CCM inafaa kutuongoza tena mwaka 2020?

Tukumbuke nchi hii ina vizazi tofauti tofauti vya CCM
ukiangalia vzr kuna vizazi kadhaa vya CCM
vizazi hivi vilizaliwa tofauti ktk miaka ya
1. 1977
2. 1980
3. 1984
4. 1987
5. 1990
6. 1992 (mara Mbili)
7. 1994
8. 1995
9. 1997
10. 2015(Magufulinism)

CCM inavizazi zaidi ya kumi. Viongozi wanabadilika hasa pale wanapogundua mapungufu yao.

Leo Utasema kuna chama gani kimebadili viongozi wake na kuweka vizazi vipya kumi tofauti?

Mfumo wa sasa wa jpm(new magufulinism) hakika ni mfumo wenye nguvu.

Huwezi kua na kiwanda unataka kuzalisha bidhaa ziuzike sokoni ilhali bado unatumia spea za kizamani.

Viwanda hapa ni vyama, spea ni hao viongozi.
Hii hoja haina mashiko kama bado hatushindani kimfumo tunaangalia jina.

Sahau CCM, sahau CHADEMA, nk chunguza mifumo na vizazi ndani ya chama.

Utapata jibu nchi hii nani atashinda 2020

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hata vikao vya ndani mnaviogopa hao watu wa vijijini watapatikanaje? Kulikuwa na kikao cha CHADEMA walitumwa Askari kwenda kuwafurusha, siku za karibuni CCM wamefanya mkutano kijiji cha Kinyika huko Iringa vijijini hakuna walichofanywa.

Unadhani hivi sasa fuko la hazina liko salama?
Acha porojo mbona lema anafanya kila siku?
 
nygax CCM inakubali kila kitu kinacholetwa na chama hicho na kukataa kila kitu kinacholetwa na vyama vingine, na hii haikuanza leo bali ni tangu mwaka 1992, na bahati mbaya wakati mwingine CCM hutumia nguvu za dola kupingana na mawazo ya vyama vingine.

Turudi kwenye mada: Kama huo uchafu wote unaodai unasafishwa na Magufuli ulisababishwa na CCM iwepo madarakani ni kwa nini CCM ipate uhalali wa kutawala wakati kila ikiwa madarakani inasababisha tatizo?

umewahi kuwazia ni kiashi gani cha fedha tulitumia kwenye tume ya Jaji Warioba na kila kitu kilichomo kikakataliwa na CCM huku Warioba ambaye pia ni Mwana CCM mwenzenu akikaa kimya kama vile hakuna kitu kilichotokea?
Ellen nitatofautiana na wewe kidogo, si kweli kwamba ccm inakataa kila kitu kinachotolewa na upinzani, kwa mfano;
-rushwa
-ufisadi
-mikataba/sheria mbovu.
haya yamekuwa yakipgiwa kelele na wpinzani kwa muda mrefu, na sasa yanafanyiwa kazi bila kujali tmechelew
 
We Mbowe hujui amekuwa mpiga dili wa kawaida? Anahangaika kurudi kwenye hali ya zamani wewe unamshangilia!!

Huyu na Manji mpiga dili hakuna tofauti. Sisi tunalia kwa sababu ya siasa, wengine wanalia kwa kuzibwa dili zao.

mwananyaso kama andiko langu halina lolote usingejibu ulivyojibu. Ufipa-Kinondoni sioni ajabu kwa mbunge kwenda Ikulu ama rais kwenda kwenye jimbo la mbunge wa chama kingine. Hapa Iringa Magufuli alikataliwa kwa kura, lakini bado atakuja kama kutimiza majukumu yake ya kibunge.

Halafu wengine mnaosema CHADEMA walifuata juice ikulu ni kama mnaidhalilisha Ikulu yetu kwamba huwa inahonga watu. Hata hivyo kwenye hilo kundi ni nani ambaye hawezi kujinunulia Juice yake mwenyewe? Ikulu ni nyumbani na ofisini kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania.

Nimeipenda picha ya Mbowe. Mtu yeyote mwenye akli timamu kuna wakati huwa anazama kwenye lindi la mawazo akiitafakari hatma yake!
 
Kusema kweli kwa mwendo huu wa JPM 2020 itapenyaa,,,kulijenga Taifa hili si kwa chama tuu hata wewe mfugaji unanafasi ya kuisaidia Taifa kujengeka imeonesha kwamba ndani ya Taifa hili kuna ushindani wa Mimi naweza Fulani hawezi kwa tabia hii hatufiki kidogo tuwe wabunifu wa maendeleo, sio kwamba Leo kaongea hivi Mimi naongea hivi ushindani wa maneno tuuache tujaribu kushindana na maendeleo ,,, kwa uadilifu tutafika

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwenye mjadala huu sizungumzii kama CCM "itashinda" tena mwaka 2020 bali najaribu kuona kama chama hcho kina uhalali wa kutuongoza tena kuanzia mwaka 2020 na kuendelea. Nimechagua kuzungumzia chama badala ya watu kwa kuwa inawezekana kabisa baadhi ya watu wasiwepo lakini naamini kwamba CCM itakuwepo mwaka 2020.

CCM ni zao la TANU na ASP na vyama hivyo ndivyo viliasisi Muungano wa Tanganyika na Zanzibar Muungano uliohitimishwa na Muungano wa vyama hivyo viwili kwa kuundwa kwa CCM mwaka 1977. Na kwa utashi wa vyama hivyo Katiba ya Tanzania ya Mwaka 1977 ikaandikwa na kuidhinishwa kutumika.

Wakati mapinduzi ya Zanzibar yanafanyika mwaka 1964, Tanganyika ilikuwa tayari imeshapata Uhuru wake toka kwa wakoloni mwaka 1961 ikifuatiwa na Zanzibar mwaka 1963. Baada ya Mapinduzi kulikuwa hakuna vyama vingine vya siasa vilivyoruhusiwa Zanzibari zaidi ya ASP, na mwaka 1965 TANU ilipiga marufuku vyama vingine vya siasa Tanganyika. Kwa mtiririko huko utaona kwamba kama kuna jambo lolote baya kwenye nchi hii kuanzia mwaka 1965 mpaka leo, ni lazima chanzo chake kiwe ni CCM.

Kama katiba ya Tanzania ni mbaya, basi wa kulaumiwa ni CCM. Kama mfumo wa kuendesha nchi umekaa shaghalabagala basi ni CCM ndiyo wamesababisha. Kwa kuwa hakuna mahali chama kingine cha siasa kimewahi kuongoza nchi hii zaidi ya CCM. Kwa ivo maovu na mabaya yote yanatokana na CCM.Lakini ni kwa nini kila wakati wa uchaguzi CCM huomba nafasi ya kurekebisha maovu yaliyosababishwa na chama hicho siku za nyuma.

Kama Mwalimu alilea uzembe hadi aliyemfuatia Ali Hassan Mwinyi aje na kauli mbiu ya "fagio la chuma" ni kwa nini tena Mkapa akaja na kaulimbiu ya "Uwazi na Ukweli' iliyopigwa kumbo na kauli mbiu ya Kikwete ya "Ari Mpya, Kasi Mpya na Nguvu mpya" ambayo imefutwa na kaulimbiu ya Magufuli ya "Hapa kazi tu"?

Kwa nini kila Rais anayetokana na CCM huonesha kwamba Rais aliyetangulia amemwachia nchi "chafu ama dhaifu" wakati wao wote wanatoka kwenye chama kimoja cha CCM? Mwinyi alikuwa waziri kwenye serikali ya Mwalimu, Mkapa alikuwa waziri kwenye serikali ya Mwinyi, Kikwete alikuwa waziri kwenye serikali ya Mkapa na Magufuli naye alikuwa waziri kwenye serikali ya Kikwete. Kwa nini wakiwa mawaziri hawaoneshi kwamba hali ni mbaya kiasi hicho mpaka wawe marais?

Nadhani CCM hakuna mtu anayeweza kutatua matatizo yaliyosababishwa na chama hicho kuwa madarakani. CCM inapata wapi uhalali wa kuongoza tena Tanzania kutokea mwaka 2020 na kuendelea?

CCM haifai kuongoza

ila ndio itaongoza kwa sababu ya ujinga wako na wapinzani

waza strategy za kuiondoa, sio mi article mireeeefu,kipi kipya hapo?
 
CCM haifai kuongoza

ila ndio itaongoza kwa sababu ya ujinga wako na wapinzani

waza strategy za kuiondoa, sio mi article mireeeefu,kipi kipya hapo?
Hii ya kuandika nayo inakukera nini kama haina madhara kwenu?
 
Nimechagua kuzungumzia chama badala ya watu kwa kuwa inawezekana kabisa baadhi ya watu wasiwepo lakini naamini kwamba CCM itakuwepo mwaka 2020
Huwezi kuongelea chama bila kuongelea watu. Chama kinaundwa kwa Sera zilizo kwenye maandishi. Watu ndiyo huyaweka hayo maandishi kuwa vitendo.

Ukiangalia maandishi yanaunda ccm utatamani isiondoke madarakani miaka 100. Lkn watu wake sasa. .....unatamani hata usiku huu wawe wamefutika ktk uso wa dunia.
 
Back
Top Bottom