Car seat

Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
92,231
113,589
Wadau, ningependa kujua sheria za barabarani Tanzania zinasemaje kuhusu kuendesha gari na mtoto akiwa ndani? Je, ni lazima uwe na car seat? Na kama ni lazima ni watoto hadi wa umri gani wanaotakiwa kuwekwa kwenye car seat? Na kama wamevuka huo umri sheria inasema wakae kwenye kiti cha nyuma au?

Wenye kujua tafadhali nijuzeni. Natanguliza shukrani.
 
ofu topik:mie nilijuaga NN ni msela msela hivi,hana mtoto wala hawazii kuwa naye....:twitch:
 
ofu topik:mie nilijuaga NN ni msela msela hivi,hana mtoto wala hawazii kuwa naye....:twitch:

Hahahaha, stank (thank) you Rosie...

See, never judge a book by it's cover and never judge a person by their user handle and some of the clowning they do here. Behind NN there is a very upstanding, very well put together gentleman. Behind NN, there is an outstanding son whom his parents are very proud of. Behind NN there is a very loving father who is a hero to her million dollar princess. Don't you ever bad mouth me in front of my daughter...she'll cut you down to size and put you in your place. She's very protective of her daddy. She's a daddy's girl.
 
What the hell? Ina maana hakuna anayejua? Well, I guess I'll have to check with the traffic police.
 
Dont you ever do it, they will ask for kitu kidogo, na najua hutakuwa tayari kufanya hivyo.

Hapana babu, moja ya kanuni zangu zisizovunjika ni kutoa kitu kidogo. Ila kuhusu hiyo sheria vipi, ipo angalau hata vitabuni au haipo kabisa?
 
NN mimi nafikiri sheria haiko wazi hapa Tanzania au hatuijui ila kwa usalama wa watoto wako na kwa ufahamu tulionao ni kuwa mtoto ni vizuri akae kwenye car seat iliyowekwa nyuma. watoto wachanga mpaka 8months wanatakiwa watumie rear facing car seat na wakubwa 9months na kuendelea, sina uhakika mapaka umri gani. hivyo ndivyo nilivyofanya mimi kwa usalama.
 
Asante dada. Nyuma ni salama zaidi kwa mtoto yoyote chini ya miaka kumi na miwili.
 
Sheria zetu za barabarani hazieleweki needs to be reviewed and amended where applicable. Mueke tu mwanao kwenye car seat proper for her age ili uendeshe gari kwa amani.

Mara kama mbili hivi hawa wanaoclaim ni matajiri wa mji huu and they live flashy lives, niliona baba kashika usukani huku amempakata mwanae na gari linatembea kabisa. Just like how Britney was nabbed i think last year or the other year akiendesha gari huku kampakata mwanae its very dangerous lakini trafiki wala hakumuona huyo baba au alimuona akamuacha apite hata sikuelewa. I wished i was a traffic police ningempeleka kituoni straight away. :mad::mad::mad:
 
Wadau, ningependa kujua sheria za barabarani Tanzania zinasemaje kuhusu kuendesha gari na mtoto akiwa ndani? Je, ni lazima uwe na car seat? Na kama ni lazima ni watoto hadi wa umri gani wanaotakiwa kuwekwa kwenye car seat? Na kama wamevuka huo umri sheria inasema wakae kwenye kiti cha nyuma au?

Wenye kujua tafadhali nijuzeni. Natanguliza shukrani.

Hakuna sheria yoyote inayotumika Tz ambayo iko valid sembuse inayohusu car seat? Tz kwenye sheria zote ni mfuko wako na ukikataa yatakupata kama yaliyonipata mie kwani nilipelekwa pale Osterbay Polisi kama mzururaji na kesho yake nikapelekwa mahakamani nikasomewa shitaka la kukutwa na mmea/Bangi gram 500 zikiwa kwenye bahasha, hapo nilinyanyua mikono nikakata pochi na kesi iliisha siku hiyohiyo mahakamani
 
Yaani hili liinji bana aaah lina kero nyingi mno
 
Brasil nawewe sasa unaogopa traffic fines au safety ya mtoto wako?.... unavyoonesha unajua sana HSE Rules ila msg yako imefika....
 
kwa usalama wa mtoto wako utakapofika bongo tumia tu hizo sheria zinazotumika huko uliko hivyo hivyo bila ya kujali kama traffic police anajua maana yake au la.

hawa makwegaz wapo wapo tu...........maana ya usalama barabarani hawaijui kabisa
 
Wadau, ningependa kujua sheria za barabarani Tanzania zinasemaje kuhusu kuendesha gari na mtoto akiwa ndani? Je, ni lazima uwe na car seat? Na kama ni lazima ni watoto hadi wa umri gani wanaotakiwa kuwekwa kwenye car seat? Na kama wamevuka huo umri sheria inasema wakae kwenye kiti cha nyuma au?

Wenye kujua tafadhali nijuzeni. Natanguliza shukrani.

kwa nchi yetu sijui kama hii sheria ipo......car seat was introduced kwa sababu ni vigumu kumfunga mtoto mdogo mkanda wa kawaida kwenye gari coz mkanda wa kawaida uko designed kwa watu wazima.
sasa kwa nchi yetu ambayo kuvaa mkanda ni ubrazameni na hata traffic police anaangalia dereva tu unategemea watajua kitu kinaitwa child car seat?mara nyingi tu nishashuhudia watu wanaendesha huku vitoto vinatoa vichwa nje ya dirisha au wengine wanawaruhusu hata kuchungulia thru sun roof......nunua na weka kwa usalama wa mwanao kama ambavyo naona watu wachache wanajali wanazo hizo child car seat.
 
nishashuhudia watu wanaendesha huku vitoto vinatoa vichwa nje ya dirisha au wengine wanawaruhusu hata kuchungulia thru sun roof......nunua na weka kwa usalama wa mwanao kama ambavyo naona watu wachache wanajali wanazo hizo child car seat.

Duuh sasa hiyo ni child endangerment....kuna haja ya kuanza uanaharakati wa kutetea haki na maslahi ya watoto. Ngoja nijipange vizuri.
 
Duuh sasa hiyo ni child endangerment....kuna haja ya kuanza uanaharakati wa kutetea haki na maslahi ya watoto. Ngoja nijipange vizuri.

OK....... ila usituletee haki za huko majuu tukashindwa hata kuwaadabisha watoto wetu wakawa kama akina SHANIQUA.......
 
Back
Top Bottom