CCM na magari ya uchaguzi...

Wewe unaonekana kujua mengi kuhusu uingizaji wa magari haya. Hebu weka wazi na siyo kuwashutumu watu wadaku wakati wewe mwenyewe unaonekana pia mdakaji. Kama si mdakaji mkuu hebu eleza ilikuwaje hasa kuhusu ununuzi huu wa magari, vinginevyo na wewe huna unalolijua kaa kimya watu waeleze wanachofahamu. Au ndiyo kampeni zimeanza?

mbona zimeanza siku nyingi tu mkuu? kwa sasa ni za chini kwa chini japo wengine uvumiliv umeaisha wanaanza kupiga rasmi hadharani. mi nitajitokeza hadharani kwa nguvu kubwa februari, na kati ya watu nitakaowaomba kura ni pamoja na wewe!


haya magari ni mwendelezo tu wa kampeni.

happy new year
 
Kuwa mkuu wa fedha na mipango wa ccm si lazima uambiwe kila kitu kinachotoka hazina ya taifa kwenda ccm. mambo mengine hayahitaji msululu wa watu kujua wao watakabidhiwa magari na fadha tu, vimetoka wapi sio kazi yao, kazi yao itakuwa ni kupanga jinsi gani watumie.

Wala usishangae ukijasikia kuwa pesa za kununulia magari zimetoka kwa 'Wafanyabiashara fulani'.
In return, wanapata nafuu ya kodi, tenda zenye akili, kuwa karibu na 'mzee' etc...
 
Namuomba Mungu na miungu yoote habari hii iendelee kuwaa tetesi hivyohivyo kani kama tumefikia hapo mwenyekiti anafanya jambo kubwa kama hilo na KM wake hajui, Mungu apishe mbali kwani itakuwa ni hitimisho kwamba SASA TUMEKWISHA!!

Na wewe una yako tu, wakishindwa kuelewana CCM, wewe unakwishaje? Siyo ni jambo la kulishangilia kwamba walau mwisho wa CCM umesogea? Though habari yenyewe ilivyokaa ni kidaku zaidi. Ina maana mpango wa uagizaji wa hayo magari umewekwa kwenye faili gani ambalo Makamba hawezi kuliona? Au tumesahau kwamba Makamba ndo mtendaji mkuu wa chama?
 
Wala usishangae ukijasikia kuwa pesa za kununulia magari zimetoka kwa 'Wafanyabiashara fulani'.
In return, wanapata nafuu ya kodi, tenda zenye akili, kuwa karibu na 'mzee' etc...

Pesa hizi ni za walipa kodi wa Tanzania zilizofisadiwa katika EPA, Meremeta, Mwananchi, Kagoda n.k.
 
Nimezisikia habari kuwa siri aliyotoboa Dr.Slaa juu ya CCM kuagiza magari 200 imemuhuzunisha sana Makamba maana hakuwa na tip juu ya kuwepo kwa mpango kama ule. Ni JK tu ndiye aliyekuwa katikati ya mpango mzima. Muhabarishaji anathibitisha zaidi kuwa ndo maana hata majibu ya Makamba yalikuwa dhaifu sana wakati ya Chiligati na Makalla yamekuwa rojorojo.

Je, kuna uongo au ukweli wowote ndani ya tetesi hii? Na
Je, kwa nini JK amenza kumficha hata Katibu Mkuu wake wa Chama?

Kama habari hizi ni za kweli basi iko kazi kwenye hiki chama.Ni ufisadi kwa kwenda mbele
 
kwa style hii fedha chafu kwenye kampeni haziweze kukwepwa kwani hakuna mahali taratibu zinafuatwa tunaambiwa chadema kuna udikteta wa mbowe tlp usiseme huu wa kikwete utakuwa ni kubwa yao mungu aepushe hili lisiwe kweli vinginevyo watz tumekwisha
 
Kama imefikia hapo basi sasa ndiyo kwaheri hivyo kwani Serikali imekwisha kuwa ngumu hii. Ila kila siku nasema inabidi vijana tuchukue hii nchi, hii tabia ya kupeana madaraka mara mtoto mara shemeji siyo nzuri, kaka embu tupe vizuri hilo dili lilivyokuwa kwani inaonekana wewe unajua vizuri hiyo dili.
 
CCM Shikamoo!!!
Kwa unyenyekezu na ushawishi mkubwa ulituomba utuongoze kwenda nchi ya ahadi sasa umegeuka mnynyaji wa hata damu yetu.
UNATISHA CCM.
Nimeambiwa Shetani hashughuliki tena kuitesa Tanzania. Kazi ya kuleta umasikini, magonjwa, kuendeleza ufisadi na kuufurahia ujinga shetani ameikasimu kwa CCM.
 
Back
Top Bottom