Elections 2010 CCM at it AGAIN. SMS zishaanza upyaa!!

Yanamwisho wake hayo nao ni October 31, upuuzi wote wa CCM utaishia hapo
 
Kwenye mdahalo wa juzi DR. Slaa alifafanua kwa ufasaha kwanini kunakuwa na conflict of interest wakati wafanyabiashara wanachanganya na siasa [ na atharia zaka kwa jamii]. Kikwete hajui maana ya conflict of interest na athari zake, angekuwa anajua angechukua hatua za kumuondoa mkurugenzi wa Ocean Road Hospital anaendesha hospital inayoshindana na ocean Road huko mwenge kwa kutumia wafanya kazi wale wale wa Ocean Road!! Huduma za hospitali ya ocean Road wanakotakiwa kupata huduma zenye tija walala hoi zinazorota wakati hospitali ya Ngoma kule mwenge inazidi kushamili. Serikali hii haina budi kuamka kutoka usingizi huu wa pono!!
 
wakuu jana tarehe 24 oktoba, 2010, mnamo saa 1:09 jioni nilipata ujumbe wa maandishi (text message) kwenye kikasha cha kupokelea cha simu yangu; uliosema:
chadema wametekeleza ahadi ya kumwaga damu. juzi wamemuua ndugu wa mgombea wa ccm maswa. mjumbe wa kampeni ya slaa amekamatwa. tuwakatae chadema wamwagaji damu.

my take;

  • je, ni kweli chadema walitoa ahadi ya mauaji kwenye ilani yao ya uchaguzi.
  • ni nani hao waliotuma ujumbe huo na kwa nini hawajitambulishi?
  • je, kuna mkuu yeyote aliyetumiwa ujumbe huu au kusikia popote au ndio mimi tu peke yangu ndiye niliyetumiwa?

Nami nilitumiwa, lakini kwa kuwa aliyenitumia namfahamu na najua asingeweza kufanya hivyo, nilimjibu hivi; "Tafadhali sana, usiyaamini ya kusemwa, bali ya kuyaona! Na kihistoria chama cha upinzani haijawahi kuanzisha vurugu duniani, bali pale chama tawala inapozidiwa nguvu ndipo vurugu huanzishwa! Mfano; Kenya & Zimbabwe. Na jana (23/10/2010) Dr. Slaa akiwa pale Moven Peak, Dar es Salaam aliwaagiza wana CHADEMA kuwa "ukitukanwa, angalia, puuzia na uondoke, na ukipigwa kofi mgeuzie na la pili, maana sipendi kwenda ikulu huku watu wakimwaga damu na kubaki vilema kwa ajili yangu". Hivyo, tafadhali sana, Tafakari, Amua na uchukue hatua". Hivyo tena, tujaribu kuwa makini sana, maana sasa CCM wanafanya maasi, then wanasambaza ujumbe wa kinyume chake kutuhumu CHADEMA...! Lakini kwa vyovyote ukweli unabaki kuwa "SIKU YA KUFA KW NYANI, MITI YOTE HUTELEZA...!"
 
Hizo ni siasa nyepesi kabisa, hata mtoto wa chekechea huwezi kumwambia hiyo akakubali. sisiem mwaka huu wenu..........pls tuachieni nchi yetu kwa amani.
 
Hata maandiko matakatifu yanasema mambo yoote yatapita lakini NENO LITASIMAMA. Hata upuuzi huu UTAPITA NA utakwisha tu 31.10.10
 
Ujumbe huo ni kweli kabisa unasambazwa walau toka jana. Kutokana na mfumo mbovu TCRA hujiona kama ni sehemu ya chama tawala badala ya kuwa chombo huru. Hamtasikia kinachoendelea as long as jumbe zinazotolewa however chonganishi hazikilengi Chama tawala.TCRA watakaa kimya.
 
Kwa Kawaida mgonjwa mahututi akishaomba Maji tu, then akakwambia anasikia HAJA kubwa basi anza kuandaa msiba. CCM ni mgonjwa Mahututi na hizi message ndo Haja kubwa - sasa sisi wenye akili hatudanganyiki na hizi propaganda za kitoto.

Tumeshawazoea, Msiba wa Wangwe (RIP) walitaka kuugeuza tufuru yao sasa waulize yaliwakuta yapi? na yule mchungaji feki wa kondoo za bwana anakumbuka ile zahma iliyomfika akiwa jukwaani.
 
Hiyo namba sijui ya mtandao gani kwa sababu jumla ya tarakimu zake ni pungufu. Mchezo huu unapikwa na mafisadi wakiongoizwa na wale papa.
 
matumizi mabaya ya technologia dhidi ya TAIFA.
bahati yao mbaya kwani mtaani kuna IT specialists wakali kuliko hao wanajipendekeza ikulu ndo maana hawafurukuti wakijaribu spinning.


Mkuu niliwahi kusema humu mwaka jana kuwa CCM wamechakachua wasomi wetu! RS & crew is among many!!!! Hawa watu wamegundua ili ufanye biashara smoothly you need to associates yourself with CCM. Its pay back time, they have to do something for them to justify their existence!!!
 
kama kawaida asiyekubali kushindwa si mshindani atatafuta hata ya kutunga kuhalalisha na kuficha madhaifu yake
Kuna ujumbe umenifikia sasa hivi kutoka namba 078049550 kupitia mtandao wa zain usemao...

Kwenye bold hapo ni kwamba shibuda ndiye anayeshikiliwa isivyo halali mpaka sasa, hivyo wanavyosema kuwa mjumbe wa kampeni wa slaa amekamatwa huo ni uwongo na kuchafuana kama walivyo wachafu.

Wakuu nimeweka hii namba hapo kwani utata wake ni kwamba ina tarakimu tano badala ya sita hivyo naamini kuna NIAmbaya makusudi imefanywa na hata hao wenye mtandao (ZAIN) kupitisha huu ujumbe.
Pili ni kwamba mimi ninaomba msaada wa kisheria niweze kushtaki maana ujumbe huu maana sijui mtumaji ana lengo gani na mimi.

nimejaribu kumpigia mwenye namba simpati. kama kuna mtaalam anaweza kuipata chanzo ya hii namba tumwanike hapa jukwaani
 
Kama nilivyoahidi jana.......baada ya kupata fununu kutoka kwa mtaalamu wetu wa Telecommunication Engineering ambaye aliweza kupata namba kamili inayofanana na moja ya namba zilizotumika na akatupa 'details' za Z.Mrisho.

Tangu jana tumejaribu kufuatilia kwa mtu fulani ambaye alikuwa akiishi mabibo na sasa amehamia sinza, huyu namba yake ya Zain inafanana tarakimu nne na moja ya namba zilizotumwa. Japo ni kada wa CCM lakini hatukupata uhusiano wake na msg hizo.

Katika mitego mingi tuliyoiweka mmoja ulikutana na 'dead end'. Tukawa 'interested' kuufuatilia japo ulikuwa na hatari zake. Jamani mambo tuliyokutana nayo yanadhihirisha kuwa CCM maji shingoni. Kumbe huu ni mpango wenye kibali kabisa kutoka kwa JK na makampuni matatu ya simu yanahusika, pamoja na kuwa TCRA wanalifahamu pia. Hizi si namba za watu binafsi bali ni namba za 'profile' za makampuni matatu makubwa ya simu na wao ndio wame'compromise' namba za simu za wateja na wala hazikutumwa 'randomly' kama tulivyodhani.

Huu ni moja ya mikakati mikubwa ya CCM inayofanya ili kubadilisha upepo wa kura dakika za mwisho.

CCM wamegundua yafuatayo kwa kusaidiwa na majasusi wa nje na ndani:

1. CUF inawagharimu kwa kuwa kura za CCM nyingi zitaenda CUF hasa maeneo ya Pwani, kusini, Zanzibar na mkoa wa Tabora.

2. Kura za CHADEMA haziyumbi, yaani ziko 'stable' na hazibadiliki kwa upepo wakati kura za CCM haziko 'stable'.

3. CCM na CUF kwa sasa wanagawana asilimia 28% na 22% respectively wakati CHADEMA iko 'stable' kwa asilimia 48% huku asilimia inayobaki wakigawana wengine.

Hii imekuwa hali ya hatari kwa CCM hivyo wameamua siku hizi chache za mwisho na hasa tatu za mwisho...haswa haswa masaa 24 ya mwisho waje na mikakati mizito ya kubadili upepo( Nimeandika mara nyingi juu ya hili)

1. tumeshaona...kupakazia CHADEMA kuwa ni wamwagaji damu

2. Kutumia vipindi vya TV zenye 'coverage' kubwa kueneza propaganda za CCM na kuwanyima CHADEMA fursa ya kuonekana kwenye luninga labda kwa muda mfupi sana.

3. Kufikisha ujumbe kwa nguvu kuwa CHADEMA wamejiandaa kuingia msituni

4. Kutishia wanataaluma wote wasiounga mkono CCM waziwazi kuwa 'watatoswa' JK akichukua nchi...na kuwatishia kuwa CCM ni lazima itashinda..hivyo wajiandae kutoswa.

5. Kuweka ndani wagombea tishio wa CHADEMA hata wakiwa ishirini ndani mpaka uchaguzi upite.

6. Kutoa uzushi mkubwa usikike nchi nzima kuwa Dr. Slaa amejitoa kwenye kinyang'anyiro zikiwa zimebaki saa chache kabla ya kupiga kura.

7. Kuiba Kura.KUCHAKACHUA MATOKEO.

Haya si mageni kunenwa hapa JF na yameshaanza kuonekana.

CCM mtatapatapa sana lakini kufa maji ndo mshakufa hivyo.

CHADEMA IMECHUKUA NCHI.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom