Bukoba: Mke wa Mwenyekiti auawa na kijana aliyemsaidia kwa kumpa hifadhi nyumbani kwake

Rare Sapphire

JF-Expert Member
Jul 24, 2021
576
1,626
Kishobo Bukoba vijijni, mtaa wa Nyamisheni National Housing, kumetokea tukio la kikatili ambapo Paskali Kagwa aliyepewa hifadhi nyumbani kwa Mwenyekiti wa eneo amuua na kumbaka Hadija ismail (29) mke wa mwenyekiti na kutokomea kusikojulikana.

Siku ya tukio Paskali alimpiga marehemu na kitu kizito kichwani na kisha kumbaka, ambapo baada ya kutekeleza tukio hilo alitoka nje ya nyumba akiwa mchafu na majirani kumuuliza kulikoni, mtuhumiwa aliwajibu alikua akifanya kazi ndani ambapo alirudi ndani akabadilisha nguo na kutokomea kusikojulikana.

Watoto wa marehemu waliporudi kutoka shuleni walimkuta amelala chini ndipo wakaita majirani waliokuta tayari Hadija alikuwa ameshafariki.

Kutokana na taarifa za polisi Paskali amekuwa akitafutwa tokea mwezi Novemba, 2022 na kuwaomba wananchi kushirikiana na polisi kufanikisha kupatikana kwa kijana huyo.

Siku ya tukio Paskali alimpiga marehemu na kitu kizito kichwani na kisha kumbaka, ambapo baada ya kutekeleza tukio hilo alitoka nje ya nyumba akiwa mchafu na majirani kumuuliza kulikoni, mtuhumiwa aliwajibu alikua akifanya kazi ndani ambapo alirudi ndani akabadilisha nguo na kutokomea kusikojulikana.
Utaalamu gani umetumika kuthibitisha kuwa tendo la kubaka lilifuata baada ya kifo na siyo kinyume chake
 
Dunia ya leo ya K za mafungu mtu unabakaje?? Kama wa huko Kagera wala hawana hiana. Angeongea vizuri na Mama Mwenyekiti angekuwa anajilia vyake kwa kujinafasi kabisa.
 
Kuna mambo mengine ukiyasikia unaishia kusikitika tu, yaani mtu mwingine anaingia jela kwa kosa ambalo halielezeki.

Hatari sana
 
Back
Top Bottom