Bunge laondoa kigezo cha kupitia JKT na JKU kuajiriwa vyombo vya ulinzi

Ni jambo zuri sana kuondoa hiko kigezo.

Kingekuwa na umuhimu kama wangekuwa wanaweka milango wazi kwa kila anaependa kupata mafunzo ya awali apitie JKT.

Walau ingeleta maana, lakin kwa utaratibu wa sasa kupitia mafunzo tu hayo ni bahati ya wanaochaguliwa. Kuna vijana wangependa kupata hayo mafunzo, kuna wengine wameenda lakini hawakutaka sema ndo umechaguliwa.

Mbona zamani tuliweza raia kujiunga kwenye majeshi bila hizi JKT za sasa? Hofu inatoka wapi? Ama kwa vile mtu amepitia JKT basi ndo ajipe umuhimu zaidi? Hapana, wote tutawapa nafasi sawa, sema uliyepitia JKT utakuwa walau na faida katika mafunzo.

Maana mitaala ya kijeshi ukiingia ni sawa haujapitia JKT, wote mnaanza sawa kila hatua.
 
Duh hili limenifikirisha sana.

Nakumbuka mwezi wa 9/10 mwaka jana niliitwa home na shemeji(kaoa kwetu) nikaamua kutii wito kwenda kumsikiliza, nilipofika nikakutana na story za kwenda jkt kwa kujitolea for 2 years na walikua wameshanitumia maombi, hapa inatakiwa after 2 days niende interview.

Plan ilikua baada ya kumaliza jkt ndo nirud home nitafutiwe nafasi JWTZ

Nilikaa usiku mzima nawaza kuhusu hili, ikumbukwe form six tu kwa mujibu nilipangiwa RUVU nikakacha nikaenda kupiga Tempo shule fulani huko.

Maamuzi nilio yaamua nikuondoka bila kuaga. Nikawatumia tu sms kua siwezi kwenda jkt kwa sasa.

Waka ni mind mwisho yakaisha.

Nikarudi town kuendelea kupambana kwa hasira zaidi kama yatima. Na mwezi wa 11 nikafanikiwa kupata ajira flani private.

Leo nakaa nawaza ningekua huko makambini naliskia hili tangazo si ningeangua kilio na kutoroka mafunzo..

Moral of the story. Usiruhusu watu wakupangie maisha yako hata kama ni wazazi wako. Wanatakiwa wakushauri lkn maamuzi ni yako.
 
Sio kweli kama wanataka kuingiza watoto wao wakaacha kuwaweka kwenye taasisi kama BoT, TPA au TRA.

Ifaamike kwamba JWTZ ina misingi yake iliyo imara sana. Kozi inayofanyika RTS au TMA sio kozi lelemama kwanba wanaweza kuwapenyesha vijana wao, ata kwa waliopitia JKT/JKU habari wanayo ila kupitia huko ilikua ni moja wapo ya mchujo ambao ulikua unapunguza watu kwenye usaili wanapohitaji.

Sasa fikiria wakitangaza nafasi za kujiunga na jeshi bila kigezo cha JKT nadhani watafanyia huo usaili Uwanja wa Taifa maana idadi itakuwa kubwa mno.
Walala hoi wana wasi wasi tu.

Yani mtu kama Waziri ang'ng'anie kumpeleka mwanae JWTZ? Kweli exposure yake bado itakua haijamsaidia.

Bado hizo ni kazi za walala hoi tu, hakuna national cake huko.

Mimi niwe waziri alafu nimpeleke mwanangu TISS bado elimu yangu haijanisaidia.

Maranyingi inakua wazazi wako JWTZ ndo wanatamani na mtoto awe JWTZ. Au wazazi wako TISS nae anatamani mtt awe huko.

Kwahyo walala hoi wenzangu toeni wasi wasi.
 
Miaka ya zamani sana, TPDF ilikua inafanya direct recruitment kutoka uraiani lakini baadae ikaja kusitisha baada ya kuibuka layer ya askari/maafisa wasio na weledi. Unakuta mtu alikua jambazi, changudoa, mwizi etc. lakini anavumilia miezi minne ya depo tayari anakua muajiriwa. Hakuna kipindi kinachopima uvumilivu kama cha u-service man. Tena kwa sisi tuliopitia vikosi vya malezi kama 837KJ kipindi hiko, fatiki za shamba ni za kutosha hadi wengine wakaanza kujiengua mmoja mmoja kwa kutoroka. Kwa msoto unaopitia JKT, ukibahatika kuajiriwa lazima uwe na weledi na nidhamu ya hali ya juu tofauti na mtu aliyepitia moja kwa moja uraiani. Somehow hata kwa maafisa , unaweza ukaona tofauti kati ya afisa aliyepitia JKT, akapitia maisha ya uaskari na baadae kwenda officer cadet, na wale madogo wa BMS ambao wanachukuliwa mujibu wa sheria wanaenda miaka 3 TMA wanapewa kamisheni. Wengi wao hua wana lack leadership skills, hata uwapeleke exposure popote wakirudi kwenye loc zao wanaonesha unanga wao.
Hawa hawajui kitu. Jeshi ni JKT. Mtiti wa JKT ni mgumu kuliko ule wa jwtz.
Jkt hata muda wa kuoga hakuna. Ratiba ya mapumziko hakuna.
TPDF kozi zao jumapili miguu juu. Zina mpaka ratiba za kuoga
 
Back
Top Bottom