CCM inawa-train mabaunsa zaidi ya 200 Kiomboi Singida - Kuelekea uchaguzi Igunga

ngurati

JF-Expert Member
Feb 14, 2011
221
240
Wanajanvi,

Habari za uhakika nilizonazo, CCM Imeweka kambi ya vijana mabunsa zaidi ya 200 huko Kiomboi Singida kuwaanda kwa ajili ya kuvuruga na kufanya vurugu kwenye mikutano ya wapinzani Igunga.

Hii ni baada ya kuona upepo umekaa vibaya na CCM inaelekea kushindwa uchaguzi huo, wameamua ku-invest kwenye maandalizi ya kufanya vurugu, kupiga na hata kuua watu kwenye maeneo ambayo upinzani utaonekana kuwa na nguvu ili kuwatisha wanaIgunga.

My. take
Ukweli haujawahi kushindwa na mwamko uliopo Tz sasa ni mpango wa Mungu, kamwe nguvu ya umma haijawahi kushindwa kwa nguvu ya mtutu na risasi.
 
Asante kwa tahadhari hiyo, lakini hao mabaunsa ni watanzania ambao wanapatwa na hali ngumu ya maisha yanayosabishwa na serikali hii? Au labda wao hali yao itakuwa nzuri kwani watapewa ujira mzuri na mwajiri wao kwa kazi hiyo lakini mwisho wa yote wataaibika wote.
 
Pongezi kwa taarifa mkuu,lkn wananchi wakiamua hao mabaunsa hawatafanya lolote. kumbuka kilichowatokea mabaunsa wa kampuni ile ya udalali kule ckumbuki ni tegeta inshu ya ardhi/nyumba.. the good thing people of our days can not be threatened easily hasa kama unawadhulumu haki yao hata wa vjjn. Juzi kati kule bukoba walitaka kumpiga Mkuu wa kituo (ocs)Nyakanazi kwa kujiingiza katika kashfa ya uuzaji ardhi yao
 
Hata Mwanza walikuwa na mabaunsa lakini wakaambulia kushindwa. Acha wajifurahishe tu.
 
Tegeta mabaunsa waliuawa kisa ni kutaka kuhamisha watu kwa nguvu eti wamevamia shamba la tajiri. Huko Igunga wananchi wanataka maendeleo na si kuchagua magamba yanayowaza posho tu. Tusubiri tuone.
 
Wamuulize Gadafi alikuwa na mabaunsa wangapi na amebakiwa na wangapi! ngoja wawalete uone Gelette zitakavyofanyakazi. Chadema hatuogopi kwenda kwenye uchaguzi mdogo.
 
narudia kusema mwigulu ni mtu corupt hapa tz kwa kiwango cha juu, ikiwa taarifa hii ni kweli, atakuwa anahusika moja kwa moja na zahama litakalowapata hao mabaunsa.
 
Wanajanvi,

Habari za uhakika nilizonazo, CCM Imeweka kambi ya vijana mabunsa zaidi ya 200 huko Kiomboi Singida kuwaanda kwa ajili ya kuvuruga na kufanya vurugu kwenye mikutano ya wapinzani Igunga.

Hii ni baada ya kuona upepo umekaa vibaya na CCM inaelekea kushindwa uchaguzi huo, wameamua ku-invest kwenye maandalizi ya kufanya vurugu, kupiga na hata kuua watu kwenye maeneo ambayo upinzani utaonekana kuwa na nguvu ili kuwatisha wanaIgunga.

My. take
Ukweli haujawahi kushindwa na mwamko uliopo Tz sasa ni mpango wa Mungu, kamwe nguvu ya umma haijawahi kushindwa kwa nguvu ya mtutu na risasi.

Vyama vya upinzani wakachukue uzoefu wa wananchi wa kule Wazo waliovamia maeneo ya viwanja vya watu na kuweza kuwasambaratisha mabaunza waliokodishwa na wengine kuaga dunia!
 
Asante kwa taarifa mkuu. Hao mabaunsa lazima wajue kuwa hawawezi kuidhibiti nguvu ya umma, wenzao kule maeneo ya tegeta walionja nguvu ya umma wengine walikufa, wengine ni vilema na wengine walinusurika baada yta kutimua mbio sasa huko Igunga watakimbiiia wapi?etu Macho
 
Hii ni kwa mujibu wa taarifa zilizofanyiwa uchunguzi na DR Wilbrod Peter Slaa.
 
Mkuu nijuze hii ya OCS Nyakanaze ikoje,mi mdau wa maeneo hayo,nifumbue macho mkuu

Pongezi kwa taarifa mkuu,lkn wananchi wakiamua hao mabaunsa hawatafanya lolote. kumbuka kilichowatokea mabaunsa wa kampuni ile ya udalali kule ckumbuki ni tegeta inshu ya ardhi/nyumba.. the good thing people of our days can not be threatened easily hasa kama unawadhulumu haki yao hata wa vjjn. Juzi kati kule bukoba walitaka kumpiga Mkuu wa kituo (ocs)Nyakanazi kwa kujiingiza katika kashfa ya uuzaji ardhi yao
 
Kama hii ni kweli, siyo jambo la kuchukulia kirahisi tu. Watu 200 ni wengi na siyo wote wanaoweza kutunza siri zao. Zitafutwe picha na taarifa sahihi kuhusu hili. Haya ni mambo ambayo mda mfupi ujao maelezo yake sahihi yatatumika kuwahukumu hawa watawala waliovimbiwa. Ktk chaguzi ndogo mbalimbali watu wamekuwa wakiumizwa, kuteswa na kuuliwa na watawala na tunaangalia tu, ifike mahali watanganyika tuguswe na kukataa mauaji na uharibifu unaofanywa na watawala ktk sehemu mbalimbali za nchi yetu.
 
kama walishindwa kuwatumia ubungo wale majambazi ya mbezi na msigani wataweza kuwatumia hao igunga, we ngoja lazima tupambane nao vilivyo
 
Back
Top Bottom