British Airways yafuta safari zote za kutoka, kuingia London kutokana na marubani kugoma

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,502
9,282
London, Uingereza (AFP). Shirika la Ndege la Uingereza (BA) limefuta karibu safari zote kutoka au kuingia Uingereza, baada ya kuibuka kwa mgomo wa kwanza wa marubani ambao umesababisha kuvurugika kwa mipango mingi ya wasafiri.

Mgomo huo wa Jumatatu na Jumanne unaohusu malipo na unaoendeshwa na Chama cha Marubani wa Ndege Uingereza (BALPA), umekuja baada ya mazungumzo ya miezi zaidi ya tisa kutopata suluhisho.

Katika siku ya kwanza ya mgomo huo, wasafiri wapatao 145,000 wanakabiliwa na kufutwa kwa safari za ndani na nje ya Uingereza, hasa katika viwanja vya Gatwick na Heathrow vya jijini London.
Shirika hilo la ndege, ambalo linamilikiwa na kundi la International Airlines Group na ambalo linaendesha karibu safari 850 kwa siku nchini Uingereza, limesema halikuwa na njia mbadala zaidi ya kufuta safari karibu zote.

"Kwa bahati mbaya, kukiwa hakuna taarifa kutoka BALPA ambayo ndiyo ina marubani waliogoma, hatukuwa na njia ya kubashiri ni watu wangapi wangekuja kazini au ni ndege gani zinaweza kusafiri, bali kufuta safari kwa karibu asilimia 100," BA ilisema katika taarifa yake.

Shirika hilo lilisisitiza kuwa bado lina nia ya kurejea kwenye mazungumzo lakini umoja huo -- ambao unataka mgao mkubwa zaidi katika faida ya kampuni hiyo ya usafiri -- unaituhumu BA kuwa haitaki kufanya majadiliano.
 
"linaendesha karibu safari 850 kwa siku nchini Uingereza, limesema"...mmh Tznia yetu nikubwa ×3 kijogorafia kuzidi uingereza.....ATCL kwa siku ifikishi hata safari 10 tu......duh God is not fair.....
 
Back
Top Bottom