nice 2
JF-Expert Member
- Aug 10, 2011
- 747
- 520
Lugola akaangwa kwenye 'caucus' ya CCM kwa kauli dhidi ya Mkulo Bungeni
Habari ifuatayo imenukuliwa kutoka kwenye gazeti la MTANZANIA:
Aliyekuwa Waziri wa Fedha, Mustafa Mkulo ambaye ni Mbunge wa Kilosa (CCM) amemtolea lugha chafu za matusi ya nguoni mbele za watu, mbunge wa Mwibara Kangi Lugola (CCM).
Tuhuma za Mkulo ziliibuka juzi mjini Dodoma wakati wa kikao cha wabunge wa CCM, kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Pius Msekwa, chini ya Uenyekiti wa Waziri Mkuu Mizengo Pinda.
Pamoja na mambo mengine, iliibuka hoja ya kujadili kitendo cha Lugola kumwandama Mkulo ndani ya Bunge.
Lugola alitakiwa kutoa utetezi wake kwa kile kilichodaiwa ni kukiangusha Chama Cha Mapinduzi (CCM) mbele ya wananchi.
Kwa mujibu wa chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya kikao hicho, wa kwanza kuibuka na ndani ya kikao hicho ambacho kiliitwa cha kujadili tuhuma za ufisadi kwa wabunge, alikuwa Mbunge wa Simanjiro, Christopher Ole Sendeka aliyelaani hatua ya Lugola kumlipua Mkulo Bungeni.
"Ndugu yangu, kikao hiki kilikuwa na mambo kadhaa lakini kubwa ni kumjibu Lugola, wa kwanza alikuwa Ole Sendeka, ambaye alisimama na kulaani hatua kuhusu mwongozo wa Spika dhidi ya Mkulo...
"Kutokana na hali hiyo, ilimfanya Mbunge wa Sikonge, Said Nkumba (CCM), kuinuka na kuzidi kupigilia msumari kwa Lugola, tena alikilani hatua ya kuwasilisha hoja hiyo kwa kutaja jina la Zitto Kabwe, ndani ya kikao...
"Hatua ya kumtaja Zitto, Nkumba, aliitafsiri kama ni kumpa ujiko, huku akilaumu kwa nini Mkulo aandamwe wakati si mbunge.
Hoja hiyo, iliwafanya wabunge kuzidi kuchagia kwa wingi, huku Mbunge wa Nkasi Kaskazini, Ally Kessy Mohammed (CCM), akipinga hatua hiyo na kusema katu hawako tayari kufungwa midomo na Serikali ya chama chao.
"Ndugu yangu, hili jambo lilizidi kuchukua sura mpya kila wakati huku nae Mbunge wa Mpendae, Salim Hassan Turky (CCM), ambaye alisema kuisema Serikali ndani ya Bunge ni sawa na si kudhalilisha mbele ya wananchi...
"Hata hivyo, ilionekana kama wamejipanga kuhusu hili maana hata mbunge wa Lushoto, Mlalo Henry Shekifu (CCM), aliunga mkono kauli iliyotolewa na Lugola, huku akiwataka viongozi wa Serikali pamoja na chama kutoa muongozo dhidi ya wabunge...
"Baba weeee hukuwepo ndani ya kikao, lakini malaika wako walikuwepo, kwani mara baada ya kusimama Lugola, aliweka wazi namna alivyodhalilishwa na Mkulo, mbele za watu kwa kutukanwa matusi ya nguoni, ambayo katu hayawezi kusema wala kuandikika gazeti...
"Kutokana na uteezi wa mbunge uyo wa Mwibara, kila mtu alibaki ameacha kinywa wazi na Waziri Mkuu Pinda kulazimika kutumia kila aina ya busara ili hali isizidi kuwa mbaya katika kikao hicho," kilisema chanzo hicho cha kuaminika kwa MTANZANIA.
Hata hivyo, hali hiyo ilionekana iliwalenga baadhi ya wabunge ambao huonekana wakorofi, ilimlazimu Waziri Mkuu Pinda, kumpa nafasi maalumu ya upendeleo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utawala Bora, George Mkuchika, kusema neno la mwisho katika kikao hicho.
"Ni dhahiri Mkuchika, alikuwa na ajenda iliyoandaliwa kwa ajli ya kuitetea Serikali, eeeee alisema huyo hakuna mfano...
"Mkuchika, alisema ni marufuku kuanzia jana (juzi), mbunge yoyote kwa CCM kuishambulia Serikali ndani ya Bunge na mbunge atakayefanya hivyo lazima atajadiliwa na chama...
"… tena alisema hivi sasa ana nafasi nzuri ya kufanya kazi na endapo atatokea mbunge na kuanza kuisema vibaya Serikali atamshughulikia kwa kuwa hivi sasa yupo wizara mayo ina vyombo vya ulinzi na salama kama TAKUKURU, tena huku akiungwa mkono kila mara na Waziri Mkuu Pinda.
"Alisema kuanzia sasa takuwa nafutilia mijadala yote ya bunge pamoja na kusoma hansard za Bunge, ili kufitilia mchango wa kila mbunge, na atakayeisema CCM, atachukuliwa hatua za kinidhamu...
"Waziri Mkuu, alisema haiwezekani unakuta mtu anachangia lakini hakitaji chama cha Mapinduzi (CCM), hata mara moja..
"Hata hivyo pamoja na yote kubwa ushahidi alioutoa Lugola, namna alivyotukanwa matusi ya nguoni na Mkulo, hakika kijana wangu huwezi kuyasikia wala kuyatamka mbele ya watu," kilisema chanzo hicho kilipokuwa kikizungumza na gazeti la MTANZANIA.