CCM ilejee kwenye misingi yake CHAMA CHA WAKULIMA NA WAFANYA KAZI

Mzururaji

JF-Expert Member
Apr 6, 2012
1,559
1,272
wakati tuna elekea maazimisho ya siku ya wafanya kazi duniani wafanyakai wa tanzania wamekuwa wanyonge bila mtetezi hasa kutokana na kunyimwa kwa stahiki zao ambazo zingine ipo kisheria haki hizo zimepokwa ama zimekandamizwa kwa makusudi na serikali ya awamu ya tano
haki kama ya kupanda madaraja na ongezo la mishahara annual increment zimekuwa ndoto za mchana kwa serikali kuwakumbuka wafanyakazi

Sasa turudi kwenye hoja ccm imeamua kuwatenga baadhi ya Wanachama wake ambao ni wanyakazi kwa kuto wasemea popote na kuamua kukaa kimya bila kusema lolote huku wakijifanya hawaoni mambo yanavyo enda upande wa wafanyakazi
Kuanzia mwenyekiti wa ccm Taifa, katibu wa CCM Taifa hadi mjumbe wa nyumba kumi wote wameamua kukaa kimya na kuona hakuna kinacho endelea kwa wanyanyakazi

tunaomba tuwakumbushe viongozi wa CCM kuwa mnajukumu la kulisemea hili msione wafanyakazi wamekaa kimya mkazani mnaeleweka hebe jaribuni kulisemea hili ipo siku mtawahitaji hawa wafanyakazi ambao mnaona hakuna haja ya kuwa na urafiki nao hasa kipindi hiki wanacho pitia.

nawatakia pasaka njema
 
Back
Top Bottom