Juliana Shonza
JF-Expert Member
- Dec 19, 2012
- 2,009
- 1,607
Aliyekuwa Katibu wa wilaya ya Lindi mjini wa Chadema, Ndg. Abdalla Madebe ambaye alikuwa ndiye mpigadebe mkubwa wa Mbunge wa CUF Lindi mjini anayemaliza mda wake, Mhe. Salum Baruan, akibebwa na wananchi baada ya kutangaza kuhamia CCM, katika mkutano wa kampeni uliofanywa na Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan katika eneo la Mnazi Mmoja, mkoani Lindi.
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Ndg Nape Nnauye akimkaribisha jukwaani, Aliyekuwa Katibu wa wilaya ya Lindi mjini - Chadema, Abdalla Madebe ambaye alikuwa ndiye mpiga debe mkubwa wa Mbunge wa CUF anayemaliza mda wake wa Lindi mjini, Salum Baruani, wakati alipoamua kutangaza kuhamia CCM.
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) kutoka Wilaya ya Lindi Mjini na Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Mama Salma Kikwete akihutubia katika mkutano huo, uliofanyika Mnazi mmoja jana.