Thamani ya shilingi ya Tanzania imekua ikishuka mfululizo mwaka hadi mwaka kutoka shilingi 20 kwa dolar miaka ya 1980 hadi tulipo shiling 1,330+ kwa dolar mwaka huu. Wataalam wa uchumi wanasema, thamani ya hela ya nchi inakua imara pale ambapo nchi husika inazalisha bidhaa nyingi za kuuza nje kiasi kwamba mahitaji ya fedha yanakua makubwa kwa watu wa nje. Yaani demand ya hela ikiwa kubwa thamani yake kwa dolar inakua kubwa.
Hivyo hivyo kama uzalishaji ni mdogo na nchi inapata mahitaji yake mengi kutoka nje, demand ya dolar inakua kubwa na dhamani ya dolar inapanda ukilinganisha na hela ya ndani. Kwa Tanzania tunauza nje mazao ya kilimo, madini, utalii n.k kupata fedha za kigeni ambazo tunahitaji kununulia mahitaji mbalimbali kama nguo, magari, malighafi, na wataalam.
Udhibiti wa fedha za kigeni uko chini ya Benki kuu ya Tanzania (BOT) na inatakiwa kuhakikisha hela ya kigeni inayopatikana inatumika kuagizia bidhaa au huduma zinazohitajika hapa nchini. Inatakiwa kuhakikisha kuwa hela ya kigeni haihamishwi kuhifadhiwa nchi nyingine. Wasiwasi wangu ni kwamba kwa jinsi Bureau de change zilivyo tapakaa hapa nchini na ufisadi uliopo BOT je kuna udhibiti wa kutosha kuhakikisha watu hawanunui dolar zilizopo na kuhamishia nje?
Je kushuka kwa dhamani ya shilingi yetu hakusababishwi na hizi bureau de change kuliko tunavyofikiri kwamba tunazalisha kidogo?
Nawasilisha.