Kwani Kinana kwao ni wapi ?
Wakuu,
Ni miezi yapata mitatu sasa imepita tokea Mkurugenzi wa Uchaguzi atangaze kwamba Uchaguzi wa Sombeti ungefanyika mwezi September.
Kwa ufupi ni kwamba CCM baada ya kupata taarifa ya uchaguzi wa Sombetini walianza kuhaha kutafuta mgombea atakayesimama kwa tiketi ya chama chao. Mwezi moja uliopita walikwenda kwa Mwalimu moja wa shule ya Secondary Sombetini baada ya kuona ana ushawishi, lakini yule mwalimu akawaambia ni kweli anafundisha Sombetini lakini anaishi nje ya Sombetini. Baada ya kugonga mwamba kwa mwalimu ccm walikimbilia kwa Mchungaji wa kanisa wakampigia magoti agombee kwa tiketi ya ccm, Mchungaji akawajibu kuwa ingelikuwa chama kingine sawa, lakini kwa hii nitakuwa nimewasaliti wanasombetini ambao miaka na miaka wamekuwa wakilalamikia utawala mbovu wa serikali ya ccm. Akawaambia CCM siyo chama cha mabadiliko, bali yeye ni mwanabadiliko wanisamehe sana.
CCM walichanganyikiwa zaidi baada ya kupata tetesi kuwa CHADEMA wanamtaja taja Kamanda Ally Bananga kuwa ndiye atakayegombea kata ya Sombetini. Baada ya kupata hizo tetesi na hasa walipogundua kuwa watu wamekataa kugombea kwa tiketi ya CCM, ilibidi wachomekee kwa Tume ya Uchaguzi kuweka kapuni tarehe ya uchaguzi kata ya Sombetini.
Onyo:
Tume ya Uchaguzi kuweni makini msiendeshwe kwa hisia za kisiasa. Taarifa ya kuwa kata ya Sombetini ipo wazi Tume walipewa na Ofisi ya Mkurugenzi mwaka umepita.
Kwani Kinana kwao ni wapi ?
Kwani Kinana kwao ni wapi ?
Kwani Kinana kwao ni wapi ?