Bwana harusi afariki dunia akifungua zawadi iliyotegwa bomu

Donnie Charlie

JF-Expert Member
Sep 16, 2009
15,159
16,238
Bwana harusi Adlyyne Wangusi amefariki dunia baada ya kufungua zawadi ambayo ilikuwa imetegwa bomu na mume mwenza.

Bomu hilo lilidaiwa kutegwa na mpenzi wa zamani wa bibi harusi, ambaye alikuwa na hasira kutokana na mwanamke huyo kuolewa na mwanamume mwingine.


Taarifa ya Jeshi la Polisi nchini India imeeleza kwamba, bomu hilo lilikuwa limetegwa kwenye zawadi na lililipuka muda mfupi baada ya kufika nyumbani.


Bwana harusi huyo ambaye alikuwa pamoja na kaka yake, alifariki papo hapo, huku kaka yake akifariki kutokana na majeraha alipokuwa akipata matibabu hospitalini.


Watu wengine wanne, akiwemo mtoto wa miezi 18, walijeruhiwa katika mlipuko huo, ambao uliotokea Jumatatu, Aprili 3, nyumbani kwa bwana harusi katika Wilaya ya Kabirdham katika Jimbo la Chhattisgarh nchini India.


Polisi wamesema mlipuko huo ulikuwa mkubwa kiasi kwamba kuta na paa la chumba hicho zilianguka.


Mtuhumiwa huyo, Sarju Markam kutoka jimbo jirani la Madhya Pradesh amekamatwa Jumanne Aprili 4. Markam mwenye umri wa miaka 33, alikuwa na uhusiano na bibi harusi huyo mwenye umri wa miaka 29 ambaye awali alitaka awe mke wake wa pili.

 
Back
Top Bottom