Leo majira ya saa kumi na nusu kumetokea vurugu hapa CCM mkoani Arusha, baada ya vijana kumtoa Mary Shitanda kwenye mkutano wekiimba hatukutaki ondoka zako.
Baada ya kuona watu wanazidi kumzonga alichukuliwa na kuingizwa ndani na askari kanzu waliofika hapo na kufunga milango. Kuna wandishi wa startv na Ch 10 walibahatika kuingia ndani.
Sijajua hasa chanzo ni nn?..nimeona twitter JMakamba anapuuza taarifa hizi, kudundwa si lazima fimbo au mawe, maneno makali ni kichapo tosha. vurugu zimetokea, labda kama atapuuza na tbc1
Siasa ni biashara na ndio maana wenye fedha sasa wanaonekana maadui kwa wale wanaotaka kwenda huko! Tutayasikia mengi hadi 2014 kila mtu atakapojidai kuwa mtii kwa chama ili maoni yasiwaangushe.