Bundi aingia ndani ya ukumbi wa Bunge leo asubuhi

Kwaiyo baada ya muswadaa kuwa Ignored Upinzani ikaamua kutuma Bundi ili kuwatisha!?

Sent from my SM-J530F using Tapatalk
 
Hahaha wanahangaikia nini, waache ccm waendelee, na uchaguzi ujao wasishiriki tuone ccm wanachotaka kufanya. Mnajua outcome halafu mnajaribu.
 
Unafahamu ni kwa nini Bundi alikaa muda wote huo hapo nyumbani kwenu? Kwa vyovyote vile, Mdogo wako alikuwa mgonjwa sana na hivi alikuwa anatoa Harufu ambayo ninyi haikuwa rahisi kui-detect lakini kwa kuwa Bundi ni very sensitive to smell, basi yeye alikuwa hapo akivizia mawindo akihisi sehemu hiyo kuna mzoga. Vinginevyo,Bundi hana uhusiano wowote na kufariki kwa Mdogo wako.

Kama Bundi ndiye alikuwa anahusika na kifo cha mdogo wenu, ni kwa nini akae hapo wiki nzima? Kama ana uwezo Wa kumchukua mtu au kumfanya afe,kwa nini asubirie muda wote huo?
Were huwelewi nadharia iliyopo. Kimsingi sio kwamba bundi anauwa, ila anakitu kama unachosema kwamba anavuta hisia au harufu ya mtu anaekaribia kufa. Kwahiyo ukimuona bundi maeneo yenu ujue hakuna dalili mzuri halo mtaani kwenu. Yani km unavyoona nzi Na mizoga kwani nzi ndo anauwa?
 
Nilichanganya kidogo mambo, unajua leo asubuhi palikuwa na bundi, bundi ‘original’ hapo juu hapo, lakini sisi Dodoma bundi wa mchana hana tatizo ila wahusiku ndo shida".Job Ndugai JAN 29,2019-Dodoma

View attachment 1007609

======

BUNGE: Ndege aina ya Bundi ameingia ndani ya ukumbi wa Bunge Dodoma asubuhi ya leo wakati Mkutano wa 14 wa Bunge la 11 ukianza kikao chake cha kwanza lakini Spika wa Bunge Job Ndugai aliwatoa hofu wa Bunge kuwa Bundi wa mchana hana madhara kama wa usiku.
Dah!!ni hatari sana,
tapatalk_1519618280004.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi nafikiri kuna kitu bundi anahisi ambacho sisi binadamu hatukioni.
Biologically Sense ya smell ya bundi IPO juu anaweza kuditect harufu ya uozo was cell zinapokufa ,harufu hii binadamu hawez kuisikia and mind that bundi hula mzoga,,ko anapotokea pahala ujue kasikia harufu ya mzoga au mzoga tarajali ,,ila hii incidence ya bungenii ni mambo yao ,,sooon utasikia maalbino wanawindwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Iman
Hizo ni imani za kizembe,eti bundi wa mchana hana tatizo,ila angekuwa wa usiku,sasa hapo unawafundisha nini watoto?Bundi ni ndege tu kama ilivyo wengine.Sijajuwa labda kwa wale wasiojulikana kama wana bundi wao maalumu!
Mkuu kunaukweli ambao unaunganishwa na imani za kishirikiana....bundi anauwezo mkubwa wa kunusa dead cells maana ni mla mizoga...sasa ipo hivi mtu anapoumwa mda mrefu kumbuka cell zinazidi kufa kwenye mwili wake ndiyo maana unaweza kusikia bundi amelia mtaani haipiti siku kadhaa unasikia mtu amefariki mtaani hapo,ukifatilia aliekufa utakuta ni mtu aliyeugua mda mrefu,bundi alinusa harufu ya mzoga,yaani mtu ambae cell zake nyingi zimekufa bundi anahisi kunamzoga ndiyo maana husogea karibu na eneo husika....jaribu kuchunguza

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu kunaukweli ambao unaunganishwa na imani za kishirikiana....bundi anauwezo mkubwa wa kunusa dead cells maana ni mla mizoga...sasa ipo hivi mtu anapoumwa mda mrefu kumbuka cell zinazidi kufa kwenye mwili wake ndiyo maana unaweza kusikia bundi amelia mtaani haipiti siku kadhaa unasikia mtu amefariki mtaani hapo,ukifatilia aliekufa utakuta ni mtu aliyeugua mda mrefu,bundi alinusa harufu ya mzoga,yaani mtu ambae cell zake nyingi zimekufa bundi anahisi kunamzoga ndiyo maana husogea karibu na eneo husika....jaribu kuchunguza

Sent using Jamii Forums mobile app
kuna mdao nae aliuliza vipi kuhusu hospitali ambazo kuna wagonjwa wengi wanakufa na hakuna hao bundi wakati huko ndipo kuna watu wengi ambao seli zao zimeanza kufa.
 
Nani kakudanganya kuwa bundi hula mizoga?. Bundi hali mizoga. Bundi huwinda wanyama wadogo wanaotembea usiku. ( panya, nyoka, vyura, paka , Hata sungura, ndege wlio ndani ya viota.).
Wanaokula mizoga, ni mwewe, tai,na kunguru,
Huyo bundi kaleta noma hapo bungeni, tena mchana kweupe. Huo mswaada wa vyama hauwaachi salama. Ngoja wajidanganye eti bundi wa mchana hana madhara.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa hiyo,Bundi ni Mnyama Wa Shetani? Na kama ndivyo,huyo shetani amejichagulia tu Bundi Wa Afrika na wa sehemu zingine Duniani anawaogopa?
Bundi,Fisi,Paka,Wolf,Popo ni miongoni mwa wanyama wa Ishara/matumizi nguvu Giza unapowaona katika mazingira ya kutilia mashaka usichelewe kupiga dua..
 
Ni mambo ya kujidhalilisha sana. Mtu kama Ndugai,Spika anayeongoza wasomi Wa kuanzia Darasa la Saba hadi viwango vya PhD na yeye akiwa msomi Mwenye Degree mbili, badala ya kuwaelimisha wabunge kwamba huyo ni ndege kama Njiwa, Popo na kadhalika, yeye anawatoa hofu wabunge kwa kuwaambia kwamba Bundi huyo angalikuja maeneo hayo usiku ndio wangalipaswa kuwa na hofu lakini sio huyo Wa mchana!

Hivi kwa uelewa kama huo,Ndugai anafahamu maana ya kuwa Spika? Kuwa Spika maana yake sio kufahamu tu Kanuni za Binge na Kuunda Kamati za Bunge bali inabidi pia uelewa wake juu ya mambo mengine(General Affairs) uwe mpana sana ama sawa na Wabunge au Zaidi ya wale anaowaongoza.
Mkuu bundi hawezi kuwa sawa na njiwa,kama wakristo hutumia ishara ya njiwa mweupe kama amani na Uwepo wa roho mtakatifu,kwa upande wa pili yupo Bundi mwakilishi wa nguvu giza..usipinge uwepo wa nguvu za giza kisa Elimu..
 
Lazima baadhi ya wabunge wameenda Kwa waganga ili wakapewe tafsiri na kwanini Bundi kaingia na Hata kama alikuwa anajipitia tu,Leo watakuwa wamepiga hela Kwa kuwadanganya
 
Bundi? Inawezekana ni mchezo wa ccm kuvuruga mjadala wa muswada wa vyama vya siasa. Wabongo wanavyopenda udaku na umbea, basi hapo kesho wataulizia habari za bundi; na sio nyinginezo.
 
Ni ishara ya Kifo cha Taifa!

Huo muswada wa sheria ya vyama vya siasa ni msumari mbaya wa mustakbali wa Taifa hili!

Farao alipewa Ishara za Vyura n.k akazidharau Sasa Bundi kaingia bungeni!!!.

Muswada haujatulia,ccm muache nafasi kwa upinzani kupumua, ikikaba, mkikaba kabisa, kila kitu na sheria inaweza kuanzisha vikundi vya ugaidi. Simple logic. Waachieni watu watu waongee.

Muhimu kuwapa nafasi upinzani, mawazo tofauti, watu tofauti, muwasikilize mawazo yao.
 
Back
Top Bottom