Bunge la Tanzania ndilo linalokaa vikao Muda mrefu sana Dunia nzima

BLACK MOVEMENT

JF-Expert Member
Mar 11, 2020
2,712
6,516
Nimejaribu kupitia vikao ya Mabunge kwanza yanayo fuata mfumo wa Jumuia ya Madola, nikajiridhisha kwamba Bunge ka Tanzania ndio Bunge linalo tumia muda mrefu sana kukaa vikao vyake miongoni mwa mabunge yote ya Jumuia ya Madola, haoa nazungumzia kutumia miezi mitatu Dodoma watu wakijadiki bajeti.

Pia nimejaribu kufuatilia mabunge nje ya Jumuai ya Madola nako bado still Bunge la Tanzania linaongoza , bunge la bajeti hutuchukua miezi mitatu na zaidi watu wakiwa Dodoma wanajadili bajeti, hii ni record za Guiness World Book of record.

Cha ajabu impact ya aanacgo kijadili huwa ni ndogo sana kwenye jamii, zaidi ya wao kukunja pesa kila siku pale Dodoma.

Hakuna nchi yoyote hata zenye uchumia mkubwa ambapo Bunge lake hukaa vikao kwa nuda mrefu hivyo, na cha kusikitisha pale Dodoma wanacho fanya ni mijadala tu isio kuwa na nguvu yoyote, ni mijadala isio kuwa na maana na hakuna maazimio wanayo pitisha ili kwamba yafanyiwe kazi.

Wanacho fanya wakina Msukuma ni kulia lia pale Dododma waonekane wana mchango wa maana na mwisho wa siku hupitisha hizo bajeti kwa asilimia 100.

Kuna haja gani kutumia zaidi ya miezi mitatu kupitidha bajeti ya kila wizara na baadae tena aje kupotisha jumla yake?
 
Kati ya makundi sina imani nayo ni hili genge linalojifanya kutetea wananchi huku likitafuna kila kilicho cha wananchi .genge hatari sana hili. Linaisimamia serikali ila kazi ni kusifu na.kuabudu Rais
 
Back
Top Bottom