Duh ingekuwa kujichotea basi ingekuwa kazi saana. Kila kitu kina usimamizi. Wale ni banker wa serikali ndio maana miaka kama 2 iliyopita serikali ilitangaza kuondoa fedha zake zote (S ikumbuki vizuri zinakadiriwa kuwa trilioni 2) kutoka kwenye benki binafsi. Na madhara yake yakaelezeka kwa kirefu saana. Wale jamaa pale BOT hawana ubavu mbele ya serikali kabisaa. Si kama mie na CRDB. Inasemekana Dr Idrisa wakati akiwa Governor alijifanya kogoma kutoa pesa kwa ajili ya kampeni, wakamuweka kando. Kwahiyo elewa si seperate entity. Ni nadharia tu hususani kwa nchi yetu.Kwahiyo unataka kusema serikali ikitaka pesa inaenda kujichotea tu BOT? Mimi naamini uhusiano kati ya BOT naserikali hauna tofauti na uhusiano wa CRDB na wewe kama account holder wa CRDB na wewe mfano ni mmoja wa directors wa CRDB. Kama wewe ni mmoja wa directors wa CRDB, unaweza tu kwenda kujikopea unavyotaka? Je, unaweza kwenda kujichote tu pesa pale?
Nadhani hata commercial banks zina accounts BOT, kama vile ambavyo serikali ina accounts BOT.
Tena shukuru hapa serikali ndio inasimamia BOT. Unajua kwamba Federal Reserve ya marekani ni partly privately owned organization?