Burundi kuna amani sana, lakini kule Kigoma ndiyo kwanza recruitment zinaendelea

BLACK MOVEMENT

JF-Expert Member
Mar 11, 2020
2,712
6,515
Ukitaka kujua wakimbizi ni Biashara nenda Kigoma kwenye zile kambi, kule kuna wakati zile NGOs zilizo jazana kule zilikuwa zina gombana wao kwa wao kila mmoja ikipigania kuwahudumia wakimbizi. Kuna wakati zilijuwa na bifu la kufa mtu, sasa jiulize kwa nini bifu kisa wakimbizi?

Kule kwenye makambi ni kawaida kukuta zile NGOs tena za nje zina hamasisha wakimbizi mule makambini wazaane kwa wingi make tue more wanavyo zaana ndo the more pesa inaletwa.Lakini hizo hizo NGOs huku mtaani zinahamasisha uzazi wa moango.

Turudi kwenye Maada, Kwa sasa Burundi kuna amani kuliko wakati wowote ule na Raisi wa sasa amepiga hatua kubwa sana kwenye swala la amani na alisha wasamehe hata wafungwa wengi wa kisiasa. Cha ajabu kwenye yale Makambi kule Kigoma ndo kwanza unakuta wanaajiri staff na huwa hata wana wahonga wakimbizi wakatae kurudi kwao ili wao waendelee kula pesa.

Zile NGOs plus UNHCR wenyewe hawako tiyari kuona wakimbizi wanarudi Burundi ndo maana huwa kuna kila aina ya jitihada za kuwafanya wasiondoke.

Kuna ile tuhuma za shirika la kuhudumia wakimbizi la Denmark kule linaitwa DRC yaani Danish refugees council, kuna wakati Walikamatwa na Sare za jeshi wana wagawia wakimbizi wanao taka kurudi Burundi, lengo ni ili wakalianzishe tena, ile seke seke naona ilizimwa juu kwa juu.

Yale mashirika maombi yao ya kila siku ni amani isiwepo Burundi.
 
Back
Top Bottom