CCM katika tope zito Arumeru

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,534
13,225
TAARIFA kwamba Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CC), imeamuru kura za maoni katika uchaguzi mdogo wa jimbo la Arumeru Mashariki urudiwe, sio za kufurahisha hata kidogo.
Hatutaki kutaja majina ya wagombea watakaochuana katika duru la pili la kura za maoni, lakini sababu inayotajwa ya mchakato huo kurejewa upya eti kati ya wagombea wawili walioongoza, hakuna aliyepata asilimia 50.
Kwetu sisi, hiyo siyo sababu ya msingi kwani CCM ilishapitisha wagombea walioshinda kwa kura moja katika chaguzi zilizopita.
Lakini sababu halisi ya kurejea mchakato huo ni makundi ya urais mwaka 2015, uliosababisha mmoja wa wagombea hao kudaiwa kuwa sio Mtanzania.
Sababu ya pili ni mchezo mchafu uliofanyika awali wakati wa kura za maoni. Rushwa ilitembezwa waziwazi kiasi cha mgombea mmoja kujitoa.
Tunachukua nafasi hii kuiambia CCM kwamba imekuwa mfano mbaya katika uchaguzi huo na kuna uwezekano mkubwa kwamba hata mchakato mwingine wa marejeo ya kura za maoni ukawa mbaya zaidi.
Tukiangalia mchezo unaoendelea kwenye kile kinachoelezwa kuwa kusaka urais na harakati chafu zinazofanywa na wahusika wakati bado kuna miaka mitatu kufikia uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, tunashindwa kuamini kama kweli hii ndiyo CCM iliyoachwa na misingi mizuri ya uongozi na Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
CCM imekuwa kama vile haina mkubwa, kila mtu anaamua lake, inapofika wakati wa uchaguzi ni vurugu tupu, rushwa ndiyo sifa pekee ya mgombea kuchaguliwa, hakika kwa hili CCM imekuwa chama cha mfano mbaya.
Sisi tunajiuliza swali moja, kama CCM imeshindwa kusimamia kura zake za maoni katika misingi ya kidemokrasia na kuepuka rushwa ni kwa vipi inaweza kusimamia misingi ya haki wakati wa kampeni za uchaguzi wenyewe?
Kwa namna yoyote, hatuoni kampeni huru na za haki Arumeru Mashariki. Hatuoni dhamira ya kweli ya CCM kutaka uchaguzi huo uwe wa haki.
Tunaonya: kama CCM itaamua kucheza rafu wakati wa kampeni katika uchaguzi huo, kuna hatari kubwa ya hali ya utulivu na amani kutoweka kwenye kampeni hizo.
Watanzania wanataka kushuhudia uchaguzi ulio huru na haki Arumeru Mashariki ili kudumisha sifa yetu ya kuendelea kuwa kisiwa cha amani na utulivu.

Source:Tanzania Daima
 
Hawa CCMwanvyopeleka mfumo mzima wa uongozi na utawala kwa mfumo mbovu wa kisiasawataleta vita itayosababisha umwagaji damu hakika
 
Natafuta hoja hapa siioni. CCM bado inatafuta mgombea. Imeamua kurudia kura ya maoni ili kujiridhisha nani Kati ya wanachama wake wawili anakubalika. Hata chadema mwanzoni walisema mgombea wao angekuwa Nassari , akaanzisha mchango wa sh 11m. Baadae wakaghairi na kuanza mchakato wa kura za maoni Kama ccm. Hili la chadema halisemwi. Linalosemwa ni ccm ccm ccm na kurudia uteuzi ambalo ni kawaida tu ndani ya ccm au chama chochote kinachotafuta ushindi. Hoja hizi hazina mshindi wowote kwamba uchaguzi unaweza usiwe wa Amani. Najiuliza Amani itavunjikaje kwa kurudia kura ya maoni!!!!!
 
Back
Top Bottom