Mwaka 2006 DP World ya Dubai ilinunua kandarasi ya kuendesha shughuli za Bandari sita za Marekani. Wabunge wa chama tawala na upinzani kwa pamoja waliopinga DPW kupewa kazi hiyo. Wananchi nao walipinga 3:1 katika kura za maoni.
Bunge likapitisha muswada wa Sheria kuzuia kampuni za kigeni kusimamia Shughuli za Bandari ili kulinda usalama wa bandari na wageni kutojihusisha na shughuli za Idara ya Forodha.
Rais George W. Bush alishatishia hatasaini (veto) muswada huo kuwa sheria kwa sababu 'itapeleka ujumbe usiofaa kwa nchi rafiki'.
Mara baada ya muswada kupitishwa na Bunge DP World wakajitoa kwenye uwekezaji huo ili kuondoa msuguano ulioibuka.
Sisi Watanzania tunajifunza nini toka Bunge la Amerika?