CCM kwaiva: Kama si Salim ni Mwandosya

Jamaa uliye Arusha, mbona umetoa kali leo, yaani huyo Mzenji na Mtanganyika wanaweza mchakamchaka, du! Tanzania ya leo haihitaji watu wa kimya kiasi hicho. Tunahitaji kiongozi shupavu ambaye hata ukimtazama anavyoongea, na usoni anaonyesha hivyo!
 
Si timu ya ushindi ya 2005 ilitwambia kwamba Salim alimMwangosi Karume na hivyo tukamkataa ndo tukamchukua jamaa wavtimu hiyo sasa leo mtatwambia kwamba hakumMwangosi au mtasemaje?? Hapana aisee ccm muwe serious kama hii kitu ni kweli. Kama ni kweli na kama kutakuwa na fair uchaguzi basis ukawa watatangazwa washindi tatu asubuhi siku ya uchaguzi. Kizazi hiki hakimjui Salim
 
Hata aje nani, ukweli utabaki kuwa ukweli ya kuwa ccm imejaa uvundo!
Mwaka 1962, mara tu baada ya Tanganyika kupata uhuru, Mwalimu Nyerere akiwa Waziri Mkuu wa Kwanza wa Tanganyika huru alijivua wadhifa wake, akamweka Rashidi Kawawa kuwa Waziri Mkuu, na yeye akarudi vijijini kukijenga upya chama cha TANU ambacho ndicho kilichoongoza harakati za kupigania uhuru.
Ukweli ni kwamba, ccm sasa hivi inahitaji kujishusha, irudi kwa wananchi ili iweze kujitengeneza upya. Huenda (?) ikirudi kivingine baada ya miaka kadhaa, ikiwa na uongozi mwingine, na sera zingine wananchi wanaweza kuipa ridhaa ingine.
Kwa mwaka huu, na kwa shida walizo nazo wananchi walio wengi, ccm jiandaeni kuangukia pua!
Wale ambao wana mvuto kwa wananchi mmewakejeli na kuwatusi. Ni kweli Dr. Salim hana makundi, na hana kashfa, lakini chama chake... (ashakum si matusi)
 
Kumbe kelele zote na mizengwe ya Nape dhidi ya Lowassa ni kumtengenezea mazingira "biological father" wake Mwandosya?
 
Kama isingekuwa utaratibu mbovu uliozoeleka hapa Tanzania, Kwamba akitoka wa dini hii anaingia wa dini ile, namkubali sana Mzee Salim. Hana makuu mzee wa watu yeye kapigwa sana mishale na wazee wa Mtandao. Ameitwa kila aina ya majina lakini mzee Salim alionyesha ukomavu mkubwa ktk siasa za maji taka zilizokithiri huko Ccm.

Ni Mzee pekee toka ccm wa upande ule mwingine wa dini anayesemekana hana chembe yoyote ya Udini, Ni tunda lililosalia la Baba wa Taifa Mwl. Nyerere (R.I.P) linaloendelea kuishi ktk misingi ya falsafa ya Mwalimu, hana kitu kinachoitwa kisasi nafsini mwake. Hilo tumeliona kwa kuchaguliwa kwake kuwa mjumbe wa Cc ya Ccm, pamoja na kutukanwa na kukashifiwa na mkubwa wa kundi la Wanamtandao lakini pindi alipotangazwa kuwa mteleule wa kamati hiyo aliupokea kwa unyenyekevu mkuwa uteuzi ule na kamwe hakunyanyua japo ukucha kumparura yeyote kwa kukashifiwa kwake hapo awali..!!!

Waweza kumpata nani mwenye moyo kama huo hapa Tanzania ktk kizazi hiki?

Na kwa bahati mbaya umri hausimami.!

BACK TANGANYIKA

mkuu kwani salim ahmed ni dini gani?
 
Ingawa nipo Arusha,naendelea kudokezwa yanayochomoza vikaoni (ndani ya CCM) na katikati ya makada wa haja. Nimedokezwa kuwa CCM inaelekea kugeukia kwa wanachama wawili ambao kura zao hazikutosha mwaka 2005 na 2010, Dr. Salim Ahmed Salim na Profesa Mark Mwandosya. Nikaambiwa kuwa makada hawa wawili wana kila sifa za kuwa Rais wa Tanzania na hawana makuu wala makundi. Pia,wako mbali na kashfa ya aina yoyote iliyoitafuna taifa.

Ninaaminishwa kuwa ripoti mpya ya CAG imempiga mweleka Dr John Pombe Magufuli kwakuwa Wizara yake ililidanganya Bunge na kufisidi mamilioni ya fedha (bilioni 262). Dr. Salim na Prof. Mwandosya sasa wanatazamwa kama dawa pekee ya kuiponya CCM katika kipindi ambacho chama na Serikali yake kimeandamwa na kashfa za kifisadi za kila aina na rangi. Nikaambiwa kuwa Salim na Mwandosya watashawishiwa kuchukua fomu za kugombea kipenga kitakapopulizwa.

Hatimaye CCM yetu imepata pakutokea. Walionidokeza na kuniambia ni wabobezi wenzangu chamani na nawaamini. Afadhali papoe jamani!

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Arusha)

Porojo
 
umechambua standard mkuu,japo mi sio gamba

Asante mkuu japo me can chama ila najikita katika kufanya uchambuzi bila kuwa biased tatizo langu ni moja me naamini katika falsafa na sio ushabiki. Ushabiki hujengwa kwa fedha, mahaba na umaarufu lakini me ninaamini kiongozi mzuri ni yule mwenye falsafa anayoiishi na kuiamini ambaye akipewa nchi tunaweza kuona ataipeleka katika uelekeo UPI na je ni sahihi? Watu wengi hasa vijana wa zama hizi tumeishia kuwa mashabiki wa wanasiasa but ukiuliza je huyo unayemshabikia ana falsafa ipi na je unaamini katika falsafa hiyo wengi hawawezi kujibu zaidi ya kutoa hoja nyepesi. Tuanze kuchagua viongozi kwa kile wanachoamini, kukisimamia na kukiishi na sio kwa sababu ya mvuto, ukwasi ama umaarufu tutofautishe unazi ww mpira na siasa .
 
umechambua standard mkuu,japo mi sio gamba

Asante mkuu japo me sina chama ila najikita katika kufanya uchambuzi bila kuwa biased tatizo langu ni moja me naamini katika falsafa na sio ushabiki. Ushabiki hujengwa kwa fedha, mahaba na umaarufu lakini me ninaamini kiongozi mzuri ni yule mwenye falsafa anayoiishi na kuiamini ambaye akipewa nchi tunaweza kuona ataipeleka katika uelekeo UPI na je ni sahihi? Watu wengi hasa vijana wa zama hizi tumeishia kuwa mashabiki wa wanasiasa but ukiuliza je huyo unayemshabikia ana falsafa ipi na je unaamini katika falsafa hiyo wengi hawawezi kujibu zaidi ya kutoa hoja nyepesi. Tuanze kuchagua viongozi kwa kile wanachoamini, kukisimamia na kukiishi na sio kwa sababu ya mvuto, ukwasi ama umaarufu tutofautishe unazi ww mpira na siasa .
 
Mwandosya mwenyewe anajua kuwa rais ajaye ni Lowasa,wabishi ni Nape nauye na Paulo makonda ambao baada ya october watakimbilia msumbiji kwa Nyusi
 
Back
Top Bottom