Ripoti ya GAG imechambua na kuainisha jinsi Mbunge wa singida Magharib Elibariki Kingu alivyohusika kwenye upotevu wa zaidi ya million 101 katika wilaya ya Igunga kipindi yeye akiwa mkuu wa wilaya.

Ripoti inasema kuwa mwaka 3013 serikali kupitia kwa waziri wa habari utamaduni na michezo aliwahi kupeleka Tshs Million 95 kwa ajili ya mfuko wa vijana katika wilaya hiyo,halmashauri nayo ilichangia Tshs milion 5,lakini cha ajabu kilichokusudiwa hakikufanyika! pamoja na hayo yote bado mwaka 2014 walipewa zaidi ya Tshs Million 6 kwa ajili ya safari ya mafunzo nje ya nchi huko china ambapo CAG anasema hakuna sehemu yeyote inayoonesha kuwa safari hiyo ilifanyika.

UHUSIKA WA ELIBARIKI KINGU.

Wakati huo Mh Elibariki Kingu akiwa mkuu wa wilaya ya halmashsuri ya Igunga ndiye alikua Mlezi wa vikundi vya vijana ndani ya wilaya hiyo muda wote na ripoti ya CAG inasema kuwa akaunti yenye jina lake ilihusika katika upokea pesa hizo"
 
Kati ya vyama hivyo chama kimoja ni groomer and donor wa mafisadi kingine ni recipient wa qualified mafisadi. Sijui chama kipi ni donor na kipi recipient kati yao. Bado nagoogle majibu!
 
Kwenye orodha ya mafisadi 11 waliotajwa na Dr Slaa pale Mwembeyanga,kwa sasa CCM inao 9(+mareh.Balali!!) ilhali CHADEMA wanaye mmoja tu.Kama hii orodha ndio kigezo na kama kweli kila aliyetajwa alikuwa fisadi,ni wazi CCM bado wana kazi kubwa ya kuhusu ufisadi nchini.

Mkuu, kulingana na CCM, Chadema ni chama cha mafisadi ambao ufisadi wao unajulikana pale tu wanapohama CCM na kwenda Chadema.

Na kulingana na Chadema, CCM ni Chama cha mafisadi ambao ufisadi wao unaisha pale tu wanapohama CCM na kwenda Chadema.

Sasa tumia akili zako kuchanganua hapo, maana siku zote huweki thread zenye mantiki kama hii.
 
Hahaha ama kwel akil kichwan
Escrow,rada,lile bonge la almas,etc zote zilitekwa mafisadi tokea CHADEMA
AKil kichwan
 
Jamani ndugu zangu, yote haya yanatokea wapi?.mafisadi, mafisadi, ivi, Mahakama ya Mafisadi si ipo tayari?. Mafisadi wapelekwe Mahakamani jamani. Ni Mahakama pekee ndiyo inayoweza kisheria kumtia mtuhumiwa hatiani. Tusijaribu kuwahukumu watu nje ya Mahakama.
 
Kama unataka kujua ufisadi wako usijulikane basi endelea kukaa CCM
Kama unataka uwe fisadi kwa kipindi cha Magu,basi hama ccm,dai katiba mpya,mwambie anadalili ya udikteta na mseme kijana wa Kolomije
Kama unataka kuacha ufisadi basi hama ccm pia.
 
Siku za nyuma ilikuwa ni wazi kabisa kuwa CCM kilikuwa ni chama cha mafisadi,wezi wa mali ya nchi hii.Orodha ya mafisadi iliyotolewa na aliyekuwa katibu mkuu wa CHADEMA na mwanasheria wa chama Dr Slaa na Tundu Lissu kwa mpangilio ilikoleza ufisadi wa CCM.
Mchakato wa uchaguzi mkuu ulimtoa mmoja wa waliotajwa kwenye orodha kutoka CCM na kwenda CHADEMA.Huo ulikuwa ni mwanzo wa debate,kwamba ni chama kipi cha mafisadi? Mpaka sasa makada wa CCM wanawaona CHADEMA kama mafisadi kwa uwepo wa huyo mtu na kujaribu kuhamisha magoli!!
Kuondoa mzizi wa fitina,lazima namba zitumike kwa kutumia ileile orodha ya aibu ya Dr.Slaa ambayo wanaCCM ndio wanaitumia zaidi kuwashambulia CHADEMA.
  • Gavana wa Benki Kuu (BoT), Marehemu, Dk. Daudi Balali (CCM)
  • Mbunge wa Bariadi, Andrew Chenge (CCM)
  • Basil Mramba aliyekuwa mbunge wa Jimbo la Rombo (CCM) na Waziri
  • Gray Mgonja aliyekuwa Katibu Mkuu mstaafu, Hazina (CCM)
  • Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Patrick Rutabanzibwa(CCM)
  • Nazir Karamagi aliyewahi kuwa Mbunge(CCM)
  • Mbunge wa Musoma Vijijini, Nimrod Mkono (CCM)
  • Mbunge wa Igunga, Rostam Aziz (CCM)
  • Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa (CHADEMA)
  • Rais mstaafu, Benjamin Mkapa(CCM)
  • Rais wa Sasa, Jakaya Kikwete(CCM)
Kwenye orodha ya mafisadi 11 waliotajwa na Dr Slaa pale Mwembeyanga,kwa sasa CCM inao 9(+mareh.Balali!!) ilhali CHADEMA wanaye mmoja tu.Kama hii orodha ndio kigezo na kama kweli kila aliyetajwa alikuwa fisadi,ni wazi CCM bado wana kazi kubwa ya kuhusu ufisadi nchini.

mytake:Tumuunge mkono kila anayepiga vita ufisadi wakiongozwa kwa sasa na mh.JPM bila kuwabeza wapiga kelele kama Tundulisuu
MAFISADI WALIZALIWA CCM YA KALE but WANAHIFADHIWA NA KUSTAAFIA CHADEMA....
 
Tuwapongeze wanachama hawa wakongwe wamefanya mambo makubwa sana katika chama chetu na tuwatie moyo ili wazidi kutoa mchango wao katika chama!

Mungu awatie nguvu

Sema Amen
 
Jibu hilo hapo
 
Attachments

  • Screenshot_2017-11-01-11-50-35.png
    Screenshot_2017-11-01-11-50-35.png
    268.7 KB · Views: 23
Back
Top Bottom