Bungeni Kunawaka Moto

hizo ni kelele za wapumbavu wa CDM, hakuna lolote hapo. Mwisho wa maneno ni kwenye kupiga kura na hapo ndio mtajua nini maana ya kuwa na wabunge wachache.

CCM ndio dume lenu nyie.
Mkuu naona siasa imekupita mkono wa kushoto, Mhe. Kafulila siyo mbunge wa CDM, ni mbunge kupitia NCCR-Mageuzi
 
Tatzo bdo ana stress, jana Lowasa kamjibu khs maamuz magumu kua 'mi nimewaambia wakitaka watafanyia kaz wakitaka wataacha'. Anatafuta jins ya ku take over
 
hivi zile furniture za CCJ na ile ofisi nani anatumia? mzee 6 si ndo kazilipia.
 
ndugu wana JF alichofanya mr.six ni kuokoa kiti pale ambapo mheshimiwa mbunge wa kambi ya upinzania na si cdm aliponukuu maneno ya mheshimiwa marehemu baba wa Taifa kuwa Taifa lisilokusanya kodi ni Taifa legelege, mheshimiwa Mb wa Nzega aliomba mwongozo wa Spika kuwa ameumizwa na kukwazika na maneno ya mheshimiwa Mbunge aliyekuwa anachangia hoja ya wizara ya afya kwamba budget iliyotengwa ni finyu na kwamba wote mle ndani including mzee Sita haoni hilo kwani wanatibiwa nje.

Ndo ubishi kati ya kiti na mbunge ukaanzia hapo na mwisho wa siku baada ya Mb. kukataa kufuta usemi wa Taifa legelege ambapo tafsiri yake kwa wana CCM ni wao ndo mzee Sita akaomba mwongozo na kusema wapinzani ni wanafiki na kwamba wasitiliwe maanani na kwamba nje ya bunge wananchi wanaona tabia zao na mwenendo wao.

Kauli ya mzee sita inakatisha tamaa na amejidhihirisha kuwa anatumia muda na nguvu nyingi kujisafisha mbele ya wenzake ili panga lisimfike. LAkini ni mwendelezo wa waziri mwenzake Marry Nagu pale mbunge wa upinzania aliposema watoto wa mawaziri na wabunge wanatibia kwenye hospitali kubwa na kwamba hili limesababisha ufa kati ya walionacho na wasionacho.

Kwamba kwa sasa hakuna anayejali hospitali za wilaya na dispensaries. Mary Nagu bila hiana akaomba mbinge afute kauli kwani mtoto wake no dr. wa Muhimbili na kwamna anatibu watu wa status zote na kwamba hata kule kijijini baba yake Nagu na yeye mwenye niko wanakotibiwa.

Wakati mheshimiwa mbunge alipokuwa anaonge ilidhihirika wazi kwamba kauli yake ilikuwa inawasha moto taratibu kwani hata sura ya waziri Lukuvi ilikiuwa imekereka na maneno yale.
 
hizo ni kelele za wapumbavu wa CDM, hakuna lolote hapo. Mwisho wa maneno ni kwenye kupiga kura na hapo ndio mtajua nini maana ya kuwa na wabunge wachache.

CCM ndio dume lenu nyie.

Kaka unawatukana Chadema bila ya sababu unaona ukiwa na chuki unafanya mambo hovyo hovyo .Kafulila ni NCCR Mageuzi na si Chadema .CCM kweli akili zenu zimepinda
 
hizo ni kelele za wapumbavu wa CDM, hakuna lolote hapo. Mwisho wa maneno ni kwenye kupiga kura na hapo ndio mtajua nini maana ya kuwa na wabunge wachache. CCM ndio dume lenu nyie.
Inaelekea CCM ndo inakuweka mjini, wewe na CCM yako hiki ndicho kipindi chenu cha mwisho KUIBA. Comes new Katiba wewe na CCM yenu tutawaacha mnaoza by the road side. wezi wakubwa nyinyi
 
hizo ni kelele za wapumbavu wa CDM, hakuna lolote hapo. Mwisho wa maneno ni kwenye kupiga kura na hapo ndio mtajua nini maana ya kuwa na wabunge wachache.

CCM ndio dume lenu nyie.

Maandiko Matakatifu Biblia inasema,
" Amwambiaye mtu mwovu, wewe una haki;
Kabila za watu watamlaani, taifa watamchukia.

Bali kwao wakemeao furaha itakuwako;
Na baraka ya kufanikiwa itawajilia." Mithali 24:24-25
 
Haya madai kwamba Mbunge asiseme maneno ya 'KUUDHI' sio sahihi hata kidogo. Bunge linatafsiri gani ya neno hili? Ina maana mbunge anatakiwa aseme maneno ya 'KUFURAHISHA?' Maana kinyume cha kutokuudhi ni kufurahisha. Ni maneno yepi hasa yanaangukia kwenye kapu la KUUDHI na yepi yanaangukia kwenye kapu la kufurahisha?

Kwa mfano kama Waziri wa nchi anautangazia umma kuwa 'mgao wa umeme' umekwisha, lakini bado mgao unakuwepo utamwita ni mtu 'makini' badala ya mtu 'mwongo' kwa sababu bunge haliruhusu 'kumuudhi?. Hivi nani anaudhika? sisi wananchi tunaodanganya, menyeka na kunyanyasika kutokana na uzembe wa serikali au 'hao wakubwa' wanatembelea mashangingi'? Ina maana hata kama wanakosea hawataki kusikia tunalalamika kwa sababu 'tunawaudhi? HILI NENO KUUDHI LIONDOLEWE mara moja kwenye kanuni za uendeshaji mijadala ya bunge. Ufisadi wa fikra!
 
Nimekutana na makelele ya mwisho nilichelewa..ila nimeshangaa sana; nchi iko katika kipindi kigumu cha mpito...wanamaombi ombeeni nchi hii si utani nawambia, hii nchi inaweza anguka siku moja tu na kuisha
 
Kila mbunge ni mtanzania na anayo haki ya kueleza analysis yake kuhusu anayoyaona yakitendeka haswa yakifanywa na viongozi waliopewa dhamana ya nchi hii. Kitendo cha mawaziri kusimamisha masikio na kuanza kuomba mwongozo ni kutaka kuviza mawazo ya watanzania hususani wabunge wenye foresight na mawazo mbadala. Status quo iliyozoeleka ya kusifia hotuba hata kama ni feki kama za kuhamasisha bajaji kama ambulance ni kuudhihirishia umma kwamba uwezo wetu wa kufiki na kuona mbali ume expire. Nampongeza Kafulila kwa kuliweka hilo bayana na usiogope Mkuu tunakuunga mkono
 
Mwaka huu namuomba Mungu anilinde niendelee kuishi ili nione mengi zaidi ya kushangaza. Angalau nipate cha kusimulia huko waendako.
 
Edson, sote tunajua kuwa Sita sio kilaza. Tunafahamu uwezo wake wa kumudu mambo. Shida hapa ni moja kuwa ukiwa CCM ni lazima ukubali kuwa mnafiki. Ijumaa alipokuwa nanazungumzia muungano yeye kama kaimu kiongozi wa shughuli za serikali bungeni alisema: "Ninayoyasema siyo ninayoyaamini mimi kama mimi ila hii ndiyo historia. ..." Kwangu mimi, hapo alimaanisha anasema kwa vile yuko huko.
Mwangalieni mtoto wa mkulima alivyochuja ... Ni sababu ya kutaka kutetea mlo kwenye sahani. Ili hilo lifanikiwe ni lazima uwe mnafiki wa nafsi yako mwenyewe.

Maoni yako yametulia kweli kweli siyo siri.
 
hizo ni kelele za wapumbavu wa cdm, hakuna lolote hapo. Mwisho wa maneno ni kwenye kupiga kura na hapo ndio mtajua nini maana ya kuwa na wabunge wachache. Ccm ndio dume lenu nyie.
m typin ths with my middle finger... Fool, u nd to shtup smtm..
 
Back
Top Bottom