Rev. Kishoka
JF-Expert Member
- Mar 7, 2006
- 4,526
- 1,529
Nimekubali, kama ilivyovigumu kwa Ufisadi kuondoka Tanzania kutokana na mfumo wake kuingilia jamii ya Tanzania na kukubalika kuwa ni kitu cha kawaida, ndivyo jinsi CCM ilivyo kwa Watanzania, mtaji wenye faida usioleta usumbufu au kuwalazimisha Watanzania kubadilika hivyo ni heri kwa Watanzania kuendelea kuwa na Zimwi CCM na si mtu mwingine.
Watanzania ni wagumu sana kukubali mabadiliko, iwe ni mfumo wa maisha, utendaji kazi au jambo lolote. Mfano kama ikiwa ndani ya CCM wanaendeleza mfumo dume wa miaka ya 1970 uliotuletea chama kimoja na mgombea mmoja na leo hii yeyote anayeamka kupingana na aliyeko madarakani huonekana ni adui, vivyo hivyo kaugonjwa haka kametambaa kwa Watanzania.
Kwa Watanzania wengi, kuendelea kuongozwa na CCM ni heri ya kuendeleza mfumo wao wa kimaisha ambao wameshauzoea na kuridhika nao.
CCM ni chama ambacho kimeondoka kuwa chama makini na kuwa chama kilicho mkao wa tupo tupo, kuna uzembe, uvivu, ubangaizaji, utegemezi, kila jambo lina sababu la kuhalalisha udhaifu na visingizio vingi.
Ama ni Chama ambacho hakina nia ya kuleta maendeleo ya kweli zaidi ya kuendeleza maisha na mfumo wa Ubabaishaji pamoja na kuwa kuna maandiko elfu yanaoonyesha kuwa kuna rasimu ya kuleta mapinduzi na maendeleo kuonddoa Umasikini, Ujinga na Maradhi.
Lakini kama CCM ilivyo, ndiyo Watanzania tulivyo, inapokuja kwenye utendaji, ni wazito, mgando na hatuna wepesi wa kuwa wenye ufanisi, umakini au ufuatiliaji wa hali ya juu. Kama CCM ya sasa kupenda njia za mkato na utegemezi, ndivyo Watanzania tunavyoendekeza dezo, misheni na kuchukia kutoka jasho, iwe ni kufikiri au kufanya kazi.
Si kwamba hatufanyi kazi, bali tunafanya kwa kiasi tu, kwa kujihimu na si kwa malengo ya muda mrefu au kwa nyongeza ili kujihakikishia akiba na uhakika wa keshokutwa achilia mbali mwezi na mwaka ujao.
Hivyo si cha ajabu kuona kuwa Watanzania tunaivumilia CCM kwa kuwa ni Chama pekee ambacho tunafanana nacho na tunaweza jitambulisha rasmi nacho, kimfumo, kiutendaji, kimaadili na hata kimipango.
Leo hatuwaamini CHADEMA, NCCR, CUF, TLP na ahta kama ingekuwa ni CCJ au Mgombea binafsi kwa kuwa hatujui kama wakija hawa watalazimisha tubadilike na kuanza mfumo mpya ambao utatuwajibisha kwenda zaidi ya kile cha mazoea (above and beyond), kuwa tutakuwa fanisi, tutaachana na utegemezi na itatubidi kubadilika kabisa.
Kama walivyo Wazee wetu ambao hawataki kubadilika na kung'angania mfumo wa kale, ndivyo sisi kama Watanzania tulivyoridhika na kupenda kuiona CCM inaendela maana tunafanana nayo.
Tunaogopa kumpa dhamana ya uongozi "Kichaa" atakayekata mirija yetu ya utegemezi, uzembe, uvivu, ubangaizaji, umisheni tauni, ufisadi, urasimu, rushwa, wizi, kuridhika na unyonge, umasikini na hata ujinga.
Kama ndugu zetu Watindiga, walivyokataa kuachana na maisha asili, ndivyo kama Taifa tunavyoogopa kumpa dhamana mtu mwingine maana tunaogopa umande na kutoka jasho.
Basi ni wazi Vyama vya Upinzanina yeyote mwenye dhamira ya kuiongoza Tanzania ambaye si kutoka CCM, ana kazi ngumu na inabidi aanze kazi na safari hii si kusubiri wakati wa uchaguzi au kuchagua vitu viwili au vittu kuongea na Watanzani abali ni kuishi maisha na kuonyesha vitendo vya mabadiliko vinavyoleta maendeleo ya kweli na hivyo kujenga wivu mzuri wa maendeleo na si inda, chuki au kubezana.
Nasikitika kuwa huu ni ukweli usiokwepeka na ni wengi wenu mtakata na kusema si sahihi, lakini jibu moja ni tawapa, subirini matokeo ya uchaguzi mkuu wa mwaka huu, kuthibitisha kuwa si lile la udhaifu wa Wapinzani kama nilivyoongelea kwa muda mrefu au mchezo mchafu wa CCM kwenye uchaguzi, bali ni woga wa Watanzania wa mabadilikouliojenga mapenzi ya ajabu kwa CCM pamoja na udhaifu na kushindwa kwa CCM kutuuondoa kutoka Umasikini, Ujinga, Maradhi, Utegemezi na kuishi kwa maadili.