Bulembo: Walioisaliti CCM wakati wa uchaguzi wajiondoe wenyewe

Ulimchoka wewe na nani acha kuingilia yasiokuhusu nyumbu wewe
hahahah mbona hakushinda pamoja na wizi wenu.... hehehe lyatonga anadaiwa milioni AROBAINI kwa ujinga wake... ccm imechokwa ndio na ndo maana zile sehemu zooote ambapo wananji wenye akili haijapita... kule wananji walipozubaa na kupenda ubwabwa maharagwe na vitenge +kofia za kijani waliibiwa kura na huo ndio ukweli
 
Bulembo anatamani sana angekuwa na ka shule labda ange lobby! Atabaia kupia domo na ubabaishaji! Hamna kitu!
 
of course sasa hivi tupo kitaifa zaidi sio kivyama target ni kuona Mama Tanzania inasonga mbele, najua haiwezi fikia hatua tukalingana vipato lakini kutopishana kwa kiwango kilichopo sasa cha umiliki wa ardhi, mapato na kuongezeka kwa ( per capital income) imbayo inaweza kuwa angalau afadhali na nafuu kwa watanzania walio wengi. #siasakandoTusongeMbele
 
MWENYEKITI%20wa%20Jumuiya%20ya%20Wazazi%20ya%20CCM%2C%20Abdallah%20Bulembo.jpg

MWENYEKITI wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM, Abdallah Bulembo, amesema, wote walioisaliti CCM katika uchaguzi mkuu uliofanyika mwaka jana, waanze kujiondoa mapema ndani ya chama hicho vinginevyo watang’olewa baada kufanyika tathimini ya uchaguzi.

Bulembo alisema kuwa chama hicho kipo mbioni kufanya tathimini ya kina kuanzia ngazi ya shina hadi taifani kuwabaini wasaliti waliochangia kukidhoofisha chama wajulikane na kwamba wote watakaobainika wataondolewa bila kuangaliwa vyeo na mahali walipo.

“Wapo watu ndani ya CCM walitusaliti katika uchaguzi uliopita hayo ni sehemu ya majipu mengi na lazima tuyatumbue, mtanuna sana lakini chama hakiwezi kuendelea kuwakumbatia wasaliti kama hao,” alionya Bulembo.

Akizungumza katika maadhimisho ya miaka 61 ya Jumuiya ya Wazazi, yaliyofanyika kitaifa mkoani Morogoro sherehe zilizohudhuriwa na viongozi wa kitaifa wa mikoa na wilaya wa chama hicho, juzi, alikumbusha kuwa wakati umefika wa kujitathmini.

Bulembo, alieleza kuwa uchaguzi umekwisha na sasa viongozi walioshinda kila mmoja afanye kazi ya kuwatumikia wananchi kwani serikali iliyopo madaraka inayongozwa na CCM imeonyesha uwezo wa kuwatumikia Watanzania lakini wakati hayao yakiendelea ni lazima CCM ifanye tathimini.

Alitoa tahadhari kuwa tathimini hiyo haitofanywa kwa chuki binafsi au kwa kumuonea mtu badala yake uwepo wa ushahidi wa kutosha wa kisaliti ndicho kigezo cha kushughulikia waliohusika.

Kadhalika aliwataka viongozi wa vyama vya upinzani pamoja na wanachama wao kuacha kutoa maneno ya kumkatisha tamaa na kumbeza Rais John Magufuli kwakuwa anaonyesha kasi nzuri ya utendaji kwa manufaa ya Watanzania.

Alisema kuwa jumuiya hiyo imeridhishwa na uchapaji kazi na kasi ya utendaji wa Rais Dk Magufuli,ikiwamo kudhibiti upotevu wa mapato ya serikali na kuvitaka vyama vya upinzani kumuunga mkono kwa kazi nzuri anayofanya.

Alisema Dk Magufuli pamoja na Baraza la Mawaziri kwa muda mfupi wamerudisha heshima ya nchi kutokana na kuwawajibisha watendaji wasio waadilifu na mafisadi bila kuwaonea haya hivyo anapaswa kuungwa mkono ili aweze kuwatumikia Watanzania.

Awali Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Mkoa wa Morogoro Meck Mdaku, aliwataka wanachama wa CCM kuvunja makundi kwani yanakidhoofisha chama na wakati mwingine kukinyima ushindi.

Alisema kuwa jumuiya hiyo imekiimarisha chama kuanzia ngazi ya shina hadi taifa na kwamba imeweza kuhakikisha chama kinapata ushindi katika uchaguzi uliopita.

Source: Nipashe
Abdallah Bulembo, amesema, wote walio kisaliti CCM katika uchaguzi mkuu uliofanyika mwaka jana, waanze kujiondoa mapema ndani ya chama hicho vinginevyo watang’olewa baada kufanyika tathimini ya uchaguzi.

Sio waliosaliti tu na mpaka walioiba kura mpaka wakakosea hesabu na kuonekana CCM ni chama cha vituko. Wale wote walioshiriki kuchafua uchaguzi Zanzibar baada ya CCM kushindwa na watunza takwimu za kura wakati wa marejeo ya uchaguzi uliosusiwa na asilimia 80% ya wazanzibari na wakaja na takwimu za ajabu na vichekesho vya asilimia 91.4%
Wewe ulikuwepo zanzibar na ulishuhudia yaliofanyika.

Bwana Bulembo na JECHA, licha ya kuutukanisha uislamu mnahitajika tena kurudia hijja yenu ya kinafiki mlioifanya. Alhajj hawi muongo wa kupindukia, mnafiki,mfitinishaji nampenda dhulma wa kupindukia kama nyinyi.Shame..Shame kuit wa AHajj labda wa kuhiji Dodoma
 
Napenda sana kurudia maneno haya; "Viongozi na wana ccm wengi akili zao mara zote hudhani kua Tanzania ndio ccm na ccm ndio Tanzania, hadi mawazo haya ya kijinga yakitoka vichwani mwetu ndipo tutakapo piga hatua ya kimaendeleo" Hivi Bulembo anamwona nani ADUI kati ya hawa, wasaliti wa chama chake wakati wa uchaguzi? (Bila shaka hapa anawalenga wafuasi wa Lowassa) na wale walifisadi nchi (Mfano wa hiyo scandal ya Limuli) nani hasa wanatakiwa kuchukuliwa hatua KALI!?
 
Back
Top Bottom