Bunge la Tanzania laendeshwa kwa uzoefu badala ya kanuni

QUALITY

JF-Expert Member
Sep 27, 2010
853
115
Leo Anna Makinda (mh. Spika) ameniachaa hoi. Amesimama na kusema kwa mujibu wa kanuni, bunge lintakiwa kuchagua watu watatu watakaosaidia uendeshaji wa Bunge. Akasema vigezo ni kuzingatia jinsia, wagombea wawe ni wenyeviti au makamu wa wenyeviti wa kamati za kudumu. Akasema ... sasa nimeleta kwenu majina matatu ili myapitishe.

ndipo mbunge (mwanamke) akamwuliza kwa kusoma kanuni akisema kanuni inataka spika kuwasilisha majina sita na kati ya hao wachaguliwe watatu. je kuleta watatu si kukiuka kanuni? Hapo ndipo makinda alipoanza kuchemka Oh umeenda mbali!! Oh Tunatumia uzoefu kwa sababu hii ni kazi ngumu!! Oh Tusibishane!!

Mwulizaji akaongeza, kama umevunja kanuni, twambie. Hapo ndipo na Lukuvu kasimama kutetea hoja (akitoa pumba bila kunukuu kifungu cha kanuni kinachompa mamlaka spika kuvunja kanuni na kutumia uzoefu kuendesha bunge).
Je Uzoefu bila kanuni, Tutafika?
 
Wanaendesha kama wanafanya ushindani,matokeo yake wanasahau kutumia kanunu yaani inatia kichefuchefu spika anapojichanganya bungeni kila kikao.
 
hahahaha lol
Hii case imenikumbusha enzi za Marehemu Chacha Wangwe na Mzee Sitta, Wangwe alimuambia Sitta "....... bunge haliendeshwi kwa tamaduni na mila za kitanzania bali kanuni za bunge...." Mzee Sitta na viwango vyake alitaptapa sana.
R.I.P. Kamanda Wangwe
 
Mkuu unashangaa nini! Huyu mama siku zote ni dikteta, hat alipokuwa naibu spika. Mimi nilijua tu ataendelea na hizo sera.
Leo Anna Makinda (mh. Spika) ameniachaa hoi. Amesimama na kusema kwa mujibu wa kanuni, bunge lintakiwa kuchagua watu watatu watakaosaidia uendeshaji wa Bunge. Akasema vigezo ni kuzingatia jinsia, wagombea wawe ni wenyeviti au makamu wa wenyeviti wa kamati za kudumu. Akasema ... sasa nimeleta kwenu majina matatu ili myapitishe.

ndipo mbunge (mwanamke) akamwuliza kwa kusoma kanuni akisema kanuni inataka spika kuwasilisha majina sita na kati ya hao wachaguliwe watatu. je kuleta watatu si kukiuka kanuni? Hapo ndipo makinda alipoanza kuchemka Oh umeenda mbali!! Oh Tunatumia uzoefu kwa sababu hii ni kazi ngumu!! Oh Tusibishane!!

Mwulizaji akaongeza, kama umevunja kanuni, twambie. Hapo ndipo na Lukuvu kasimama kutetea hoja (akitoa pumba bila kunukuu kifungu cha kanuni kinachompa mamlaka spika kuvunja kanuni na kutumia uzoefu kuendesha bunge).
Je Uzoefu bila kanuni, Tutafika?
 
huyu mama kwa kweli anakoelekea c kuzuri hata kidogo, anaamua kupindisha kanuni wazwaz na wabunge werevu wakihoji hasa wa upinzan (CDM, kwan hao wengine haswa wa CUF ni sawa na CCM tu, fikra zao kwa sasa ni Mgando) huyu mama anakuwa mkali, na kiundani hapa ni kwamba analinda au kuendeshwa na baadhi ya watu ndan ya serikal haswa CCm, akumbuke kwamba anaposimama kama spika anawakilisha bunge la watanzania bila kujali CCM au upinzani. mama tumia kanuni badala ya UZEEFU
 
BUnge limemshinda huyo hili bunge la 10 sio saizi yake kabisa, alitakiwa ajipange upya kwanza ukimtoa makamba kwa kukiharibu chama chao huyu spika nae anafuatia kukivunja chama chao cha magamba.... mwenzie makamba kajivua gamba yeye sijui atajivua kitu gani ama atavaa lile gamba lilitoka kwa makamba???
 
Hamna kitu kizuri kama historia duniani, unajua historia itamuhukumu yeye na ccm yake, sasa kwa mawazo mgando aliyonayo anaona anaisaidia ccm lakini ukweli anaimaliza, sijui hao consultants ccm inaowatumia hawawaambii kuwa mambo yanazidi kuwa mabaya hasa kwenye situation kama hizo!!
 
Back
Top Bottom