Nikupateje
JF-Expert Member
- Dec 22, 2009
- 1,334
- 988
Kinachoendelea bungeni sasa hivi tumekiona. Kwamba Tundu Lissu na wenzake wanamshtaki Spika Anne Makinda kwa kukiuka kanuni.
Ukiitizama hii kwa umakini kinachoelekea ni kwamba inawezekana Spika ama amelidanganya bunge.
Lakini hoja ya Spika ilikuwa kwamba akina Tindu Lissu tayari walikuwa na kesi mahakamani. Hivyo yeye kama Spika angeruhusu hoja ile, ingekuwa ni kulifanya bunge liingilie uhuru wa mahakama.
Wakati Tundu Lissu hoja yake ni kwamba hakushitakiwa kwa yale mauaji bali alishtakiwa kwa kungia kwenye eneo lile.
Wote tumesikia hoja hizi mbili. Ya Spika na Tundu Lissu. Na zote mbili si hoja za kupuuza. Cha msingi ni ipi hoja yenye ukweli itakayosambaratisha ya mwingine. Hivyo tusubiri mwisho wake.
Ninakubali kwamba bunge, mahakama au dola ni mihimili mitatu isiyotakikwa kungiliana. Sina haja ya kutaja mifano mingi lakini tumeona heshima ya mahakama kwa bunge kwa suala la independe candidate a.k.a Kesi ya Mtikila.
Ninahitaji kusadiwa uelewa kwa ninachokiona ni tatizo. tatizo kwangu ni kwamba ni aina gani ya mawasiliano rasmi yanayotumika kwa vyombo hivi vitatu kwa masuala haya kuhakikisha hayaingiliani.
Nakumbuka Spika huyuhuyu aliwahi kushauri kwamba habari za magazetini zichukuliwe kama barua. Kwa mtizamo huu ninashawishika kuamini kwamba kama kesi ya akina Lissu iliendeshwa kule Tarime basi taarifa ya magazeti si taarifa rasmi kwa spika na bunge. Mwalimu wetu Anna Makinda kishatufundisha kwamba tunaweza kuichukulia kama barua.
Hivyo mama yetu Anne Makinda (kiumri kwangu ni mama), alipomkatiza Tundu Lissu kuongea suala lile ninaamini kuna mawasiliano rasmi aliyoyapata kwamba lile ni suala la mahakama, halihitajiwi bungeni.
Na kama kweli yapo mawasiliano rasmi toka mahakamani kwenda bungeni katika kippindi hiki cha technology, basi tutegemee Tundu Lissu asifike mbali, kwani atakachofanya Anne Makinda ni kutoa ushahidi wa taarifa ya Mahakama ikimtaarifu yeye kwamba "hawa wabunge wako wana kesi hii na huku Tarime".
Ndicho ninachokitegemea kwa uelewa wangu. Sijui ni uelewa mzuri, mbaya au mdogo, waheshimiwa JF thinkers mtaamua.
Kama si hivyo, yaani kama hakuna mawasiliano rasmi, basi hakuna tofauti na bunge kuwa kama wana-Kariakoo na kule ninakoishi mimi. Kwani kama Spika alitegemea taarifa za media basi hiyo media tunaiona au tunaisoma wote kule kwangu (ninakoishi), Kariakoo (Dar), Mwigobelo (Musoma), Mwaloni (Mwanza), Kibororoni (Moshi), Bristol (London).
Maana pamoja na kwamba ni kweli huko hakuna mpangilio wa kusema kama bungeni, lakini jinsi wanavyonunua magazeti ndivyo kila mmoja duniani anavyonunua na kuyasoma. Kwa hili hatutofautiani. Na kama ni hivyo, basi ni hatari sana kwa bunge kama bado lina mtindo huu.
NImesema kama bado lina mtindo huu kwani ninataja mfano mmoja wa miaka ya tisini. Kuna wakati Augustine Mrema aliwahi kutakiwa kuleta ushahidi bungeni. Siku ya kusoma hukumu yake kumfungia kwa muda vikao msomaji alivikebehi kuwa vile vilikuwa ni vipande vya magazeti ya Shaba.
Hivyo, naomba msaada wenu kujua ni vipi hasa mawasiliano yanavyokwenda kati ya mahakama na bunge.
Wenu katika kutumaini kueleweshwa.