Kila anayejaribu kushauri, kuonya, kukemea baadhi ya mapungufu ya CHADEMA mtasema anatumiwa na CCM. Hivi kama mtu au chama unakipenda utakaa kimya tu na kukisifia hata kama unaona kinakoelekea siko? Sasa hivi Jaji Warioba anajaribu kuwa juu kidogo ya siasa za vyama. Jana alivikosoa vyama vyote ikiwemo CCM yake. Wewe umeyaona maoni haya ya CHADEMA tu. Kwa namna ulivyoleta, utaungwa mkono sana tu humu JF. Umeongea lugha ya wengi humu.
si mlisema chama cha msimu!kushindana kwa sera. Sera zipi? Ninachojua ni kwamba chadema wamaekuwa tu wakosoaji bila kueleza ni kipi walichoandaa ambacho watawaletea wananchi iwapo wataingia madarakani. Ni kulia lia na kulalamika wakati kwenye majimbo wanayoyaongoza hali ni hoi bin taabani na wala huoni kama kuna kitu kinachoweza kuipambanua chadema na ccm na kuwapa watu matumaini kwamba chama hicho ni mbadala wa ccm.
Ama Kweli Chadema mnaonesha ni jinsi gani heshima Huyo unaye mtukana na Sawa na baba yako na pia aliwahi kuwa kiongozi Wa nchi hii. Hivi nikweli hakuna alichokifanya alipokuwa madarakani? Au umezaliwa juzi hujuwi tulikotoka? Achani siasa za chuki
Nimesoma habari ya Jaji Warioba katika gazeti la Raia Mwema la leo, nikagundua kuwa CCM bado inafikiri kuwa Watanzania kuwa ni wajinga kiasi hicho, wanachofikiri wao ni kuwa bado kuna watu wanaweza kufikiri vizuri kwa ajili ya watu wengine.
Kingine nilichogundua ni kuwa CCM wanaweweseka, na CCM ndio itakayoleta vurugu nchi hii kwa kuwa haiko tayari kushindwa kidemokrasia yamejidhihirisha katika mazungumzo hayo ya Jaji Warioba.
Lingine nililojifunza ni kuwa CCM sasa wanatumia mbinu zozote zile zidi ya CHADEMA kuwa kuwa haiwezi tena kushindana na CHADEMA kisera imebakia kuropoka, sasa wamebuni mbinu za kuwatumia watu maarufu kama Warioba kujifanya wanazunguzia mustakabali wa nchi bila upendeleo huku wakiingiza maoni ya kuiponda CHADEMA.
Warioba anasema Chadema kule igunga wasifikiri wanapanda chati ile inaweza kuwa nguvu ya soda halafu anaingiza propaganda za CCM za udini na kuwa CHADEMA si chama cha watu.
Tumuulize Warioba atupe data zinazoonyesha kuwa kule si kupanda chati bali ni nguvu za soda si kuzungumza kisiasa na kinadharia. Wengine sisi si wanasiasa tunataka analysis and fact.
Angalizo kwa CHADEMA ni kuwa kuna nguvu iliyo nyuma ya pazia ya kuiangamiza ambayo ni kubwa sana, sasa hivi wanawatumia wakongwe hao wameanza na Warioba, atafuata Salim, gazeti la Raia Mwema limeshachukuliwa! Kumbuka Warioba na Jenerali na Mkapa walikuwa marafiki wakubwa sana kabla ya wawili wao hawajagombana.
Mimi nimefanya kazi kwa Jenerali Ulimwengu wakati wanaanzisha gazeti la Mtanzania nawafahamu vizuri.
Watanzania tusikubali kuruhusu watu kufikiri kwa niaba yetu, CCM hawako tayari kuona chama kingine kwa kuwa wanaogopa utawala mwingine kwa kuwa wanajua katika CCM hakuna aliyemsafi kamili. Watajifanya kujikosoa wenyewe ili wabaki madarakani ili kulinda madhambi yao. Tuendelee kupambana mapaka ukombozi kamili upatikane.
Mungu ibariki Tanzania.
kuna wakati alikua anajifanya kuwasema mafisadi wakamkumbusha pesa za meremeta Hana la kufanya ili apone inabidi aungane nao na si kuwapinga maana hatA yeye ni fisadi mzee!.KUNA MAONI YA MTU MMOJA KASEMA UKIINGIA CCM KUTOKA NI VIGUMU.Yawezekana fedha za meremeta zimeisha
Ndoto za mchana mchana hizo.Waache waendelee kujifariji.CHADEMA inasonga mbele,mdogo mdogo mpaka Ikulu,Kikwete anatoka,Slaa anaingia!!
Ndoto za mchana mchana hizo.
Mkuu Mahindi yameisha yote igunga? kuna kata bado zinayahitaji please!! give us update on this asap.Ndoto za mchana mchana hizo.