Budapest Memorandum: Ulaghai wa kihistoria Warusi waliowafanyia Marekani, Uingereza na Ukraine

Vipi kuhusu uvamizi wa Crimea 2014?
Kama unapenda kujifunza na kujielimisha, hii itakusaidia. Crimea imekaa kimkakati zaidi yaani kama wamagharibi walivyolazimisha muungano wa Tanganyika na Zanzibar!

Why Crimea is the key to the Ukraine war​

Crimea was a vital strategic possession of the Russian Empire following its capture from the Ottomans in 1783. Britain and France went to war in 1854 to try to dislodge the Tsars from Crimea.

If Putin wants to restore Russia to its status as a leading European power, something that it achieved under the rule of Peter the Great and Catherine the Great, then he needs Crimea.

One reason why Crimea is so important is that it hosts the natural harbor of Sevastopol — the only deep-water port on Russia’s Black Sea littoral. (The ports of Sochi and Novorossiisk are shallow and require ships to moor offshore.)

Without Sevastopol, Russia would not have a home for its Black Sea fleet, which it uses to project power into the Mediterranean — and to wage war in Syria.

Huo sio ukweli, Ukraine haijawahi kuwa na utaratibu wa viongozi kubadilishana madaraka kati ya Pro-west na Pro-Russia. Viongozi wote wa nyuma waliotangulia kabla ya Viktor Yanukovych hawakuwa na upande wowote, walikuwa neutral. Viktor Yanukovych aliyechaguliwa mwaka 2010 ndiye aliyeanzisha vurumai za Pro-Russia na Pro-Russia West kutokana na kuwa fisadi aliyepitiliza na maslahi binafsi makubwa ya biashara huko Russia.
Ukimtoa Leonid Kravichuk ambaye ndo raisi wa kwanza 1991 aliyemfatia ni Leornid Kuchuma 1994 ambaye alitawala mpaka 2004 huyo unaemsema kuwa ni pro-russia viktor Yanukovych alikuwa ni prime minister kwenye serikali yake na mpaka kipindi Kuchuma anamaliza mda wake alikuwa anamsapoti huyo Viktor Yanukovych na chama chake kama mrithi wa kiti cha uraisi cha ukraine unazungumzia ufisadi huyo kuchma mwenyewe alikuwa na skendo za ufasadi mkubwa tu.
 
Sababu waliyotoa Russia ya kuivamia Georgia mwaka 2008 ni madai ya kwamba serikali ya Georgia ilikuwa ikifanya mauaji ya kimbari"genocide" dhidi ya South Ossetia ambao walikuwa waasi wanaotaka kujitenga kama kule Donbas.
Ilikuwa lazima watoe sababu kama hiyo unafikiri watakaa mbele ya kamera nakusema wanaivamia kwasababu ilitaka kujiunga na NATO. Tukirudi tu kwenye huu uvamizi wa sasa Ukraine putin si alisema anavamia Ukraine kwasababu anataka kuondoa Nazi ideology ambayo inapelekea Genocide kwa raia wa Russia waishio Ukraine wewe unafikiri ni kweli?

Ukifatlia Historia wa hayo mambo na kufanya uchambuzi basi hupati shida kuelewa motive ya hayo yote
 
Na wewe ni mmoja wa victims walioathirika na hizo propaganda za Putin za kudai kuwa Marekani inataka kuiangusha Urusi. Iwapo Marekani ingekuwa inataka kufanya hivyo, kwanza isingesimamia hiyo Budapest memorandum kuhakikisha silaha zote za Nyuklia zinakwenda Urusi na kuiacha Ukraine haine Kitu. Pili, Marekani ilikuwa na takriban miaka kumi za kuingusha kabisa Urusi yote baada ya kuvunjika kwa USSR. Badala yake katika kipindi cha kuanzia 1994 hadi 2004 Marekani iliisaidia sana Urusi kuimarisha uchumi wake bila vikwazo vyovyote; Mpaka sasa hivi Urusi inadaiwa fedha nyingi sana na Marekani ilizokopeshwa kwa ajili ya kujenga uchumi wake. Elewa hapa kuwa inadaiwa pesa ilizokopa (kama Tanzania inavyokopa), siyo pesa za kuuza hati fungante kama ambazo Marekani inadaiwa.

Tatizo la Putin ni nia ya kung'ang'ania madaraka tu, kwani kosa kubwa la Ukraine na Georgia limekuwa lile la kufanya uchaguzi na kubadilisha viongozi. Huo unakuwa ni mfano mbaya sana mlangoni mwake ambaye haamini utamaduni wa kubadili viongozi; hawezi kuishambulia Belarus mpaka pale watakapobadilisha rais
Jamani jitahidini kusoma historia,kama mambo yangekuwa rahisi hivyo kama unavyosema basi USA asingehangaika kuisambaratisha USSR.
Russia unaitesa USA na UK toka miaka ya Joseph Stalin.
 
Kuvamia nchi jirani siyo option. NATO ilikuwa na uwezo mkubwa sana wa kuitawanya Urusi katika kipindi cha kuanzia mwaka `1993 hadi 2004 kwani ilikuwa na control kubwa sana juu yake lakini haikufanya hivyo, badala yake ikajikita katika kuisaidia Urusi ili isimame imare tena, halafu baada ya hapo eti ndipo uadui uanza kama Putbi hakuwa na usongo wa ndani siku hizo zote?

Kitendo cha kuivamia Ukraine hakijasaidia lolote kwenye maslahi ya nchi yake bali ndipo ameikaribisha NATO zaidi mlangoni mwake huku vijana ambao niyo nguvu ya kesho ya taifa wakiwa wanakimbia nchi. Sasa hivi Putin anajivunia wale wazee wa zamani waliokulia ndani ya Soviet Union na watu wa vijijini wanasikiliza habari kwenye TV ya Taifa tu. siyo generation mpya inayoishi kwenye majiji kama Moscow na St Pettersberg.
Hicho kipindi cha 1994-2004 huyo USA alimsaidia nini Urusi??,hebu fafanua.
 
Finland na lithuan wamejiunga NATO na majiran wakaribu wa Urussi kwanini hajawashambulia
Tanzania tunazungukwa na Nchi 8 katika pande zote na Zanzibar ni ya 9 je kiusalama na kiuchumi katika hizo Nchi 9 ni yupi ambaye ni threat kwa Tanzania???
Hivyo kwa Russia kwake aliona Geogia na Ukraine ndio threat kama watakuwa kwenye muungano wa NATO.
 
Urusi haiwezi kuishambulia Finland kwa sababu tangu uvamizi wa USSR kwa Finland mwaka 1940 uliozua Winter War Finland imekuwa ikijiandaa kikamilifu kivita na Urusi wakati wowote.
We jamaa unavituko,sasa kama haogopi hawezi kuvamiwa why kukimbilia kujiunga na NATo?
Yani Europe nzima & USA zote zimuogope Urusi mpaka waunde umoja wa kujihami dhidi ya Russia halafu Finland pekee ndio awe mwambo kuliko hao au sio??
 
Tanzania hapa una kisingizio gani wakati mna kila kitu. Visingizio hivi vya kijinga vitafanya Afrika ibakie kuwa kichekesho cha dunia milele.
Ni kweli vyote vipo katika ardhi yako lakini vyote sio vyako.vitakuwa vyako kama una kiongozi aina ya Nyerere au Magufuli.
Mfano mdogo kabisa ni ule wa issue za madini vs Magufuli.
 
Yaani wewe ni mrusi zaid ya Gorbachev kweli kiashi cha kumwita puppet wa west? Usilete utani hapa
Je Boris Yelstin ambaye ndiye aliyesini ile Budapest Memorandum na ndiye aliyemchagua Putin kumrithi kuwa Rais wa Urusi naye alikuwa "Puppet wa west?"

Wewe kuwa na anti-west attitude kama ya Putin haina maana kuwa basi Putin yuko sahii
Kumbuka yelstin ameingia ndipo siasa za ubepari zinaanza kushika hatamu Urusi.Yelstin alizungukwa na matajiri wa kubepari wwngi wakiwa wenye mafungamano na West,alipoona maji yanazidi unga ndio akaamua ampe Mwamba putin adili nao.
 
Na wewe ni mmoja wa victims walioathirika na hizo propaganda za Putin za kudai kuwa Marekani inataka kuiangusha Urusi. Iwapo Marekani ingekuwa inataka kufanya hivyo, kwanza isingesimamia hiyo Budapest memorandum kuhakikisha silaha zote za Nyuklia zinakwenda Urusi na kuiacha Ukraine haine Kitu. Pili, Marekani ilikuwa na takriban miaka kumi za kuingusha kabisa Urusi yote baada ya kuvunjika kwa USSR. Badala yake katika kipindi cha kuanzia 1994 hadi 2004 Marekani iliisaidia sana Urusi kuimarisha uchumi wake bila vikwazo vyovyote; Mpaka sasa hivi Urusi inadaiwa fedha nyingi sana na Marekani ilizokopeshwa kwa ajili ya kujenga uchumi wake. Elewa hapa kuwa inadaiwa pesa ilizokopa (kama Tanzania inavyokopa), siyo pesa za kuuza hati fungante kama ambazo Marekani inadaiwa.

Tatizo la Putin ni nia ya kung'ang'ania madaraka tu, kwani kosa kubwa la Ukraine na Georgia limekuwa lile la kufanya uchaguzi na kubadilisha viongozi. Huo unakuwa ni mfano mbaya sana mlangoni mwake ambaye haamini utamaduni wa kubadili viongozi; hawezi kuishambulia Belarus mpaka pale watakapobadilisha rais
Mkuu, nilikuwa naamini ukiandika kitu basi ni madini matupu, ila sasa napata mashaka kama una ID moja au?

Baada ya US kufanikiwa kuiangusha USSR ndo fedha hizo unozisema zikaingizwa kwenye mfumo wa fedha wa Russia.

Kila kitu kikabadilika na hata küpelekea Urusi kuwa nchi ya wapigaji, ikiongozwa na magenge ya wahuni, wenye pesa na madon.

Watu kuuawa mitaani ilikuwa ni kawaida na khasa raia wa kigeni waliuawa sana, nchi ilikuwa haina order.

Mazee au Deep State wakawa wamechoshwa na mwenendo wa Boris Yetsin na kama wakumbuka Yetsin alikuwa mlevi wa kupindukia.

Putin alianza kusogezwa kwenye system ilosukwa upya na DS na ndo akaanzia kwenye manispaa, ukurugenzi wa FBI baadae FSB, waziri mkuu na kisha uraisi.

Wakati jina la Vladimir Putin latajwa kuwa afaa kuwa waziri mkuu yeye mwenyewe alikuwa vekesheni nchi moja hivi akiwa mkurugenzi wa FSB.

Hiyo yote unosema US alitoa fedha yaweza kuwa ni sawa lakini fedha hizo zilikuwa zaliwa na wapigaji, maana huşuna huduma muhimu kama afya zilizorota.

Urusi sasa hivi ina fedha au mali katika mabenki ya US na huko West lakini ni fedha zake na zikichukuliwa ili apewe Ukraine huo ni wizi.

Pia hawa West wakichukua fedha za Russia watasababisha mtikisiko kwenye mfumo wa fedha kwani China au Saudi Arabia na nchi zingine zaweza kuamua kuundosha mali zao huko, wadhani litakuwa jambo jema?

Walosoma alama za nyakati ni wazalendo wa DS ambao walikuwa kutambua kuwa Urusi inaweza kusimama kuwa taifa kubwa tena lenye uchumi imara, kijeshi, kiteknolojia na kujasusi duniani na ikachagua rasmi nchi rafiki Iran na China kuwa nchi mwenza kwenye malengo hayo.

Kuvamiwa kwa Crimea 2014 mama Angela Makel amesema kwamba mkataba wa Minsk ulikuwa ni kuwanunulia muda Ukraine ili waweze kujijenga kijeshi kwa silaha za NATO.

Je, ulidhani Urusi na majasusi wake wangeketi tu bila kumtahadharisha Putin kuwa wakati wowote Urusi yaweza kuvamiwa?

Hata kuvamiwa kwa Ukraine mwaka 2022 ilikuwa ni baada ya waasi wa Donbas ambao walitangaza kujitenga na Ukraine ambao kwa sera zao mbaya za kikatili walikuwa wakiwatesa na kuwaua raia wengi yaani majority ambao wazungumza kirusi na si kiukraine.

Walosaidia kuiweka madarakani serikali ya Kyiv ni haohao West lakini wakawa wakiwafumbia macho hao wanazi na kuachia wafanye mauaji.

Ndugu, tambua kuwa Dunia sasa ishageuka uwanja wa vita, kuna binadamu wenzetu wajiona wao ni super race na waweza kufanya chochote na wasiwajibishwe.

Bila shaka umeona yanotokea Gaza ni mfano tosha. Kanchi kamoja kanaamua kuleta zogo na kasiguswe bali ni kushikwa tu sikio.

Vita kubwa ni resources na ni lazima utoe resources hizo kwa watu sahihi ambao ni nchi za Magharibi wakiongozwa na Marekani.

Russia wasema hapana lazima kuwepo usawa katika kuitawala dunia maana neno New World Order limebadilishwa na kuwa Rules Based Order yaani kikundi cha nchi chache chajipa mamlaka ya kuamua mambo ya Dunia.

Nina mengi ya kuchangia lakini haya yatosha.
 
Ni kweli vyote vipo katika ardhi yako lakini vyote sio vyako.vitakuwa vyako kama una kiongozi aina ya Nyerere au Magufuli.
Mfano mdogo kabisa ni ule wa issue za madini vs Magufuli.
Afrika bado hatuna viongozi hata hao unaowataja hawana lolote wamefanya nini waliiacha nchi ikiwa maskini zaidi ya walivyoikuta wakati wanaingia madarakani.
 
1. Utajiri wa Afrika unaporwaje wakati tunaona kila nchi ya Afrika ikiwa inatawaliwa na waafrika wenyewe. Unaweza ukatupa uthibitisho wowote wa madai yako..?

2. Mimi nafikiri Ukraine ni nchi huru tu kama vile Tanzania, Kenya, Zambia nk, sasa kuna nchi duniani yenye haki ya kuichagulia nchi yoyote maadui au marafiki.

3. Unafahamu chochote kuhusu Budapest Agreement iliyohusisha mataifa ya Ukraine, Marekani, Uingereza na Russia.

View: https://youtu.be/uljs0MKzfic?feature
 
Back
Top Bottom