CCM itawatishia wabunge wake hadi lini?

Kama kweli Mkuchika amesema hayo basi tuna tatizo kubwa sana. Mkuchika atatumiaje vyombo vya ulinzi na usalama kama TAKUKURU kushughulikia wabunge anaoona wanapingana na CCM? Kubambikizia kesi maybe?

Mpelekeni shule huyo ili wamwelemishe demokrasia maana yake nini na nini wajibu wa vyombo vya dola
 

"Ni dhahiri Mkuchika, alikuwa na ajenda iliyoandaliwa kwa ajli ya kuitetea Serikali, eeeee alisema huyo hakuna mfano...

"Mkuchika, alisema ni marufuku kuanzia jana (juzi), mbunge yoyote kwa CCM kuishambulia Serikali ndani ya Bunge na mbunge atakayefanya hivyo lazima atajadiliwa na chama...

"…
tena alisema hivi sasa ana nafasi nzuri ya kufanya kazi na endapo atatokea mbunge na kuanza kuisema vibaya Serikali atamshughulikia kwa kuwa hivi sasa yupo wizara mayo ina vyombo vya ulinzi na salama kama TAKUKURU, tena huku akiungwa mkono kila mara na Waziri Mkuu Pinda.

"Alisema kuanzia sasa takuwa nafutilia mijadala yote ya bunge pamoja na kusoma hansard za Bunge, ili kufitilia mchango wa kila mbunge, na atakayeisema CCM, atachukuliwa hatua za kinidhamu...

"Waziri Mkuu, alisema haiwezekani unakuta mtu anachangia lakini hakitaji chama cha Mapinduzi (CCM), hata mara moja..

.

Blackbold: Huu ni ushahidi vyombo vyetu vya usalama vinavyotumika kulinda maslahi ya wanasiasa badala ya wananchi wote.

Hii inahalalisha kusuka upya vyombo vyetu vyote vya usalama haraka iwezekanavyo.
 
Huyu Lugola anaonekana ni shujaa sana sijui kwa nini hakihami hicho chama kinachokufa,nimemsikia akiwa na mbunge wa kisesa wakiapa kuwa lazima wawe na msimamo wakati wa kuchangia burget..jamani makamanda waukweli hameni mje cdm kama hamuamini mtashangaa 2015.
 
Huyu Mkulo bana si amulaumu aliyekuwa bosi wake aliyemwambia Mdhibiti Mkuu apeleke ripoti bungeni ijadiliwe,madudu afanye yeye ,halafu amutamfute mbaya,hapana mla rushwa hana haki ya kusimama mbele ya kikao na kuanza kulalamika ,hivi kweli Mkulo baado ana jeuri ya kutaka kujisafisha?na baado wanataka kitumia dodoki CCM kujisafisha ?da huyu naye wa Simanjiro amsubiri Millya amukaange kumbe ni bonge la mnafiki,ngoja wamsendekee mbali
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom