CCM inafaa kutuongoza tena mwaka 2020?

nygax CCM inakubali kila kitu kinacholetwa na chama hicho na kukataa kila kitu kinacholetwa na vyama vingine, na hii haikuanza leo bali ni tangu mwaka 1992, na bahati mbaya wakati mwingine CCM hutumia nguvu za dola kupingana na mawazo ya vyama vingine.

Turudi kwenye mada: Kama huo uchafu wote unaodai unasafishwa na Magufuli ulisababishwa na CCM iwepo madarakani ni kwa nini CCM ipate uhalali wa kutawala wakati kila ikiwa madarakani inasababisha tatizo?

umewahi kuwazia ni kiashi gani cha fedha tulitumia kwenye tume ya Jaji Warioba na kila kitu kilichomo kikakataliwa na CCM huku Warioba ambaye pia ni Mwana CCM mwenzenu akikaa kimya kama vile hakuna kitu kilichotokea?
 
Kama haifai manake kuwe na chama Pinzani chenye
1. nguvu,
2. muundo stahiki wa uongozi,
3. wanachama hai yakinifu,
4. viongozi wenye sifa chanya,
5. viongozi safi wasio na tabia za upepo
6. Wamejiandaa kushika dola

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nadhani CCM hakuna mtu anayeweza kutatua matatizo yaliyosababishwa na chama hicho kuwa madarakani. CCM inapata wapi uhalali wa kuongoza tena Tanzania kutokea mwaka 2020 na kuendelea?
Tatizo mnawekeza sana propaganda chafu mitandaoni badala ya vijijini kwa wapiga kura.
Sawa ccm haistahili kutuongoza,tumpe nani fuko la hazina?
 
Tatizo mnawekeza sana propaganda chafu mitandaoni badala ya vijijini kwa wapiga kura.
Sawa ccm haistahili kutuongoza,tumpe nani fuko la hazina?
Hata vikao vya ndani mnaviogopa hao watu wa vijijini watapatikanaje? Kulikuwa na kikao cha CHADEMA walitumwa Askari kwenda kuwafurusha, siku za karibuni CCM wamefanya mkutano kijiji cha Kinyika huko Iringa vijijini hakuna walichofanywa.

Unadhani hivi sasa fuko la hazina liko salama?
 
Jamani! jamani!
jueni kuwa;-
Ccm siyo mfumo kama wengi mnavyodhani, ccm ni chama cha siasa kama vyama vingine nchini, ccm ni imani chini ya falsafa za kichama na sio mpangilio maalumu wa kisayansi, ndio maana hata wanachama wa ccm wanaweza kuhama na kujiunga na chama kingine, vivyo hivyo wa vyama vingine wanaweza kujiunga na ccm ( imani ).

Kinachotakiwa kuangaliwa ni mtu ( mgombea) je, anafaa? sio kumpa mbumbumbu kisa yuko chama fulani

Ngw'ana Kabula
 
Ccm ni kama ng'ombe aliepo machinjioni, tatizo mchinjaji yupo yupo tu. Na kisu butu hakina makali. Au niseme ccm ni sawa na timu ya Yanga imevaa jezi ya kijani lakini muamuzi kavaa jezi ya njano.




Ndukiiiii

Sent using Jamii Forums mobile app
 
wewe bhanaa!
1. kutokuwa na uaminifu
2. vigeugeu n.k
nayo yanavurugwa na dola?? hahaha

Ngw'ana Kabula
Inategemeana na unavyoyaangalia mambo ya siasa. Cha ajabu watanzania wengine wanadhani kukwama kwetu kama nchi kunasababishwa na vyama vya upinzani dhaifu lakini hawataki kabisa kujua kama CCM na yenyewe inataka vyama vya upinzani Imara.

Ugeugeu wa vyama vya siasa uko kwenye nini na wamekosaje uaminifu wakati kila jambo baya wahusika wakuu na wengi huwa ni CCM?
 
Back
Top Bottom