CCM msitulazimishe vita mkoani Singida kwa kutumia vijana wenu wa green guard

Suphian Juma

Senior Member
Apr 2, 2019
133
546
CCM NA SERIKALI YENU MSITULAZIMISHE VITA SINGIDA.

Na Suphian Juma.

Nipo kwetu mkoani Singida kusalimia kwa takribani wiki sasa. CCM tunajua mna kambi mnayowapa mafunzo ya kijeshi vijana wenu wa GREEN GUARD mliowakusanya kutoka kata takribani zote za mkoa wa Singida. Tunajua kambi ilipo, idadi ya vijana wanaowafundisha, posho mnaowalipa, ukatili mnaowafundisha na tunajua LENGO la mkakati huu unaovunja Sheria za vyama vya Siasa na Katiba yetu

Ni kuwatumia vijana hawa kuunajisi Uchaguzi haramu mlioshupalia kuitishwa na Tume ya Uchaguzi Jimbo la Singida Mashariki (Jimbo halali la Mbunge Tundu Lissu) unaotarajia kufanyika tarehe 31 July 2019, na pia Kuuvuruga Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Kuu ujao ili mshinde kiharamu.

Na mbaya na kusikitisha zaidi katika kuonesha madhara ya kuanzishwa kwa Kambi hii ya kishenzi inayooana na vikundi vya kigaidi duniani kama AlShabab, IS na kadhalika Leo 6, July 2019, bila kuogopa imevamia Mkutano halali wa ndani wa chama cha CHADEMA na kuwapiga viongozi na wanachama wa Kikao hicho na kuamua kujichukulia na kutokomea pasipojulikana na viongozi wa Chama hicho akiwemo Mwenyekiti wa Chama Jimbo la Singida Mashariki huku Jeshi la Polisi hadi naandika taarifa hii fupi jioni hii halijafika eneo la tukio licha la kujulishwa mapema mchana kwa kigezo eti "HAWANA MAFUTA YA GARI".

WanaSingida na Watanzania tunasema huu sio Utanzania, Utu wala Ustaarabu waliotuachia waasisi wa Taifa hili, hivyo kwakuwa Katiba yetu inatutambua Wananchi kama wenye mamlaka ya juu zaidi katika nchi kuliko Serikali, Chama wala Rais, hivyo TUNAWATAKA mvunje hiyo Kambi HARAKA, LASIVYO kama Jeshi la Polisi na vyombo vingine vya Ulinzi na Usalama vikishindwa kuwadhibiti msije mkatufikisha wananchi katika hatua ya kusababisha TUKAWAUMIZA HAO WADOGO ZETU. MSITULAZIMISHE VITA AMBAYO KIMSINGI ITAWAFUTA KATIKA RAMANI YA TANZANIA.

Suphian Juma
WanaSingida
6th July, 2019
IMG-20190706-WA0025.jpeg
 
Hiki chama cha majambazi kimeishiwa sera, sasa imebaki vitisho na ubabe
Ndiko tumefikia. Itafika mahali kama wewe siyo CCM unabaguliwa hata kuawawa lakini hakuna marefu yasiyo na ncha. Hata Hitler, Idd Amini, Mobutu na wengine walikuwa hivyo lakini leo wako wapi?
Wao waendelee na vitisho lakini majibu yatapatikana tu. Waliomaliza chuo wanazidi kurundikana mtaani bila kazi, hakuna nyongeza ya mshahara, biashara nying zinakufa, korosho imeshabuma, subiri pamba na mazao mengine yabume. Tutaelewana tu
 
Tanzania ya mitandaoni na ile isiyo ya mitandaoni ni Tanzania mbili tofauti

Tanzania ya mitandaoni ni yenye vurugu, fujo na ugomvi wa kila aina.

Watanzania hawa hawa wanaopigana vita ya maneno mitandaoni wakizima tu data kwenye simu zao utawakuta wanacheza draft/bao pamoja hapo shule ya msingi Uhuru.
 
Umelewa, na hatujui umelewa nini? Amka kumekucha ndugu
Tanzania ya mitandaoni na ile isiyo ya mitandaoni ni Tanzania mbili tofauti

Tanzania ya mitandaoni ni yenye vurugu, fujo na ugomvi wa kila aina.

Watanzania hawa hawa wanaopigana vita ya maneno mitandaoni wakizima tu data kwenye simu zao utawakuta wanacheza draft/bao pamoja hapo shule ya msingi Uhuru.
 
Tanzania ya mitandaoni na ile isiyo ya mitandaoni ni Tanzania mbili tofauti

Tanzania ya mitandaoni ni yenye vurugu, fujo na ugomvi wa kila aina.

Watanzania hawa hawa wanaopigana vita ya maneno mitandaoni wakizima tu data kwenye simu zao utawakuta wanacheza draft/bao pamoja hapo shule ya msingi Uhuru.
Nchi kubwa zinaamini mitandaonkuliko wewe usiejua hata it
 
Jambo la ajabu ni kwamba hayo magreen guard yanaongoza kwa maisha magumu,wengi wao wana maisha magumu gamba la kakakuona,wana afya mbovu na kila jambo la kuonewa huruma.Pu**bavu zao kabisa!
 
NO NO NO ifike mwisho sasa na nyinyi kulalamika kila siku hapana sipendi kuona mtu anaonewa kiasi cha kuzalilishana kwa nn kila siku ni nyi nyinyi tu wa kulalamika . hapo sasa ndipo wengine tunauliza kamanda lwakatele uko wapi mbona wanachana wako wanaonewa na wewe ndiye mkuu wa kurungezi ya usalama ndani ya chama. nendeni kwenye mkutano ya ndani na ZZK ili wakija tu mnaanza nao. inakera sasa
 
Back
Top Bottom