Cannavaro astaafu rasmi timu ya Taifa, Kujikita na Yanga

Zamani nilikuwa nasema makocha wazawa wanaonewa lakini kwasasa napingana na fikra zangu kuwa sio sahihi ni kwamba wana uwezo mdogo sana, kama huyu Mkwasa sijui ni kule kuzoea kufundisha timu ya wanawake au la, naombea afukuzwe haraka na hata Yanga wasimfikirie tena abaki kufundisha timu za kukwepa kushuka daraja kwakuwa ameonyesha kuwa sio kocha anayejitambua hata kidogo
 
AONDOKE NI WAKATI SAHIHI ANASEMAJE AMEPIGANIA TAIFA WAKATI GOLI SABA ZILIMPITA PALE PALE ANAZIANGALIA,TUNATAKA VIJANA SASA
SAMATA si alikuwepo uwanjani alifunga mangapi kupunguza tofauti ya magoli kama si kurukaruka tu? Huo uchezaji bora wenyewe kabahatisha tu aliyekuwa anastahili ni Kidiaba
 
Tatizo la viongozi wa soka katika club zetu hapa nchini na TFF wamejaa uswahili mwingi, wazee wa zengwe, embu fikiria tuu msemaji wa timu anatakiwa kuwa mtu mwenye taaluma na weledi wa hali ya juu ila hapa bongo ni mtu anayeweza kuropoka na kuponda wapinzani au kutoa majibu ya mkato kwenye vyombo vya habari...nonsense

Suala la kumvua unahodha cannavaro TFF wampe onyo kocha, na kumuomba samahani cannavaro, endapo wachezaji wakiamua kumsusia huyo jamaa yao na kocha timu haitakuwa stable
Mkwasa hajamfanyia fair Nadir kabisa, alipaswa aastafu kwa heshima.. Mkwasa kachemka sana sana...
 
Binafsi sikuona sababu ya msingi Samata kupewa unahodha. Tatizo siasa kila mahali nchi hii
 
H
Nakumbuka enzi za Mbrazil Maxmo kuna kapten fulani hivi alistaafu team ya taifa na akaagwa kwa mechi maalumu, kama sijakosea ni Salumu Swed au Meky kocha wa Mtibwa, sasa why na kwa Cannavaro haikufanyika hivi?!
By the way, anaondoka stars akiwa na record tamu sana ambayo hakuna mchezaji mwingine aliyewahi kuipata duniani im sure.
1.Capten wa klabu yake (Yanga)
2.Capten wa team ya taifa ya ZNZ
3.Capten wa team ya taifa Tanzania.
Hakuna mchezaji aliyewahi kuwa capten wa team tatu kwa wakati mmoja!!
Go Cannavaro go ulipo tupo!!!
Huyu amesusa kwa mujibu wa Maelezo yake, hastafu kwa sababu ya umri, Bali kwa kunyang'anywa unahodha kwa kutaarifiwa kwa njia ya simu, na lawama za mashabiki. Ila simuungi mkono kwa kustaafu eti kwa lawama za mashabiki, popote pale Duniani mashabiki hawaachi kutoa lawama timu inapofanya vibaya, na sidhani Kama alikua akilaumiwa yeye Kama nahodha Bali lawama ilikua kwa timu mzima pamoja bench la ufundi. Kwa sababu hizo alizotoa sidhani Kama anastahili kupewa heshima ya kuagwa, maana Ana kinyongo, anaowatuhumu wana kinyongo. Mnaweza kuandaa hafla ya kumuaga, hasitokee, kwaheri Nadiri, huko ulikobaki hata ufanye vizuri, sikusifii hadharani nami mna nyongo atii.
 
Last edited:
Nathamini mchango wa Haroub lakini kwa hili siungani nawe hata kidogo! Kwanini? Kuwa kapteni maana yake unatakiwa kuwa na vitu vya ziada ambavyo wenzako watakuwa wanaKUSOMA!!! nimejaribu kumwangalia Haroub kama mfano lakini nimekosa kuona vitu vya ziada kutoka kwake.Utulivu bado sana,uwezo wake kuupoza mpira ili timu ijipange ndipo atoe pasi yenye macho ni mdogo.nakubali yupo agressive katika kuharibu mpango ya adui,ni mzuri sana kwenye kuosha.Amekuwepo kwenye timu yetu ya Taifa muda mrefu hata matokeo ya 7 - 0 yamemkuta yupo.Nashauri yeye na genge lote la Timu yetu ya Taifa waondolewe kwanza pamoja na huyo Mkwasa...!tuanze upya.
 
Kama kwa mtazamo wake anaona ni muafaka kupumzika bila shaka yuko sahihi ukizingatia umri nao unamtupa mkono na ni muendelezo wa utamaduni mzuri kwa wanamichezo kuachia ngazi pale ambapo umetumikia timu kwa muda bila mafanikio. Sababu zingine alizotoa zilizompelekea kufikia huo uamuzi zinatia ukakasi kidogo. Kuvuliwa unahodha si jambo jipya katika dunia ya soka na hakuna nahodha anayedumu katika unahodha milele. Kwa uzoefu wa uendeshaji wa masuala ya soka nchini pasipo kufuata mkondo wa weledi namna alivyovuliwa unahodha haishangazi na kama mchezaji mkongwe hakupaswa kulalamika kihivyo. Hata uvumilivu wa kuisubiri barua umemshinda hata baada ya kuambiwa kwa njia ya simu na mkwasa. Pamoja na kuchezea yanga miaka yote hiyo bado hajui kuwa timu ikifungwa mabeki ni wahanga wa tuhuma za kusababisha timu kufungwa hata kama sivyo. Kama una dhamira hai ya utumishi kwa taifa lako maneno maneno hayawezi kuua dhamira yako wala utaratibu usiozingatia weledi hauwezi kukukatisha tamaa. Je canavaro amestaafu kuchezea timu ya taifa kwa kuvuliwa unahodha bila kuandikiwa barua, maneno maneno au kwa heshima ya damu changa kuleta changamoto mpya? bado hajaeleza kwa ufasaha na pasipo ufasaha huo bila shaka atakuwa amejistaafisha mwenyewe pasipo heshima.
 
Tunakushukuru kwa kuwa lengo lako liikuwa zuri kutupigania waTZ, hata hivyo umetugharimu mno mno.Wewe na genge zima inabidi muondoke ili tusuke kikosi kazi kingine.Tunamsubiri mkwasa naye apate ujasiri kama wewe atangaze kuachia ngazi ili kama Taifa tujipange..! Mambo ya 7 - 0 ni AIBU...!!!unaanzaje kusema mimi timu yangu ni ile iliyofungwa 7 - 0...?
 
Kisa eti Samata kachukua uchezaji bora wa africa kwa wachezaji wa.ndani basi anapewa unaodha hii sio sahihi ata mi nilishamgaa mkwasa kusema eti ili kumpa heshima tumeona bora apewe unahodha…!! Mess kachukua uchezaji bora mara 5 ila ukapteni katika klabu yale kaupata lini? Xavi alichukua unaodha kisa alichukua uchezaj bora? Sio kweli tuangalie soka lawenzetu linaendaje, tulinde vipaji vyetu, heshima za pekee kwakoNadir umelipigania Taifa, sifa zako zilivuma ila sisi ndio watanzania tunaofanya vitu kwa kukurupuka… huko Algelia ile mechi tunafungwa 7 Samata alionekana mara 4 tu uwanjani ndani ya dakika 90 afadhali ata ya Ulimwengu nikimuona lakini kama lawama unatupiwa wewe ilihali beki pekeehawezi fanya kitu ikiwa kiungo na washambuliaji hawakai na.mipira wanategemea nini?
...acha kulia, wachezaji mastaa wote kwenye timu hua wanapewa unahodha,haijalishi kapewa lini huo unahodha,muhimu apewe yeye ili kumfanya ajitume zaidi kwa ajili ya timu.
Hata kufahamika,ni rahisi zaidi marefa wa nje kumsikiliza Samatta kwenye mechi zaidi ya huyo canavaro anaefahamika jangwani.
 
Na Saleh Ally
ALIYEKUWA nahodha wa timu ya soka ya taifa, Nadir Ali Haroub ‘Cannavaro’ ameamua kutangaza kustaafu kuichezea timu hiyo baada ya kuitumikia kwa miaka 10.

Cannavaro anaendelea kubaki kuwa nahodha wa mabingwa wa Tanzania Bara, Yanga pia timu ya taifa ya Zanzibar maarufu kama Zanzibar Heroes.

Cannavaro kama alivyo, hajawa mnafiki kwa kusema sababu ambazo zinaonekana kumkwaza hadi kufikia uamuzi huo wa kutangaza kuitumikia timu ya taifa.

Sababu kuu ambazo alizizungumzia wakati akisema hilo, moja ni lawama lukuki alizorushiwa kwamba amekwisha na alichangia Taifa Stars kufungwa mabao 7-0 na Algeria ikiwa ugenini.



Lakini yeye akaeleza alivyopambana pamoja na wenzake, tena kwa nguvu kuu huku wakiwa pungufu baada ya Mudathir Yahaya kulambwa kadi mbili za njano kisha nyekundu. Ninaamini angekuwa makini, kadi zile zingeepukika.

Sababu ya pili ya Cannavaro ilikuwa ni uamuzi wa kuvuliwa unahodha, akapewa Mbwana Ally Samatta mara tu baada ya kutwaa tuzo ya mwanasoka bora Afrika kwa wanasoka wanaocheza ndani ya Afrika.

Cannavaro ameweka wazi, kwamba hapingi yeye kuvuliwa unahodha, wala halazimishwi kubakiwa nao, lakini utaratibu uliotumika kuuchukua kwake kwenda kwa Samatta unaashiria dharau kubwa tena ya kuumiza moyo.

Kwa mara ya kwanza, Cannavaro anasema alijua sasa si nahodha wa Taifa Stars baada ya kuona kwenye runinga, Kocha wa Taifa Stars, Charles Boniface Mkwasa akiwa anatangaza kuhusiana na hilo. Baada ya hapo, kesho yake, kocha huyo akampigia simu kumtaarifu kuhusiana na hilo.

Sasa jaribu kupata picha ya kiungwana, ambayo kamwe haitakiwi kuwa na chembe ya ushabiki. Kwamba wewe ndiye Cannavaro, utasikiaje, utalichukuliaje suala hilo na uamuzi wako utakuwa upi?


Kwanza niwe wazi, niseme naungana na maumivu ya Cannavaro kwamba alichofanyiwa ndiyo mambo ya ‘Kiswahili’ ambayo tumekuwa tukiyapinga na unaanza kupata hisia, kweli kungekuwa na kocha mgeni angeweza kufanya mambo kisiasa na kukurupuka hivyo, ninaamini hapana.

Bado narejea palepale kwamba, kweli kwa miaka yote ya Taifa Stars kwa Cannavaro, alipaswa kuvuliwa unahodha kwenye runinga yeye akiwa hajui lolote?

Au Mkwasa alishindwa kufuata taratibu ambazo ni rahisi na laini kabisa, kwa kumtafuta Cannavaro, wazungumze naye, akimalizana naye, azungumze na Samatta baada ya hapo lije suala la kutangaza na ikiwezekana akiwa na wote wawili mbele ya waandishi wa habari.

Sijui, inawezekana kwa kuwa Samatta alikuwa gumzo, kila mmoja akitoa zawadi na pongezi. Mkwasa aliona kumpa ‘unahodha’ ni zawadi. Kama aliona anastahili, basi angefanya hivyo miezi miwili nyuma au baada ya kuipa TP Mazembe ubingwa wa Afrika na ingewezekana kabisa.


Pia angeweza kusubiri hadi kikosi cha Taifa Stars atakapokitangaza, kikiwa kambini, angetangaza hilo na si kukurupuka sasa kwa kufuata tu kwa kuwa upepo unakwenda upande huu.

Uamuzi wa Mkwasa kufanya hivyo akiwa nyumbani kwake, aliona ni rahisi kwa kuwa alimchukulia Cannavaro kama mshikaji, kijana wake, au alimchukulia ‘poa’ tu? Kwangu nasema Mkwasa amevurunda katika hili na anapaswa kujifunza namna ya kuepusha mambo mengine yasiyokuwa na msingi.

Cannavaro alikuwa anajua asingekuwa nahodha milele. Ndiyo maana alihoji kama kweli wengine waliopita kama Shadrack Nsajigwa na wengine, waliondolewa kwa dharau kama yeye? Mkwasa alikuwa mchezaji, kocha wa klabu, kote amepita na anajua machungu ya mchezaji kudharauliwa, sasa vipi kuyajua hayo na kufanya mambo vululuvululu?

Nimetolea mfano kocha wa kigeni, kwamba asingeweza kufanya hivyo, ninaamini hivyo. Mimi ni kati ya wale waliokuwa wakiamini na makocha wazalendo wanapaswa kuthaminiwa na ikiwezekana kulipwa mishahara mizuri na nyumba bora kama ilivyokuwa kwa makocha wageni.

Ninapoona makocha ambao tunawalilia wanaanza kuingia kwenye siasa, kufanya mambo kwa kulipua naanza kuingia woga, najisikia vibaya na kuanza kuona kama tunaowalilia nao si watu makini kwa kuwa wanaweza kutuangusha katika vitu vidogo kabisa ambavyo vilikuwa havihitaji akili nyingi hata kidogo.

Ushauri wangu katika hili; moja, Mkwasa amuite Cannavaro, azungumze naye na kumuomba radhi, hakika amemkosea na hakuna haja ya kupindisha maneno. Kweli Cannavaro kaipigania Stars miaka mingi na anastahili kupewa heshima yake.

Pili; namshauri Cannavaro, kuendelea kuitumikia Stars kila atakapoitwa. Kwangu namuona wala hajazeeka na hapaswi kushinikizwa na mashabiki, wengi wao hawajui mpira na mambo wanayafanya kishabiki.

Kocha ndiye ataamua hilo pia ninaamini ana uwezo wa kuitumikia Stars kwa mwaka mmoja, miwili au mitatu ijayo kulingana na anavyojiweka mwenyewe.

Taifa Stars si ya Mkwasa, hata yeye ana haki kama za Cannavaro, hivyo usiwatupe Watanzania wote wanaokuamini na usiachane nao vibaya kwa hili. Dunia ina mitihani, huja, hupita na kwenda. Tafakari.

SOURCE: CHAMPIONI
 
Tunakushukuru kwa kuwa lengo lako liikuwa zuri kutupigania waTZ, hata hivyo umetugharimu mno mno.Wewe na genge zima inabidi muondoke ili tusuke kikosi kazi kingine.Tunamsubiri mkwasa naye apate ujasiri kama wewe atangaze kuachia ngazi ili kama Taifa tujipange..! Mambo ya 7 - 0 ni AIBU...!!!unaanzaje kusema mimi timu yangu ni ile iliyofungwa 7 - 0...?
Mbona Thiago Silver hajavuliwa uCaptain pamoja na Brazil kupigwa 7 - 1 kombe la dunia?
 
Samatha ataweza wacontrol akina yondan, canavaro? Kuwa bora c lazima kuwa captain mkwasa kachemka
sidhani kama mkwasa alifanya critical thinking kwenye maamuzi yake! alichemka sana! nmeanza kuwa na maswali mengi kuhusu uwezo wake wa kumanage! glafla hivi!!!
 
Yaya Toure ameichezea barcelona kwa miaka 3 baadae akajiunga man city alipata nafas ya kuonyesha uwezo wake na kufanya apate namba ya kudumu kwenye team ya Taifa ameichezea kwa mafanikio kuanzia 2011hadi 2014 kachukua tuzo lakin 2014 ndo wakaona umuhimu wa kumpa ucaptain baada ya Didie drogba kustaafu kuichezea team ya Taifa ilipaswa Cannavaro mwenyewe aamue na cyo kumpokonya ucaptain bila hata ya mwenyewe kujua nilikuwepo Zanzibar Mapinduzi cup half time mechi ya nusu fainal Yanga na ura walipotangaza samata ndo captain mpya wa stars muda huo huo nikampigia Nadir kumtania kavuliwa ucaptain kumbe mim ndo mtu wa kwanza kuumpa hizo taarifa baadae naongea na mkwasa ananiambia Cannavaro hapatikani week yote hii hili ndo soka letu
 
bravo canavaro, umetumikia taifa kwa moyo mmoja, ila wapenda sifa za kijinga ndo wameona wakimpa C hyo ndo wamemthamini sana kumbe wanaua soka kwa unafiki wao, bhasi na ulimwengu wampe unaodha msaidizi maana yeye pia amechukua Africa champions league kuliko uyo boko ambae ni bure tu katika national team, tutegemeee week zingine kwenye mashindano
Kwan ye canavaro kafanya nn. Ameisaidia nn taifa stars. Apewe heshima kwa lipi alilolifanyia taifa. Tuache ubwege kama ni jiwe tuliite jiwe. Canavaro aishie zake apite vile aachie vijana. Huo ni upuuzi tu. Yaani afungishe goli saba halafu adai heshima. Stupid.
 
Back
Top Bottom